Wabongo bhana... yaani mnaokoteza tu tweets from Anonymous Members na hiyo kwenu ndo inakuwa stori?!
Tatizo lenu mnadhani kila kinachokuwa posted online basi ni taarifa sahihi bila kujishughulisha kujua credibility ya source mnazotumia!!
Matokeo yake, source uliyoweka, ya mtu anayejiita Spartacus, anataka kuwaaminisha watu aina yako kwamba Trump alikuwa anazungumzia mRNA ya Bill Gate, chanjo ya COVID-19!
Lau kama ungetumia hata dakika 2 kutafuta original source ambayo ni MNBC, ungekuta screenshot aliyoambatanisha Spartacus, original clip ni hapa chini:-
Hapo utaona the original video ilikuwa uploaded YouTube on May 18, 2018 hata kabla ya hayo mambo ya COVID-19! Na ukisikiliza, utaona Bill Gate aliongea ama December 2016 or early 2017.
Basically, Bill Gate alikuwa anaongea na Wafanyakazi wa Bill & Melinda Gates Foundation, na mmoja wao alitaka kujua alimfahamu vipi Donald Trump kwa sababu, by the time, Trump ilikuwa ndo kwanza kachaguliwa kuwa rais!!
Gate alipokutana na Trump kwa mara ya kwanza mara ya kwanza ndani ya Trump Tower na mara ya pili alimtembelea White House. Mara zote hizo Trump alitaka kufahamu ikiwa chanjo ina madhara, na chanjo waliyokuwa wanaizungumzia hapo ni HIV Vaccines, na kwa maneno yake, Gate anasema---
Btw, hivi ulijaribu kutafuta na taarifa za Dr. Peter McCullough ambae clip yake imepachikwa baada ya maelezo ya Gate?!