Polepole ni Mkwara mbuzi tu, anatishia nyau ila hana lolote

Kama umoja wa kitaifa ni kuwafumbia macho wahuni wanaopora rasilimali za Tanganyika basi ujinga umeshinda vita!
 
Polepole kasema rostam ni tapel na ni muhuni anaendesha genge la wahuni ccm tena kwa ushahid njo hapa ukanushe maneno yake na sio uanze kumjadili polepole.
Chawa mkubwa wa Rostam ni Hussein Bashe!! Hawa wahuni wametumia fedha nyingi sana kuwaangusha wabunge wasio “Chawa” kwenye kura za maoni akiwemo Kingwangallah! Na hizo fedha zimetokana na Ufisadi ndani ya wizara ya kilimo uliofichuliwa na Mpina bungeni kuhusu vibali vya sukari.
 
Hana impact ndio maana CCM imempuuza, wanajua ni sisi tu ndio maana hakuna kiongozi anayemwongelea. Kimsingi ni jinga ht hajajipima ya kwamba CCM ni jitu kubwa hawezi ht kulitingisha
 
CHADEMA hakunaga msimamo wala maono. Leo Polepole shujaa wenu ambaye alishiriki kuwaminya kwa miaka karibu 6.
Ndiyo uzembe wa CHADEMA huo. Hata Lowassa waliyemnanga kwa ufisadi walimsafisha.

Kazi yao kutakatisha wanasiasa waovu
 
Kuwa na msimamo mazee. Tumpuzee au tumfuatilie? Mbona unamwanzishia nyuzi kama ni wa kupuuzwa?
 
Maskini wewe na familia yako. Hela kidogo tu ukipata unanunua bando kuja JF kuichamba Serikali, wenzio wanaingiza kwenye fursa za biashara
 
Polepole kasema rostam ni tapel na ni muhuni anaendesha genge la wahuni ccm tena kwa ushahid njo hapa ukanushe maneno yake na sio uanze kumjadili polepole.
Rostam ni mwekezaji mzawa, anajenga uchumi na kutoa ajira kwa Watanzania.
 
Ni kweli akishasema fulani kazaa na fulani , au akisema fulani kaua wawili, na atakaposema fulani Babaake ni fulani , Hakuna atakayejali ila sisi wananchi tutamsikiliza na kunakili kila Ujumbe wake

Hayo akiyasema yatatusaidiaje kufikia kwenye REAL REFORM?
 
Maskini wewe na familia yako. Hela kidogo tu ukipata unanunua bando kuja JF kuichamba Serikali, wenzio wanaingiza kwenye fursa za biashara
Situmii bando natumia wifi ; hata ingekuwa bando nafurahi kutoa mawazo yangu kupitia jamii forum!
Hela gani ya kuingiza kwenye biashara wakati Samia na Kikwete na genge lao la wahuni wanakomba hela zote mpaka zingine wanafukia shambani mwao huko Msoga na Kizimkazi!
 
Tatizo lako linaanzia kwa kinyongo chako na JPM
Ni kweli Magufuli ndiye aliyefanya yafuatayo;-
-Kusitisha shughuli za vyama vya siasa
- Kumshambulia Tundu Lissu
-Kuiba uchaguzi wote wa Serikali za Mitaa 2019
-Kuiba uchaguzi Mkuu 2020
-Kutishia vyombo vya habari na uhuru wa maoni
-Kuiitishia na kuiingilia Mahakama
-Kuliendesha Bunge kwa remote
-Kutumia Wasiojulikana kuteka na kuua
-Kumfukuza CAG baada ya kuibuliwa kashfa ya TZS 1.5 Trillion kwenye magesabu ya Serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…