Pole mzee Malecela, amepoteza watoto wanne!

Pole mzee Malecela, amepoteza watoto wanne!

Sasa na Dr Mwele alikuwa anagombania? Alikuwa amekosa nini?
Afrika kumejaa wivu na roho mbaya.
Kuna ndugu zangu fulani hawapatani kwa sababu baba yao alimpa bunduki kaka yao.
Wanasema kwa nini ampe yeye? Bunduki ipo moja watoto wapo tisa na wana uwezo kifedha lakini wanagombea bunduki tuu na mpka Leo hawapatani.
 
Kale ka mifupa na baadhi ya watoto wa mzee walimpiga sana vita lemutuz asitambulike kama mtoto wa mzee Malecela, lemutuzi siku zote aliandika kwa uchungu na kila kitu alikiweka wazi.

Lemutuz hakupata upendo wa wazazi wake mpaka alilelewa na baba yake mkubwa.

Alipambana mwenyewe kwenda Us.
Mzee alikuwa akimtambua kama mwanae na ni mtoto wake pekee alomfanana kuliko wote.
Ila mzee kuna nyakati alikuwa akimsaidia tho sio mara nyingi.

Kuna siku zamani sana mzee alimuandikia balozi wa malawi kama sikosei akimuomba amsaidie mwanae lemutuz. Hiyo barua iko insta kwenye pg yake.

Kale ka mifupa siku zote ni kumsema lemutuz sio mtoto wa mzee hapo lemutuz ataleta ushahidi wa vitu ambavyo mzee alimsaidia kama mwanae.

This world sometimes is stupid mtoto anazaliwa bila kosa lolote anateseka anatengwa kwa makosa ya wazazi.

Baada ya mafanikio lemutuz aliamua kujipa. Raha maana hakupata raha yeyote ya familia.
Mkiona anajilia raha mnaanza kupiga kelele mnajua alitoka wapi?
Baadhi ya watu hata humu jf mnatakiwa kusoma ukweli wa lemutuz kwenye pg. That's why aliamua kujipa raha mpaka kifo chake kinamkuta alikuwa anatoka batani.

Nadhani kale ka mifupa kameona jana baba yake alivyo muita lemutuz mwanae.

Tujifunze kutoka kwa lemutuz, kamwe wamama usizae na mtu ambae hataki kuzaa na wewe. Mtoto ataishi maisha ya shida sana.

Rip king.
Mimi ushauri wangu:

Wazazi, iwe baba au mama au nyote msipungukiwe upendo kwa watoto wenu. Sijui katika uislam, lakini katika ukristo, soma vitabu vyote na kitabu kikuu cha biblia, hakuna hata sehemu moja ilipoandikwa kuwa mimba ni dhambi au kupata mimba ni dhambi au mtoto wa aina fulani ni dhambi. Dhambi ni uzinzi, mimba siyo dhambi, mtoto siyo dhambi. Bali tunaambiwa wapendeni watoto wenu wasije wakakata tamaa. Tubu uzinzi wako, kisha katimizi wajibu wako kwa mwanao.

Na kwa watoto waliofanywa wa hadhi ya chini kwa sababu ya historia ya kupatikana kwao, msihuzunike na kujilaani, mmekuja Duniani kwa mapenzi ya Mungu. Jibidisheni, pambaneni, msikose kutimiza wajibu wenu wa kuwaheshimu wazazi wenu.
Kumbukeni Mungu amewashusha wenye enzi katika viti, akawakuza wanyenyekevu. Mungu wetu huwabariki zaidi wanyenyekevu waliodharaulika ili kuwafedhehesha wenye nguvu waliojawa kiburi.

Jiulizeni, mfalme Sulemani alizaliwa kwa mama yupi? Obedi baba yake Yese, Yese aliyekuwa Baba yaje Daud, alikuwa wa mama Yupi? Maadam umezaliwa, ni binadamu kama wengine, mengine yatategemea juhudi zako na baraka za Mungu.
 
Yaani ndo hapo sasa,wakati kila kitu kitabaki duniani,huyo Anne nae ataliacha hilo jumba,hata wanae wataliacha.Inahitajika busara kubwa sana na Hekima katika kuona mali zote zitabaki tu.Utu kwanza mali baadae.

