Mtu anapoajiriwa sehemu fulani anakuwa amejitoa kufanya kazi na nguvu na muda wake vinaelekezwa kwenye kazi. Mategemeo ni kuwa atapata kipato cha kutosha kuendesha maisha yake yaani kipato kinachotosha kwenye "basic needs zake" kwa ngazi yake. Lakini mara nyingi mambo hayako hivyo hasa katika nchi zetu. Katika nchi zetu kipata kinakaribia (note the word kinakaribia) kutosha basic kwa watu wa ngazi za juu. Siyo rahisi mtu kutumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Huwezi ukawa mtumishi full time na mfanya biashara full time. Pia haiwezekani TZ kila mtu akawa mfanya biashara. Tukiwa wote wafanya biashara wanunuzi watakuwa wake na nani. Hata kwenye nchi za wenzetu, majority ya watu ni wafanya kazi wa sekta mbalimbali. Wachache ni wafanya biashara. Ebu fikiria ofisi zote za halmashauri kila mtu ni mfanya biashara/mkulima. Wakiwa kwenye biashara huduma atatoa nani? Pia nimesoma watu wengi wakiongelea kupata kazi zenye maslahi kama vile uwezekano au urahisi wa kupata pesa za kuiba, kuhongwa, au illegal earnings. Kila mtu akilenga kupata kazi palipo rahisi kuiba tutajenga taifa gani? Inabidi tukazanie maboroshe ya mishahara kuliko hizi ndoto za kupata pesa kimkato. Mimi huwa nawashangaa wanaoponda walimu. Ni kweli mimi nilichukia saana ualimu. Nilipokuwa secondary na high school sikutaka kusikia kitu ualimu. Nilipoenda chuo nilichukuwa fani nyingine na baada kupata digrii niliajiriwa na wizara idara fulani. Kufika huko tulikuwa vijana sita, idara ilikuwa haina mtumishi wa diploma au digrii. Hapo idarani tulikaa muda mfupi wote tukaondolewa kwenda chuo cha idara kufundisha, cha ajabu tangu wakati huo sijawahi kufanya kazi nyingine zaidi ya kufundisha! Baadaye niliipenda hii kazi kwa sababu marupurupu yake halali unajitafutia (research projects & consulting) unajitafutia mwenyewe na zinalipa kuliko kungoja mwanya wa kukwanguwa (kuiba) na ukishikwa. unaozea jela.