February 3, 2020
Toronto, Canada
Mh. Zitto Kabwe mazungumzo exclusive na chaneli ya LCTV ya Canada
Katika ziara yao Mh. Zitto Kabwe na Nassor Mazrui wanatarajia kuzungumza na jumuia ya kimataifa kuhusu siasa za Tanzania. Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe, amechkua fursa hiyo kujibu shutuma za Bunge la Muungano na maswali kuhusu suala la kutuma barua Benki ya Dunia ili kusitisha mkopo wa elimu kwa Tanzania . Maoni juu ya uraia pacha kama ACT Wazalendo wakichukua dola pia nafasi ya diaspora ktk ushiriki wake ktk siasa za Tanzania ili kuchagua wabunge na chama kinacho kubaliana na uwepo wa uraia-pacha.
Takwimu zinaonesha waTanzania waliopo nje kwa mwaka wanapeleka miamala inayofikia dola 480 milioni za Kimarekani sawa na mchango wa zao la korosho linaloongoza kwa kuchangia dola milioni 500. Hivyo diaspora inatakiwa isitengwe kuwa wao siyo raia wa Tanzania kutokana na mchango mkubwa ktk mapato ya fedha za kigeni kwa Tanzania.
Source : Lete Chai TV