Polisi Afrika Kusini waanzisha msako baada ya watu 17 kuuawa katika shambulio la risasi klabuni

Polisi Afrika Kusini waanzisha msako baada ya watu 17 kuuawa katika shambulio la risasi klabuni

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Polisi nchini Afrika Kusini walisema siku ya Jumapili Septemba 27, 2026 kuwa wameanzisha msako mkali baada ya watu 17 kuuawa katika shambulio la risasi usiku wa Jumamosi Septemba 26, 2026 kwenye kilabu cha pombe (tavern) katika mtaa wa Wedela, kusini magharibi mwa Johannesburg.

Huduma za dharura za matibabu ziliwatangaza waathiriwa wote 17 kuwa wamefariki dunia papo hapo katika eneo la tukio, na chanzo cha shambulio hilo bado hakijajulikana, kulingana na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini.

Polisi waliongeza kuwa "watuhumiwa inasemekana walikuwa wamejihami kwa bunduki za AK-47 na bastola."

======

South African police said on ‌Sunday ⁠they had launched a manhunt ‌after ‌17 people were ‌killed in ‌a shooting at a tavern in ⁠Wedela ‌township southwest of Johannesburg.

Emergency medical services ‌declared all 17 victims dead at the scene, and the motive for ⁠the shooting ⁠was ⁠not known, the South African Police ‌Service said, adding ‌that "suspects were reportedly ⁠armed with AK-47 rifles ⁠and pistols".
 
Soon tanganyika.
Kazi ni kipimo cha utu
 
27 September 2026
Carletonville, Gauteng
Republic of South Africa

RIPOTI YA : Shambulio la Risasi la Johannesburg MUBASHARA : Watu 17 Wauawa, Watu Wenye Bunduki Wafyatua Risasi Katika Kilabu Cha pombe [Tavern]

View: https://m.youtube.com/watch?v=080wNAvxMsQ

Polisi wa Afrika Kusini wameanzisha msako mkali baada ya watu 17 kuuawa na 15 kujeruhiwa katika shambulio la risasi katika kilabu cha pombe mmoja huko Wedela, kusini magharibi mwa Johannesburg. Polisi wanasema washukiwa wanane wasiojulikana wanaripotiwa kuwa na bunduki aina ya AK-47 na bastola.

Maharamia hao walitekeleza uhalifu huo kwa zaidi ya dakika 30 mfululizi kisha waliwapekuwa wahanga na kuiba simu pia fedha kabla ya kutokomea

Police wa Gauteng wasema uchunguzi unaendelea, mamlaka zinasema uhalifu huo unahusisha jamii ya hapo Carletonville pia wale wa ZamaZama [Machimbo ya madini] na hadi sasa hakuna aliyekamatwa na nia bado haijulika.

Wahanga waliokumbwa na shambulio uraia wao 13 ni waSauzi, 1 MuEthiopia, 3 Lesotho na wengine bado haujajulikana

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZrExMRvOvt4

Wananchi waongea kuhusu shambulio hilo, lililosababisha watu 17 kupoteza maisha yao kilabuni

View: https://m.youtube.com/watch?v=-vPcQ23DdNM
 
Watumie huo upepo kuweka sheria kali, au kufanya kama kule El Salvador.
 
27 September 2026

27 WAUAWA NCHINI AFRIKA YA KUSINI, KATIKA MATUKIO MAWILI MAENEO YA GAUTENG NA CAPE TOWN

Afrika Kusini - Angalau watu 27 wameuawa na zaidi ya wengine 20 wamejeruhiwa katika ufyatuaji risasi mbili tofauti katika vitongoji vya Afrika Kusini, huku polisi wakianzisha uchunguzi ili kuwasaka washukiwa hao.

Shambulio la kwanza lilitokea Jumamosi jioni katika kilabu cha pombe huko Wedela, kusini magharibi mwa Johannesburg, ambapo watu 17 waliuawa na wengine 15 kujeruhiwa.

Polisi walisema ufyatuaji risasi ulianza yapata saa 3:30 usiku katika Extension 3, Wedela, katika wilaya ya West Rand katika jimbo la Gauteng.

Kulingana na mamlaka, watu wenye silaha waliwafyatulia risasi watu waliokusanyika nje ya mgahawa kabla ya kuingia ndani ya jengo hilo na kuendelea na shambulio hilo. Baadhi ya wateja waliripotiwa kupekuliwa na simu zao za mkononi kuchukuliwa.

Washukiwa baadaye walikimbia kwa magari mawili, huku magari mengine mawili yakichomwa moto.

Polisi walisema washukiwa wanane waliripotiwa kuwa na bunduki aina ya AK-47 na bastola. Chanzo cha shambulio hilo hakijajulikana na hakuna mtu aliyekamatwa aliyetangazwa.

Kapteni Tintswalo Sibeko alisema wapelelezi na vitengo maalum vya polisi vimetumwa ili kuwatambua na kuwakamata washukiwa.

Polisi walifungua kesi 17 za mauaji, kesi 15 za kujaribu mauaji na kesi mbili zinazohusiana na uharibifu wa mali kufuatia shambulio hilo.

Katika tukio tofauti mapema Jumapili, watu 10 waliuawa na wengine 11 kujeruhiwa wakati watu wenye silaha walipofyatua risasi katika duka moja huko Lwandle, karibu na Cape Town. Polisi walisema washukiwa kadhaa walikuwa wakitafutwa kuhusiana na ufyatuaji risasi wa pili, ambao ulitokea baada ya usiku wa manane.

View: https://m.youtube.com/watch?v=VFEoMbwjuFc
At least 10 people were killed and 11 wounded after gunmen opened fire at a late-night venue in Lwandle near Cape Town, South Africa. Police have launched a manhunt for the suspects, with no arrests reported.

Mashambulizi hayo yalitokea siku chache tu baada ya watu 11, tarehe 23 September 2026 akiwemo mwanamke mjamzito, kuuawa wakati wa ufyatuaji risasi katika sherehe ya kifamilia [house party] karibu na Durban.

View: https://m.youtube.com/watch?v=zmzLh8eVFhw
Three shooters killed at least 11 people, including a woman who was believed to be pregnant, in an attack at a house party near Durban in South Africa.

Afrika Kusini inaendelea kurekodi viwango vya juu vya uhalifu wa kutumia nguvu, ikiwa ni pamoja na mauaji yanayohusiana na silaha za moto, na kusababisha wasiwasi mpya kuhusu vurugu za bunduki katika jamii
 
Back
Top Bottom