PM Majaliwa: Watanzania tunaomba mtuamini (kuhusu uwekezaji Bandarini)

Kama anafoka hahaha hii issue ya bandari ndugu waTanganyika halijakaa vizuri,muangalie Majaliwa anavyoongea kama analalamika hivi na panic juu na anaonekana kakubaliana na malalamiko ya wananchi maana anaishie kusema serikali umemsikia na itayafanyia KAZI ina mana wananchi tuko sahihi hivyo ndugu zangu tuendelee kukomaa mpaka kieleweke maana tulikuwa tunauzwa kijinga
 
DPW haishi kuwekeza hapo bandarini tu. Ulimwengu wa kisasa maana ya bandari imebadilika kabisa sio ile ya miaka ya nyuma.

Sasa tunaongelea the whole logistic chain tukimaanisha bandari. Huyu DPW anamiliki mzigo huko Congo na Rwanda pia anamiliki dry port huko huko Kigali.

Kwa ufupi anamiliki mzigo unapotoka na anataka amiliki sehemu ya bandari unapopita na ana miliki soko la huko unakoenda.

Maana nzima ya bandari imebadilika, umiliki wa bandari haushii katika kupakua makasha na kuyapakia melini hujumuisha masuala mazima ya logistics.
 
Huu mkataba unaenda kutengeneza "Radicals" wengi sana. Naona serikali inacheza na mioyo ya watu.

Kama kilichosainiwa ni IGA, imekuwaje huyo mwekezaji ajitokeze kwenye makubaliano ya nchi na nchi?

Makubaliano ya nchi na nchi yanawezaje kusainiwa na mwekezaji? PM anataka kutudanganya wazi wazi.
 
Naomba ufafanuzi zaidi ....Sijaelewa kabisa unalenga nini kwa maelezo hapo juu kuhusu bandari na DPW.
 
Kumwamini Majaliwa tenaaa?!!!!! aliyetumbia kuwa Magufuli yupo na afya njema na anachapa kazi kumbe mzee wa watu....
 
Ni sawa sawa na Mtoto asiyejielewa analazimishwa kunywa uji, hatuutaki.
 
Amesema mkataba ni miaka mingapi?

Na vipi kuhusu maslahi ya nchi kasema ni yapi?
 
Watu wasioona aibu kama huyu kusema uongo hata wakati akishajulikana kuwa ni mwongo huwa sijui wanawaza nini.

Huyu wakati huu alitakiwa akae kimya kabisa. Maneno ya huyu mtu yanapomtoka kinywani hayana maana yoyote.

Mtu aliyedai kiongozi wa nchi yupo ofisini anachapa kazi, huku akijua kiongozi huyo alishakufa, mtu wa aina hiyo utamwamini kwa jambo lipi tena?

"Watu waiamini serikali" wakati wakiona katika maandishi wananadisha mali za waTanzania. Hii ni akili ya namna gani hii?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…