Jaffo mnampa tu kiki hasizostahili....
Yule dogo hawezi kuwa Rais..kwanza hayuko smart enough kichwani, anafanya mambo kwa mihemko, hata haiba ya Urais hana.. Kwa kifupi hafai
Rais ajae ni lukuvi japo hana elimu. Sub yake ni kabudi alafu mwigulu ni shabiki nje ya uwanja...
Kwa sheria za mafao ya marais Kumchagua Rais chini ya miaka 55 ni janga kwa Taifa.
Kuna Siku tutalea mabilionea 10 kwa wakati mmoja waliojilimbikizia fedha kupitia Ikulu kwa mgongo unaoitwa wastaafu.
Kuwahudumia kwa mwaka itakua kama kuhudumia Wizara mbili.
Afrika tunakua maskini kwa sababu ya umaskaini wa mawazo yetu wenyewe.
Eti mtu anasema sasa ni zamu ya vijana bila kutuambia kuwa faida yake nini na hasara yake kwa taifa nini ?
Marekani na nchi zilizoendelea sio wajinga kuchagua marais wenye umri mkubwa. Umri mkubwa unaondoa ubinafsi. Upendeleo ,ufuska ,uhuni ,wizi, urafiki ,kuchaguana kwa sura na kuangalia maumbile ya wadada n.k.
Vijana wasubiri umri wao utafika na akili zai zitatulia watapata urais.
2021 Lukuvi, Mwinyi, Majaliwa, Lisu, Membe ,Lowasa,Wasira, Mwakyembe n.k wanatisha kuchukua Form na kugombea . Urais sio kubeba zege.