Polisi Dar wazuia Mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika

Polisi Dar wazuia Mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezua Mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Kibamba John Mnyika na Wananchi wake, Uliokuwa ufanyike leo Feb 8, 2020 kata ya Mbezi njee kidogo na Jiji la Dar es salaam.

Polisi wamedai kuwa eneo la stendi ya zamani ulipotakiwa kufanyika mkutano huo kuna ujenzi wa barabara unaendelea.

#MTZ
Jeshi letu limeamua kuweka weledi pembeni na hata kujitoa ufahamu ili tu kuwafurahisha makada wa CCM, kwa kuwa wanatambua kuwa ndio watu pekee wenye kuwahakikishia vyeo na mishahara yao.

Kusimamia sheria, usalama na mali za watu hili limekuwa si tena "primary" kwao isipokuwa ni kama "secondary objective" ikitegemea wameambiwa wafanye nini ama hata kwa kujipendekeza tu pasipo hata kuelekezwa kufanya kitu chochote kile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezua Mkutano wa Hadhara wa Mbunge wa Kibamba John Mnyika na Wananchi wake, Uliokuwa ufanyike leo Feb 8, 2020 kata ya Mbezi njee kidogo na Jiji la Dar es salaam.

Polisi wamedai kuwa eneo la stendi ya zamani ulipotakiwa kufanyika mkutano huo kuna ujenzi wa barabara unaendelea.
Sasa si wangeelekeza eneo mbadala au?!Polisi bwana.......?????!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hali hii mpaka lini bora kukinukisha tu mpaka kieleweke,sababu za kipumbavu sana..
 
Mh Waziri Mkuu Majaliwa, alidanganya bungeni Alhamisi?
 
Wazee wa kumwaga mafuta gate moja washafanya yao!! Twafwaaa!!
 
Nimetoka mkutano wa chama CCM kirumba, polepole anahutubia ambavyo sivielewi kabisa, mpaka nikakumbuka matamko ya CDM, kumbe bado wapinzani tumekalia kaa la moto la kutofanya mkutano,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
INAKERA, INAKEREHESHA, INAKIRIHISHA na kukufanya mtu ubakie unacheka kicheko cha Mwendawazimu!!
 
Back
Top Bottom