Polisi: Dereva wa Basi la SATCO alitishiwa na silaha bandia (Toyi), aliyetishia akamatwa

Polisi: Dereva wa Basi la SATCO alitishiwa na silaha bandia (Toyi), aliyetishia akamatwa

DEREVA ALIYETISHIA KWA SILAHA BENDERA AKAMATWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa kosa la kumtishia kwa kitu kinachodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la SATCO lenye usajili T308 EME, aina ya Yutong aitwaye Said Fadhili (54).

Tukio hilo lilitokea wakati Said Fadhili akiwa anatoka kuweka mafuta katika kituo cha Total Energies na kudaiwa kukutana na gari mali ya TARURA lenye usajili STM 5806, aina ya Land Cruiser LX 70 Series, lililokuwa likiendeshwa na mtuhumiwa huyo.

Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John. Baada ya upekuzi, ilibainika kuwa kitu alichokuwa ameshika hakikuwa silaha halisi kama ilivyodhaniwa awali.

Aidha, Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari la TARURA lililohusika katika tukio hilo lilikuwa halitumii namba zake halali za usajili, ambapo namba STM 5806 ilidaiwa kuwa mali ya mtu mwingine, huku gari hilo likiwa na namba T 881 ENZ.

Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari, kwani kufanya hivyo ni kuficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

MY TAKE;
Kwanini Polisi hawajataja jina la mtu alompa hiyo namba? Hata John Heche alikuwa anafuatiliwa Nyumbani kwake. Tulipofuatilia namba ya gari, tukakutana ni namba ya Tela la Trekta. Haya mambo yataisha lini. Hata hivyo Polisi naona wameanza kujitenga na wauaji.
Namba bandia zinabandikwa kwa kuchomekwa na zipo wazi dah ila ... au basi tu.
 
POLISI HAMUAMINIKI KATU
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari, kwani kufanya hivyo ni kuficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Cover ya spare tyre ina nembo hii

1790083270448.png

Huku nembo ya TPDF inafanana kidogo na ya landcruiser spare tyre

1790083825284.png

LINGANISHA NEMBO HIZO MBILI
 
Jambo ambalo huenda watu wengi hawalijui ni kwamba kila gari ya serikali ina namba za kiraia ambazo usajili wake unakoma haraka pindi linapopata nambari ya kiserikali lakini namba zile huhifafhiwa kwasababu dharura huweza kutokea ili zitumike.
Ila kama jamaa aliweka tu za kuchonga msala wake unaweza kuwa mkubwa zaidi ila kama alitumia zile za awali si issue kubwa
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Sath John Masawa (31), baada ya kubainika kutumia bastola ya kuchezea (toyi) kumtishia dereva wa basi la abiria, huku akiwa ametumia namba za usajili za kughushi kwenye gari la Serikali.

Tukio hilo lilimhusisha dereva wa basi la Kampuni ya Satco lenye namba za usajili T 308 EME, Said Fadhil (54), linalofanya safari zake hapa nchini.

Akizungumza kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo leo, Septemba 22, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, ameeleza kuwa uchunguzi wa kina wa Jeshi la Polisi ulibaini chombo alichokitumia mtuhumiwa huyo hakikuwa silaha halisi ya moto.

"Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa kitu hicho hakikuwa bastola halisi kama ilivyodhaniwa awali, bali kilikuwa ni bastola ya kuchezea (toyi)," amebainisha Kamanda Hyera.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limebaini kuwa wakati wa tukio hilo, gari hilo la TARURA lilikuwa likitumia namba za usajili T 881 ENZ badala ya namba zake halisi za usajili wa Serikali ambazo ni STM 5806, huku namba hizo za bandia zikigundulika kuwa ni mali ya mtu mwingine.

Kufuatia kubainika kwa ukiukaji huo wa sheria, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kali kwa madereva na wamiliki wote wa vyombo vya moto nchini kujiepusha na matumizi ya namba za usajili zisizo halali.

#SasaLive #PolisiDodoma #TARURA #GallusHyera #SatcoBus UsalamaBarabarani Dodoma Tanzania
1790083710645.jpg
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari, kwani kufanya hivyo ni kuficha utambulisho halisi wa gari na ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Cover ya spare tyre ina nembo hii
Cover ya spare tyre ina nembo hii

View attachment 3675769

Huku nembo ya TPDF inafanana kidogo na ya landcruiser spare tyre

View attachment 3675776

LINGANISHA NEMBO HIZO MBILI

Nini jeshi la polisi na TPDF watu wake wa utambuzi intellejensia wanatufafanulia matumizi ya TARURA kutumia nembo inayofanana ya jeshi la ulinzi ?

1790084004789.png

1790084050183.png
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa tuhuma za kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la SATCO, Said Fadhili (54).

Tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya basi hilo lenye namba za usajili T308 EME, aina ya Yutong, kukwangua gari la TARURA lenye namba STM 5806, aina ya Land Cruiser LX 70 Series, lililokuwa likiendeshwa na Masawa.

Soma: Dereva wa SATCO aoneshewa bastola, abiria wamnusuru "walitaka kumchukua"

Polisi ilifika eneo la tukio baada ya taarifa kutolewa na kumkamata Masawa, ambapo upekuzi ulibaini kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni kilikuwa toyi, si bastola halisi. Aidha, Polisi ilibaini kuwa gari hilo lilikuwa likitumia namba T881 ENZ, ambazo ni za gari mali ya mtu mwingine, badala ya namba zake halisi STM 5806.

TAARIFA KWA UMMA YA JESHI LA POLISI IMESEMA, DEREVA ALIYETISHIA KWA SILAHA BANDIA AKAMATWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma Sath John Masawa (31) kwa kosa la kumtisha kwa kitu kilichodhaniwa ni bastola dereva wa basi la SATCO lenye usajili namba T308 EME aina ya Yutong aitwaye Said Fadhili (54) wakati akiwa anatoka kuweka mafuta katika kituo cha Total Energies na kudaiwa kukwangua gari mali ya TARURA lenye usajili namba STM 5806 aina ya Land Cruseir LX 70 series iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa huyo.

Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John na baada ya kufanya upekuzi lilifanikiwa kutambua kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni ni toyi siyo silaha halisi kama ilivyodhaniwa na wananchi.

Pia, Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari hilo lilikuwa halitumii namba za usajili halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA wakati tukio hilo bali namba za usajili T 881 ENZ ambayo ni gari mali ya mtu mwingine. Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari na kwa kufanya hivyo kunaficha utambulisho halisi wa gari kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Director amepuyanga..arudi kuandika script upya..
 
Back
Top Bottom