Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba

Polepole hata wewe ulikula kwa urefu wa kamba enzi zako...
 
Anachohoji huyu ndugu hapo kwamba Leo Polepole anaonekana mnafiki akikosoa kisa alikuwa hakosoi enzi za JPM. Jamaa anahoji Chadema walimtukana Lowasa nchi nzima kuwa fisadi papa enzi za JK hadi akajiuzulu Kwa makashfa kibao ambayo hakuna mtanzania asiye yajua lakini baadae Chadema hao hao tena chini ya mwenyekiti yule yule Mbowe wakamchukua kuwa mgombea wao wa urais na kumnadi majukwaani!! Je huu sio unafiki? Mbona Leo Mbowe akikosoa hasemwi vibaya kuwa ni mnafiki wakati hapo awali alishakula matapishi yake yeye mwenyewe na viongozi wenzeke wa Chadema?

Kwanini Polepole ahukumiwe kwa makosa yaliyopita hadi sasa anyimwe uhalali wa kukosoa?

Hayo mambo ya mafanikio tuyaache pembeni kwanza la sivyo unambie kuwa ni halali kutumia mafisadi kisa tu yanaleta faida Fulani.
 
Comrade Punguza jazba
 


Halafu we jamaa ni bogus sijapata kuona ingawa mwenyewe unajiona 'machinowa'

Kwamba haukukubaliana na ujio wa lowassa CDM ,lakini mpaka leo bado upo humo humo CDM na hao viongozi waliomleta lowassa bado wapo kama viongozi,na daily unawapigania humu,kwani hiko chama ni Baba/Mama yako? na hao viongozi wake wana 'uspesho' gani kwako mpaka kuwang'ang'ania hivyo?


Sasa kama unazo akili jiulize kwa nini ulipinga ujio wa lowassa CDM, ukishapata jibu jiulize tena kama akili zako zina akili (unaishi kwa principles au unaishi tu kama bendera?)
 
Yeye ameshavimbiwa atulie na wenye njaa nao wale zam yao
 
Bora umenisaidia maana kuna wengine wanavichwa vigumu
 
Mwamba anaushabiki wa kisiasa unaosababisha ajitoe ufahamu
 

Anavyoongea hivi sasa haogopi kufa? Kama alikalia kimya mambo maovu, leo hiyo kula usawa wa kamba yake ndio inamtisha?
 

Kama hiyo awamu ya tano alipinga kila zuri lililo nje ya utashi wa mlo wake, mnatoa wapi nguvu ya kutaka sisi tuunge mkono hayo mnayoita mazuri sasa? Huyo Polepole hapigi kelele kwa ajili ya uzalendo, bali ni kukosa mlo. Akipewa mlo na kauli hiyo ikatolewa hawezi kujiuzulu. Nyinyi wenye upendo na yeye muungeni mkono, sisi wenye chuki na yeye kwasababu alikuwa kwenye awamu ya tano, msimamo wetu ndio huohuo. Hatuungi mkono muhuni yoyote no matter what.
 
Hiki unachokisema hapa kinaondoa ukweli wa kauli ya Polepole ?

Kwema lakini mkuu!!?
 
Kweli kabisa
 
Hiki unachokisema hapa kinaondoa ukweli wa kauli ya Polepole ?

Kwema lakini mkuu!!?

Sina tatizo na kauli ya Polepole kwani ni kauli inayosemwa mara zote na wapenda haki. Nina tatizo na Polepole kusema maneno hayo ili apate support ya kumfungulia njia ya kurejea kwenye mlo.

Mimi niko poa sana, nimerejea mjini toka shamba maana mvua imegoma. Nasikitika kuendelea kupoteza hela zangu kwa kuendelea na kilimo cha kutegemea biblia ili mvua inyeshe. Acha niendelee na biashara yangu wa kuwa wakala wa miamala ya fedha ya kampuni za simu na mabenki hapa mjini.
 

Acha kupanick dogo. Nilipinga ujio wa Lowassa maana nilijua Lowassa ni take away, na ukweli unajua saa hii Lowassa yuko wapi. Viongozi waliomleta bado wako maana wamechaguliwa na wengi kwa kura halali, hata kama sikubaliani na kiongozi yoyote dunia hii kukaa madarakani zaidi ya miaka 10. Mimi nina imani na taasisi na sio mtu. Kama ingekuwa naamini katika mtu basi ningeondoka wakati wa ujio wa Lowassa. Una lingine kwa msaada zaidi?
 
Huyu mzee ni shetani kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…