Lakin Anne nae si ana pesa tu nzuri
 
Huyo mama alimtoa Tatu Ntimizi,watu wote walijua Tatu Ntimizi ndo ataolewa,hadi mzee alibadili dini na kujiita Jumanne cof of Tatu,ila Anne kapambana mpaka akaolewa yeye.Mke wa ndoa nae aliugua kimaajabu alitibiwa mpaka Kigoma huko enzi zile Makamba ni mkuu wa mkoa Kigoma. Ikute mama wa watu michepuko ndo walimpiga juju. Ila mzee nae alikuwa zip wazi enzi zake ,mweh..
Wapi huyu Mama(ex-soldier) Tatu Ntimizi?
Nakumbuka Mzee alidata sana kwa huyu Mama.
 
Tujifunze kutoka kwa lemutuz, kamwe wamama usizae na mtu ambae hataki kuzaa na wewe. Mtoto ataishi maisha ya shida sana.

Rip king.

Pana Interview yake moja kule you tube akihojiwa na Channel ya Global anasema wazi wazi hata Mama yake mzazi alikuwa mbinafsi sana na hakumpa kipaumbele cha kumlea ndiyo akaishia kuhangaika mwenyewe.

Inaonekana Mama yake Mzazi na yeye alilipiza kisasi cha kuachwa na Mzee kwa kutomlea vizuri mwanae.Ni kama Le mutuz tangu utotoni hakupata kabisa malezi na mapenzi ya Wazazi wake vile alikuwa anategemea,kuwa kwake mtoto wa nnje ya ndoa kuliambatana na kukosa mapenzi ya dhati ya Wazazi wake.Japo mwisho wa interview alikiri at some point waliyamaliza na Baba yake kwa kuombana radhi.
Apumzike kwa Amani.
 
OIF.IZbuKpy8ek6Z9mtXRIbb9Q
Inauma!

Mtu akiwa wa umri, anategemea kimaisha watoto kumzika baba au wazazi.

Kwa mzee Samwel Malecela imekuwa kinyume.

Kwa kushuhudia msiba wa mtoto wake wa nne, imesikitisha sana.

Nimehudhuria shughuli za kumuaga Le Mutuz, Le Mbebez, William Samwel Malecela.

RIP Le Mutuz
Nionapo amani kama shwari
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu
 
Afrika kumejaa wivu na roho mbaya.
Kuna ndugu zangu fulani hawapatani kwa sababu baba yao alimpa bunduki kaka yao.
Wanasema kwa nini ampe yeye? Bunduki ipo moja watoto wapo tisa na wana uwezo kifedha lakini wanagombea bunduki tuu na mpka Leo hawapatani.
Hiyo ni chuki tu na roho mbaya. Inaelekea mama yao na Dr Mwele alikuwa na chuki na nongwa
 
Mimi ushauri wangu:

Wazazi, iwe baba au mama au nyote msipungukiwe upendo kwa watoto wenu. Sijui katika uislam, lakini katika ukristo, soma vitabu vyote na kitabu kikuu cha biblia, hakuna hata sehemu moja ilipoandikwa kuwa mimba ni dhambi au kupata mimba ni dhambi au mtoto wa aina fulani ni dhambi. Dhambi ni uzinzi, mimba siyo dhambi, mtoto siyo dhambi. Bali tunaambiwa wapendeni watoto wenu wasije wakakata tamaa. Tubu uzinzi wako, kisha katimizi wajibu wako kwa mwanao.

Na kwa watoto waliofanywa wa hadhi ya chini kwa sababu ya historia ya kupatikana kwao, msihuzunike na kujilaani, mmekuja Duniani kwa mapenzi ya Mungu. Jibidisheni, pambaneni, msikose kutimiza wajibu wenu wa kuwaheshimu wazazi wenu.
Kumbukeni Mungu amewashusha wenye enzi katika viti, akawakuza wanyenyekevu. Mungu wetu huwabariki zaidi wanyenyekevu waliodharaulika ili kuwafedhehesha wenye nguvu waliojawa kiburi.

Jiulizeni, mfalme Sulemani alizaliwa kwa mama yupi? Obedi baba yake Yese, Yese aliyekuwa Baba yaje Daud, alikuwa wa mama Yupi? Maadam umezaliwa, ni binadamu kama wengine, mengine yatategemea juhudi zako na baraka za Mungu.
Andiko safi sana kiongozi
 
Back
Top Bottom