Pole mzee Malecela, amepoteza watoto wanne!

Sasa na Dr Mwele alikuwa anagombania? Alikuwa amekosa nini?
Afrika kumejaa wivu na roho mbaya.
Kuna ndugu zangu fulani hawapatani kwa sababu baba yao alimpa bunduki kaka yao.
Wanasema kwa nini ampe yeye? Bunduki ipo moja watoto wapo tisa na wana uwezo kifedha lakini wanagombea bunduki tuu na mpka Leo hawapatani.
 
Mimi ushauri wangu:

Wazazi, iwe baba au mama au nyote msipungukiwe upendo kwa watoto wenu. Sijui katika uislam, lakini katika ukristo, soma vitabu vyote na kitabu kikuu cha biblia, hakuna hata sehemu moja ilipoandikwa kuwa mimba ni dhambi au kupata mimba ni dhambi au mtoto wa aina fulani ni dhambi. Dhambi ni uzinzi, mimba siyo dhambi, mtoto siyo dhambi. Bali tunaambiwa wapendeni watoto wenu wasije wakakata tamaa. Tubu uzinzi wako, kisha katimizi wajibu wako kwa mwanao.

Na kwa watoto waliofanywa wa hadhi ya chini kwa sababu ya historia ya kupatikana kwao, msihuzunike na kujilaani, mmekuja Duniani kwa mapenzi ya Mungu. Jibidisheni, pambaneni, msikose kutimiza wajibu wenu wa kuwaheshimu wazazi wenu.
Kumbukeni Mungu amewashusha wenye enzi katika viti, akawakuza wanyenyekevu. Mungu wetu huwabariki zaidi wanyenyekevu waliodharaulika ili kuwafedhehesha wenye nguvu waliojawa kiburi.

Jiulizeni, mfalme Sulemani alizaliwa kwa mama yupi? Obedi baba yake Yese, Yese aliyekuwa Baba yaje Daud, alikuwa wa mama Yupi? Maadam umezaliwa, ni binadamu kama wengine, mengine yatategemea juhudi zako na baraka za Mungu.
 
Yaani ndo hapo sasa,wakati kila kitu kitabaki duniani,huyo Anne nae ataliacha hilo jumba,hata wanae wataliacha.Inahitajika busara kubwa sana na Hekima katika kuona mali zote zitabaki tu.Utu kwanza mali baadae.

Lakin Anne nae si ana pesa tu nzuri
 
Wapi huyu Mama(ex-soldier) Tatu Ntimizi?
Nakumbuka Mzee alidata sana kwa huyu Mama.
 
Tujifunze kutoka kwa lemutuz, kamwe wamama usizae na mtu ambae hataki kuzaa na wewe. Mtoto ataishi maisha ya shida sana.

Rip king.

Pana Interview yake moja kule you tube akihojiwa na Channel ya Global anasema wazi wazi hata Mama yake mzazi alikuwa mbinafsi sana na hakumpa kipaumbele cha kumlea ndiyo akaishia kuhangaika mwenyewe.

Inaonekana Mama yake Mzazi na yeye alilipiza kisasi cha kuachwa na Mzee kwa kutomlea vizuri mwanae.Ni kama Le mutuz tangu utotoni hakupata kabisa malezi na mapenzi ya Wazazi wake vile alikuwa anategemea,kuwa kwake mtoto wa nnje ya ndoa kuliambatana na kukosa mapenzi ya dhati ya Wazazi wake.Japo mwisho wa interview alikiri at some point waliyamaliza na Baba yake kwa kuombana radhi.
Apumzike kwa Amani.
 
Nionapo amani kama shwari
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu
 
Hiyo ni chuki tu na roho mbaya. Inaelekea mama yao na Dr Mwele alikuwa na chuki na nongwa
 
Andiko safi sana kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…