Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa tuhuma za kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la SATCO, Said Fadhili (54).
Tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya basi hilo lenye namba za usajili T308 EME, aina ya Yutong, kukwangua gari la TARURA lenye namba STM 5806, aina ya Land Cruiser LX 70 Series, lililokuwa likiendeshwa na Masawa.
Soma: Dereva wa SATCO aoneshewa bastola, abiria wamnusuru "walitaka kumchukua"
Polisi ilifika eneo la tukio baada ya taarifa kutolewa na kumkamata Masawa, ambapo upekuzi ulibaini kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni kilikuwa toyi, si bastola halisi. Aidha, Polisi ilibaini kuwa gari hilo lilikuwa likitumia namba T881 ENZ, ambazo ni za gari mali ya mtu mwingine, badala ya namba zake halisi STM 5806.
TAARIFA KWA UMMA YA JESHI LA POLISI IMESEMA, DEREVA ALIYETISHIA KWA SILAHA BANDIA AKAMATWA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma Sath John Masawa (31) kwa kosa la kumtisha kwa kitu kilichodhaniwa ni bastola dereva wa basi la SATCO lenye usajili namba T308 EME aina ya Yutong aitwaye Said Fadhili (54) wakati akiwa anatoka kuweka mafuta katika kituo cha Total Energies na kudaiwa kukwangua gari mali ya TARURA lenye usajili namba STM 5806 aina ya Land Cruseir LX 70 series iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa huyo.
Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John na baada ya kufanya upekuzi lilifanikiwa kutambua kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni ni toyi siyo silaha halisi kama ilivyodhaniwa na wananchi.
Pia, Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari hilo lilikuwa halitumii namba za usajili halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA wakati tukio hilo bali namba za usajili T 881 ENZ ambayo ni gari mali ya mtu mwingine. Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari na kwa kufanya hivyo kunaficha utambulisho halisi wa gari kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.