Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Kwani kutoendesha ibada ya mazishi ndio kuhukumu? Kuna kitu hamuelewi hapa. Kanisa Katoliki hutoa huduma za kiroho kwa Wakatoliki tu. Kwa mujibu wa taratibu za kiroho, Ole Mushi hakuwa Mkatoliki
Kwakua alipinga walaka?
 
Kuwepo kwa habari hii ni dalili tosha kuwa marehemu amepungukiwa. Angekuwa hajapingukiwa, isingekuwa habari
Aliepungukiwa ni kanisa kwa kumpiteza kondoo wake wala marehemu hana haja nao. Imeandikwa, mchunga kondoo mwenye kundoo kumi, akimpoteza mmoja, ataawacha wale tisa na kumtafuta yule aliepotea mpaka ampate. Akipatikana atamkumbatia na kumrejesha kundini na wenzie.

Soma maandiko tajiri. Achana na utapeli wa ukatoliki wa kisasa.
 
Ni kweli mkuu kanisa Katoliki hailimtengi mtu ila halilazimishi mtu kulifuata. Kama alijitenga akiwa hai, kwa nini kanisa limlazimishe akiwa ameshakufa na bila kujua sababu ya yeye kujitenga huko.

Suala la Waraka inaweza isiwe sababu ila maisha yake ya ukatoliki, ndoa n.k hatuyajui yanaweza kuwa ni sababu pia.

Wapo wengi mfano bilionea Mrema wa Arusha (Ngurudoto na Nauru Spring) nae hakupata ibada ya mazishi ya kanisa Katoliki. Nyie mnaosema haina umuhimu wowote kwa nini mnalalamika na kuleta uzi?

Ile ni Ibada/ Misa ya kuonesha ushindi katika kuiishi imani katoliki (Ukristo) katika maisha yako hapa duniani. Kwamba "Nimevipiga vita vilivyo vizuri mwendo nimeumaliza na Imani nimeilinda."
 
Kanisa katoliki ni ovyo mnooo
 
Hapa ndio dini yangu huwa inanichosha kabisa!

Hata wakatae kumsalia, what difference does it make to a dead man?🧟‍♂️ AbsoFREAKINGlutely NONE!!!!
Sio siri mimi nimebakia kuwa Mkatoliki kwa ajili wa watoto tu ila kiuhalisia hili dhehebu sio kabisa
 
Hapa ndio dini yangu huwa inanichosha kabisa!

Hata wakatae kumsalia, what difference does it make to a dead man?[emoji3446] AbsoFREAKINGlutely NONE!!!!
Ulichokiona ndio difference yenyewe.
Huwezi kupinga ule waraka ambao umenyooka vile na umejikita kwenye mapugufu ya mkataba wa kibwege kabisa achilia mbali kwamba waliotoa ni jopo la viongozi wako wa kiroho alafu watu wakuchekee...
Bandari ni future ya Watanzania wote na vizazi viijavyo.
Thadei alikosea sana simuhukumu ila atapambana na Muumba wake.
Usaliti, Roho mbaya ..Ubinafsi ndio umeleta haya yote.
Waliokula hela ya Dp wanajijua.
Nasimama na Viongozi wangu wa kiroho always...siwezi kusimama kamwe na wanasiasa uchwara na wezi NEVER.
 
Sasa kama marehemu hana hoja na Kanisa, malalamiko yaliyomo kwenye uzi huu yanahusu nini? Au ni kiherehere cha watu kujidai kumtetea marehemu wakati yeye hana hoja na Kanisa? Tangu lini ukaona Kanisa Katoliki likashughulika na kondoo aliyeamua mwenyewe kwa akili zake timamu kujipoteza?
 
Kama ni kweli basi kanisa limepotoka kwani wao ni mungu!
 
Kwani wao ndo wenye uamuzi wa nani aingie mbinguni au hapana. Wanaona jamaa mchochezi kama TL alivyokuwa anasakamwa? Waache utoto
Kwani unaombewa ili uingie mbinguni. Hizo taratibu zimeshawekwa. Ukikosea, utahukumiwa kidunia, hata kama umekufa, ili liwe fundisho kwa walio hai.
 
Hakuwa na pesa. Kama anapesa maaskofu wangaligombea mwili kuuombea. Au nasema uongo wadau?
 
Kama ni kweli basi kanisa limepotoka kwani wao ni mungu!
Mnachanganya, nani kasema kanisa ni Mungu. Utaratibu lazima ufuatwe. Mlio hai ndio mjifunze. Kwani mtu akihukumiwa kuua, adhabu anapata yupi? Maiti, funzo kwa walio hai.
 
Duh aiseee wamezingua sana
Mkuu ni sahihi kabisa, watu ni wanafiki sana humu. Utakuta mtu anaanzisha uzi wa kupinga kushiriki jumuiya akidai zinawachangisha hela, halafu mtu huyo huyo anakuja kuanzisha uzi kuwa Kanisa linazingua kukataa kumzika marehemu. Sasa kama wewe unahitaji huduma, kwa nini ukiwa hai hautaki kushiriki na wenzako? Ukiamua kujitenga hutakiwi kuja kuomba huruma siku watakapokukana kuwa sio mwenzao. Yaani wakiwa wanakuhitaji unawakana, wewe ukiwa unawahitaji wakikukana iwe nongwa? Kimsingi unatakiwa kujua umejitenga mwenyewe, wala hujatengwa
 
Hakuwa na pesa. Kama anapesa maaskofu wangaligombea mwili kuuombea. Au nasema uongo wadau?
Kuna msiba uliokuwa na hela kama wa Ruge Mutahaba kwa siku za hivi karibuni? Muulize ndugu yake yeyote kama alizikwa kikatoliki. Ukiishi bila ndoa umejitenga na Kanisa, utazikwa na wahuni
 
Ni kweli, watu wanasema mara yeye maiti, wengine pigo la mwisho. Somo fuata taratibu za mifumo tuliyojiwekea, kokote kule. Kama hajui hata taratibu za kupinga kanisa, yamkini hakuwa anaenda kanisani kama mimi. Kuzika ni ibada, mbona kama sio ibada hakuna dhehebu linaenda mochwari kubeba miili isiyo na ndugu wakazike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…