TISSKuna kitu kinapunguzwa uzito hapo, cheki code zfuatazo:
- Gari la Serikali
- Dereva wa Serikali
- Silaha toy
- Plate namba tofauti
- Plate number nyingine ilikutwa imebebana
- Gari ya ....
- Unga hizo code mwenyewe
TISSKuna kitu kinapunguzwa uzito hapo, cheki code zfuatazo:
- Gari la Serikali
- Dereva wa Serikali
- Silaha toy
- Plate namba tofauti
- Plate number nyingine ilikutwa imebebana
- Gari ya ....
- Unga hizo code mwenyewe
Unaamini kwa sababu wametoa haraka? Jeshi la polisi mimi huwa nawaita jeshi la uongo. Ni waongo sijawahi kuona. Hata hii wameongopa na kuna kitu wanaficha. Hawa walikuwa ni mauaji wa Samia.Kumekucha Hili Wamelitolea Ufafanuzi Haraka Zile Gari Nyingine Mbona Wanapata Ganzi Miaka Tele
Yako mengi hayo,hasa baada ya kuruhusu madereva walale na magari ya serikali huku Huku Dodoma!
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa tuhuma za kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la SATCO, Said Fadhili (54).
Tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya basi hilo lenye namba za usajili T308 EME, aina ya Yutong, kukwangua gari la TARURA lenye namba STM 5806, aina ya Land Cruiser LX 70 Series, lililokuwa likiendeshwa na Masawa.
Soma: Dereva wa SATCO aoneshewa bastola, abiria wamnusuru "walitaka kumchukua"
Polisi ilifika eneo la tukio baada ya taarifa kutolewa na kumkamata Masawa, ambapo upekuzi ulibaini kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni kilikuwa toyi, si bastola halisi. Aidha, Polisi ilibaini kuwa gari hilo lilikuwa likitumia namba T881 ENZ, ambazo ni za gari mali ya mtu mwingine, badala ya namba zake halisi STM 5806.
TAARIFA KWA UMMA YA JESHI LA POLISI IMESEMA, DEREVA ALIYETISHIA KWA SILAHA BANDIA AKAMATWA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma Sath John Masawa (31) kwa kosa la kumtisha kwa kitu kilichodhaniwa ni bastola dereva wa basi la SATCO lenye usajili namba T308 EME aina ya Yutong aitwaye Said Fadhili (54) wakati akiwa anatoka kuweka mafuta katika kituo cha Total Energies na kudaiwa kukwangua gari mali ya TARURA lenye usajili namba STM 5806 aina ya Land Cruseir LX 70 series iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa huyo.
Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John na baada ya kufanya upekuzi lilifanikiwa kutambua kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni ni toyi siyo silaha halisi kama ilivyodhaniwa na wananchi.
Pia, Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari hilo lilikuwa halitumii namba za usajili halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA wakati tukio hilo bali namba za usajili T 881 ENZ ambayo ni gari mali ya mtu mwingine. Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari na kwa kufanya hivyo kunaficha utambulisho halisi wa gari kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.
CCM yenu ndo imetufikisha Huku!Dereva mtu mzima anayeweka toy kiunoni apelekwe kwanza Mirembe akachekiwe akili. Halafu dereva anayetumia namba bandia anaonywa tu au hiyo peke yake inatosha kumfungulia mashtaka? Polisi fanyeni kazi yenu kwa weledi msiangalie sura na kuwa na double standards.
Hata Heche alikutana na caterpillar!Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari hilo lilikuwa halitumii namba za usajili halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA wakati tukio hilo bali namba za usajili T 881 ENZ ambayo ni gari mali ya mtu mwingine.
Huu ujinga Serikali isipoufuta,kuna siku Rais atapiga shaba na gari lenye namba feki
Peleka upuuzi mbali.Jambo ambalo huenda watu wengi hawalijui ni kwamba kila gari ya serikali ina namba za kiraia ambazo usajili wake unakoma haraka pindi linapopata nambari ya kiserikali lakini namba zile huhifafhiwa kwasababu dharura huweza kutokea ili zitumike.
Ila kama jamaa aliweka tu za kuchonga msala wake unaweza kuwa mkubwa zaidi ila kama alitumia zile za awali si issue kubwa
Mashuhuda wanasema “driver wa lile gari allmkwida driver wa Bus akawa anamvutia kwenye gari la Serikali….kwa lengo ka kuondoka nae”Mashuhuda wanasema “driver wa lile gari allmkwida driver wa Bus akawa anamvutia kwenye gari la Serikali….kwa lengo ka kuondoka nae”
Hakuna driver wa Serikali anaweza kujiamulia kuchange plate number bila boss wake kujua
Hakuna driver wa TARURA anawazea kubeba na kutembea na toy la Bastola kiunoni. Hayupo
Hii story ya kindezi sana, aibu tunaona sisi na polisi hawajali wala nini
ok.Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Sath John Masawa (31), baada ya kubainika kutumia bastola ya kuchezea (toyi) kumtishia dereva wa basi la abiria, huku akiwa ametumia namba za usajili za kughushi kwenye gari la Serikali.
Tukio hilo lilimhusisha dereva wa basi la Kampuni ya Satco lenye namba za usajili T 308 EME, Said Fadhil (54), linalofanya safari zake hapa nchini.
Akizungumza kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo leo, Septemba 22, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gallus Hyera, ameeleza kuwa uchunguzi wa kina wa Jeshi la Polisi ulibaini chombo alichokitumia mtuhumiwa huyo hakikuwa silaha halisi ya moto.
"Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa kitu hicho hakikuwa bastola halisi kama ilivyodhaniwa awali, bali kilikuwa ni bastola ya kuchezea (toyi)," amebainisha Kamanda Hyera.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limebaini kuwa wakati wa tukio hilo, gari hilo la TARURA lilikuwa likitumia namba za usajili T 881 ENZ badala ya namba zake halisi za usajili wa Serikali ambazo ni STM 5806, huku namba hizo za bandia zikigundulika kuwa ni mali ya mtu mwingine.
Kufuatia kubainika kwa ukiukaji huo wa sheria, Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limetoa onyo kali kwa madereva na wamiliki wote wa vyombo vya moto nchini kujiepusha na matumizi ya namba za usajili zisizo halali.
#SasaLive #PolisiDodoma #TARURA #GallusHyera #SatcoBus UsalamaBarabarani Dodoma TanzaniaView attachment 3675775

Wekeni hiyo picha ya hiyo silaha bandia hapa tuione!
POLISI MJUE MUNGU ANAWAONAPolisi hawa watu kwa Mungu hukumu yao itakuwa tofauti na watu wengine wao kila neno ni uongo uongo tu.
PoiliCCM..... atakua kada huyo.Dereva mtu mzima anayeweka toy kiunoni apelekwe kwanza Mirembe akachekiwe akili. Halafu dereva anayetumia namba bandia anaonywa tu au hiyo peke yake inatosha kumfungulia mashtaka? Polisi fanyeni kazi yenu kwa weledi msiangalie sura na kuwa na double standards.