Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba

Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
Mbowe na genge lake.Kwahiyo kauli ni sahihi kisa Lisu alipigwa Risasi?
 
Kwahiyo Polepole inatakiwa aendelee kuunga mkono mabaya?
 
Kwa taarifa yako gaidi jiwe ndio maana Mungu akaamua ampeleke haraka sana motoni .
Marehemu gaidi alikuwa anatumia vijana wake akina mfungwa sabaya
Kwa hiyo huyo bibi ako au babu yako alipofariki naye ni gaidi? Vipi yule binti wa CHADEMA aliyefariki wiki jana nae ni gaidi maana ni mdogo sana kiumru kwa nini afariki kama sio gaidi! Nyie CHADEMA akili hamna kwa hiyo hata Watoto wanapofariki nao ni magaidi? kichwa panzi kweli wewe!
 
Na inawezekana kabisa nakumbuka wakati Raisi Mwinyi anamaliza muda wake Kuna mtia Nia mmoja alipiga biti kuwa atataja majina ya viongozi wote walioshiriki mauaji wananchi wakati wa operesheni ya vijiji vya ujamaa iliyoendeshwa na Raisi Nyerere ,Nyerere akataka kujitoa CCM.
 
Wanasiasa vigeugeu

Huyu naona sahv kahamia team malalamiko fc

Ova
 
Polepole tuambie nani alimpiga Lisu risasi haya mengine ni mambo yenu ya kihayawani tangu zamani
Wewe kila kitu Lissu!

Kama Peleka unayo nauli.....
mzigo akapakuwe basi.

Watu wanachinjwa kama kuku nchini,wewe umekomalia hizi Political scripts?

Tumewachoka sasa.......

Lissu mwenyewe anakula vizuri na familia yake + watoto wanasomeshwa EU.

Wewe unalala njaa na ukiamka Lissu...Lissu......

Si akheri hata uandike Yesu....Yesu.....
 
Kuna kitu sijawahi elewa, enzi za Msoga kuna mtu alipigwa Bomu, kuna kijana Arusha Alipigwa risasi hadharani kwenye maandamano just like Akwilina na PM akasema wapigwe tu, owner wa Mwanahalisi alimwagiwa tindikali, kiongozi wa madaktari alitekwa akaja kupatikana ameng'olewa kucha bt sijawahi kuskia hili likihusanishwa na Mzee wa Msoga au Nape aliekua Katibu Mwenezi...
Now days kuna mauaji kila siku, like everyday ukiamka unakutana na habari za mauaji( I lost a school mate aliekua mwenezi wa cdm mwanza, alipotea akaja patikana mochwari)
bt siskii Mama akisemwa ktk haya...
Unless tuambiane kuna exception inapokuja ktk haya masuala...kwamba yakifanyika utawala fulani then ni lao, yakifanyika tawala fulani haya hayawahusu...Or its a syndicate maalum kuchafua watu fulani na kukwepesha kwa wengine.
 
Hivi CHADEMA Wana msimamo wa kupinga Kila aongealo Polepole?! Na hili ni la kumbeza?!!
Rais kateleza, Ila pia yeye ni mwanadamu. Ila kwa vile nikiongozi, Tena wa kidemokrasia, ilibidi ashambuliwe kweli kweli kwa kauli ile, mithili ya jinsi alivoshambuliwa Ndugai kwa kauli ake iliopelekea yeye kujiuzuru.

Hii nchi ni ngumu sana, hasa ukiwa unafuatilia mijadala ukiwa huna upande.

Nadhani shida ni mfumo wa elimu tulionayo.

Tuna kizazi Cha kijinga Sana, ambacho hata tungeanza Leo kua serious, Basi mabadiriko yata Anza kuonekana mwaka 2050.

Kwa Sasa, CCM ni hovyo, Ila Chadema ni hovyo zaidi, wamekua lakini bado Wana Mambo ya kiharakati. Vyama vingine ndio kabisaa.
Nilidhani TISS, 2022, tuleteeni Chuma zaidi ya kile kilichotangulia mbele ya haki halafu kidumu Hadi 2050.

Mawazo binafsi.
 

Weka koma na nukta hata kama unachokiongea ni kweli. Sio kila mtu alikubaliana na walichofanya CDM kwa kumpokea Lowassa, bali imani imebaki kwa CDM kama taasisi. Polepole ni mtu na sio taasisi. Kwani Polepole anapingwa na wote kwenye huo uhuni wake anaouongea sasa?
 
Acheni rais apingwe akifanya makosa, ataruhusuje mawaziri wafanye ufisadi eti sababu ni wakati wao halafu chadema wafurahi na kumbeza polepole kisa katoka hadharani na kulaani ile ruhusa? Chadema msipende kupinga Kila kitu kisa Polepole ni CCM.

Lini Polepole aliwahi kuwaunga mkono CDM alipokuwa kwenye ulaji ili tujue hapingi kila kitu? Unataka watu walie na upuuzi wa Polepole wakati tunajua yeye ni mnafiki ambaye mlo wake umetikiswa?
 
Mbona mie nimeielewa tofauti kauli ya mh rais?

Sent from my SM-G935V using JamiiForums mobile app
 


Polepole hata aongee zuri vipi ataungwa mkono na wanafiki wachache. Alishiriki kwa mkono wake kuua demokrasia hapa nchini, kisha leo anategemea demokrasia hiyo hiyo ipambane na hizo kauli za bibi ushungi. Ukate mahindi shambani, kisha njaa ikikuumiza uje hadharani unalia kisha utegemee kueleweka? Huyo Polepole sasa hivi akipewa uwaziri atanyamazia uhuni wote. Alipokuwa kwenye tume ya katiba mpya, alikuwa anapinga kwa nguvu zake zote cheo cha DC, alipopewa cheo hicho akanyamaza! Huyo muhuni hata akipiga kelele nani atamuelewa?
 



 
Polepole analitafuta kwa nguvu valangati ka kisiasa.
Ndugai alianza hivyo hivyo, mwishowe akawa analia nimekosa mimi, nimekosa sana.
Stay tuned, Polepole ajali anaitafuta.
 
Ingelikuwa bora sana kama tungejadili hoja ya Polepole kama ina mashiko au la kuliko kuibeza kwa sababu tu eti hamumpendi. Suala la kiongozi mkuu wa nchi kuhalalisha wateule wake kufuja mali za umma bila kukemea kwa nguvu kubwa sio sawa. Hata kama anajua kuwa viongozi wanapata sehemu zao, je ni halali kushadadia hilo wakati wako pale kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi na sio kula?? Hamuoni kuwa waliotoa hiyo kauli wanafurahi kuona mnaiunga mkono? Maana kupinga maoni ya Polepole ni kuunga mkono maneno hayo yaliyotamkwa. Pole pole yuko sahihi kuzungumza vile ingawa anaweza asiwe mtu sahihi wa kuongelea hilo maana alikuwapo kwenye system na mambo mengi ya hovyo yalitendeka huku akikaa kimyaa. Lakini haina maana leo hii akikemea suala ambalo sote tunalikemea basi tusiunge mkono hoja yake.
Aliyoyaongea ni mazuri ila yeye sio mzuri kiasi hicho. Tuichukue hoja yake na tusiwavimbishe kichwa waliotoa kauli hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…