Tetesi: Polepole na Dkt. Hassan Abbas wanawatisha watu wa media

Tetesi: Polepole na Dkt. Hassan Abbas wanawatisha watu wa media

Media ziko kibiashara mnategemea mteremko, jinga kabisa.Kipindi cha uchaguzi ni cha kufanya biashara unategemea media zitumie mb zake kutangaza pumba za chadema. Zameni mfukoni mtaona media zitakuja kwenu
Mungu aipe CCM uhai mrefu wa kuwa wapinzani mtashuhudia kila rangi
 
Kwenye biblia kuna mstari huu!

34 Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo,
35 akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa.
36 Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.
37 Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.
38 Basi sasa nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa,
39 lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.
40 Wakakubali maneno yake;
 
Jamani wanaJF, nimepenyezewa ubuyu hapa na source yangu moja hivi kwamba ktk matukio 2 ya chadema; mkutano mkuu na uchukuaji fomu kule Dodoma. Polepole na mwenzake Hassan Abbas wamekuwa wakivipigia vyombo vya habari simu ili kuvikataza kurusha hotuba za Lisu

Kuna audio ya Polepole nimesikilizishwa (japo source amegoma kuirusha kwambangu, hivyo sitoiweka hapa) na kuna namba ya simu ya Abbas na muda aliyopiga nimetajiwa.

Kama hii kitu ni kweli siyo uzushi, basi ni dhahiri shahili kwamba ccm na mawakala wao akina Abbas wana wasiwasi usio mithilika kiasi cha kukosa usingizi. Na hii inazidi kumpalilia njia Tundu Lisu

My take.
Kama Lisu ameshinda kifo cha risasi basi hata uchaguzi wa hila atashinda kwa kudra zake Mola. Amen!

Mkuu weka ushahidi
 
Kwa kuwa ni tetesi tusubili habari kamili vyombo vilivyozuiliwa.
 
Media ziko kibiashara mnategemea mteremko, jinga kabisa.Kipindi cha uchaguzi ni cha kufanya biashara unategemea media zitumie mb zake kutangaza pumba za chadema. Zameni mfukoni mtaona media zitakuja kwenu

Hata TBC chombo cha habari cha TAIFA?
 
Nyie chadema habari zenu zinarushwa na CCN, BBC na DW .
Sasa mnalalamika nini
Ni aibu kutamka maneno Kama haya vyombo vya habari ni vya wananchi so kila mtanzania anatakiwa kupewa nafasi sawa kwa vyombo vya habari kwa kuwa hivyo vyombo ni Mali ya umma si Mali ya mtu mmoja Ni Kodi ya watanzabia wote wanachama na wasio na chama.
 
Majungu na Propaganda.

Kuna MATAGA mwenzako nimemwambia mchana huu kuwa vyombo vya habari vinapigiwa simu na watu wa serikali kutishwa kuhusu kuwapa covarage cdm. Akaishia kusema kwani mimi nina access na watu wa vyombo vya habari, nikamuuliza kuwa hao watu wa media ni marehemu useme hatuwezi kuwa na access nao? Huo ni ukweli wa asilimia 100 kuwa ccm na serikali wanavitisha vyombo vya habari wasiwatangaze cdm. Hizo ni tabia za udictator uliokomaa.
 
Kuna redio moja apo Singida nimesikiliza taarifa yao ya habari ..Sijui kama utaendelea kurusha matangazo
 
Wakati mpo katika mihemuko ya kumpokea Lissu mngekumbushana kudai tume huru, kwa mfumo wa sasa kukitoa chama tawala madarakani ni kama kupaka rangi upepo
 
Weka uthibitisho wa authentic audio ambazo Polepole na Abbas wakitishia watu. Vinginevyo we ni mnafiki ambae unatafuta kick tu.

Watu waovu huwa wanaweka uovu wao hadharani? Wenye media wanakiri tabia hiyo. Hizo ni tabia za vyama vyote vilivyochukua utawala kutoka kwa wakoloni, huwa wana tabia ya kushuritisha vyombo vya habari kuwabeba, na kukandamiza vyama washindani wao.
 
Wekeni ushahidi juu ya Polepole na Abbas kutishia wamiliki wa vyombo vya habari. Tena muweke audio clip authentic jinsi wanavyotishia. Vinginevyo ni uzandiki.
 
Watu waovu huwa wanaweka uovu wao hadharani? Wenye media wanakiri tabia hiyo. Hizo ni tabia za vyama vyote vilivyochukua utawala kutoka kwa wakoloni, huwa wana tabia ya kushuritisha vyombo vya habari kuwabeba, na kukandamiza vyama washindani wao.
Vyama vya kiimla au una maana gani?
 
Back
Top Bottom