Polisi: Dereva wa Basi la SATCO alitishiwa na silaha bandia (Toyi), aliyetishia akamatwa

Polisi: Dereva wa Basi la SATCO alitishiwa na silaha bandia (Toyi), aliyetishia akamatwa

Ni fala, angemkuta mtu ana Mkwaju angemuua au kumsababishia majeraha na ulemavu wa kudumu kwa kujihamo na usenge wake huo.
Huwezi mtishia mtu silaha hata kama ni bandia.
Kuna mbinu ya kumiliki silaha inaitwa "rise and kill first", unamtisha mtu na kitoi anakubutua kweli anajua unataka kumuua. Alimkuta dereva hana mkwaju, mimi ningeshakuwa nyuma ya nondo saa hii.
 
Ni fala, angemkuta mtu ana Mkwaju angemuua au kumsababishia majeraha na ulemavu wa kudumu kwa kujihamo na usenge wake huo.
Huwezi mtishia mtu silaha hata kama ni bandia.
Kuna mbinu ya kumiliki silaha inaitwa "rise and kill first", unamtisha mtu na kitoi anakubutua kweli akujua aunataka kumuua. Alimkuta dereva hana mkwaju, mimi ningeshakuwa nyuma ya nondo saa hii.
Je umeamini kweli silaha ilikuwa bandia?
Je umeamini kweli plate number 'bandia' iliwekwa na dereva kwa utashi wake?
Je unaamini yule ni dereva wa TARURA tuu!?🤣
 
Je umeamini kweli silaha ilikuwa bandia?
Je umeamini kweli plate number 'bandia' iliwekwa na dereva kwa utashi wake?
Je unaamini yule ni dereva wa TARURA tuu!?🤣

Vyovyote iwavyo; huyo jamaa alikuwa anabeti maisha yake kwa kumtishia mtu silaha kifala namna hiyo. Ni bongo tuu, South Africa hakuna kosa la kujihami na kujitetea maisha yako. Unatoa chuma mtu anakuwahi, vyovyote vile kukutuliza.
 
Jambo ambalo huenda watu wengi hawalijui ni kwamba kila gari ya serikali ina namba za kiraia ambazo usajili wake unakoma haraka pindi linapopata nambari ya kiserikali lakini namba zile huhifafhiwa kwasababu dharura huweza kutokea ili zitumike.
Ila kama jamaa aliweka tu za kuchonga msala wake unaweza kuwa mkubwa zaidi ila kama alitumia zile za awali si issue kubwa
Linda mgongo wako mkuu!! Wewe wakiume alafu unajiita Mama Samia unatafuta wateja??
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma, Sath John Masawa (31), kwa tuhuma za kumtishia kwa kitu kilichodhaniwa kuwa bastola dereva wa basi la SATCO, Said Fadhili (54).


Tukio hilo linadaiwa kutokea baada ya basi hilo lenye namba za usajili T308 EME, aina ya Yutong, kukwangua gari la TARURA lenye namba STM 5806, aina ya Land Cruiser LX 70 Series, lililokuwa likiendeshwa na Masawa.

Soma: Dereva wa SATCO aoneshewa bastola, abiria wamnusuru "walitaka kumchukua"

Polisi ilifika eneo la tukio baada ya taarifa kutolewa na kumkamata Masawa, ambapo upekuzi ulibaini kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni kilikuwa toyi, si bastola halisi. Aidha, Polisi ilibaini kuwa gari hilo lilikuwa likitumia namba T881 ENZ, ambazo ni za gari mali ya mtu mwingine, badala ya namba zake halisi STM 5806.

TAARIFA KWA UMMA YA JESHI LA POLISI IMESEMA, DEREVA ALIYETISHIA KWA SILAHA BANDIA AKAMATWA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa TARURA Wilaya ya Dodoma Sath John Masawa (31) kwa kosa la kumtisha kwa kitu kilichodhaniwa ni bastola dereva wa basi la SATCO lenye usajili namba T308 EME aina ya Yutong aitwaye Said Fadhili (54) wakati akiwa anatoka kuweka mafuta katika kituo cha Total Energies na kudaiwa kukwangua gari mali ya TARURA lenye usajili namba STM 5806 aina ya Land Cruseir LX 70 series iliyokuwa ikiendeshwa na mtuhumiwa huyo.

Baada ya kuripotiwa kwa tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kumkamata Sath John na baada ya kufanya upekuzi lilifanikiwa kutambua kuwa kitu alichokuwa amevaa kiunoni ni toyi siyo silaha halisi kama ilivyodhaniwa na wananchi.

Pia, Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari hilo lilikuwa halitumii namba za usajili halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA wakati tukio hilo bali namba za usajili T 881 ENZ ambayo ni gari mali ya mtu mwingine. Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa onyo kwa madereva kuacha kutumia namba bandia za magari na kwa kufanya hivyo kunaficha utambulisho halisi wa gari kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa sheria.


Of course wasiojulikana wanapaswa kuendelea kuwa wasiojulikana, Tarura inapaswa nayenyewe iweke wazi inawezekanaje hela za umma za mafuta, magari na watendaji wake kuhusika kwenye mental retarded activities kama hizi...na ni sahihi gari ya Tarura kujazwa Tinted hivi wanaficha nini humo ndani ? Wamegundua lami mpya ?
 
Jeshi la Polisi liligundua kuwa gari hilo lilikuwa halitumii namba za usajili halisi ambazo ni STM 5806 mali ya TARURA wakati tukio hilo bali namba za usajili T 881 ENZ ambayo ni gari mali ya mtu mwingine.

Huu ujinga Serikali isipoufuta,kuna siku Rais atapiga shaba na gari lenye namba feki
Kuna ubaya gani kama atapigwa?
 
Of course wasiojulikana wanapaswa kuendelea kuwa wasiojulikana, Tarura inapaswa nayenyewe iweke wazi inawezekanaje hela za umma za mafuta, magari na watendaji wake kuhusika kwenye mental retarded activities kama hizi...na ni sahihi gari ya Tarura kujazwa Tinted hivi wanaficha nini humo ndani ? Wamegundua lami mpya ?
Ngoja nikupe code

Ambulance,stk ,na hizi land cruiser full tinted mm zikifka nilipo naondoka zangu ...
 
Ufafanuzi huu uko kimtego sana.
1. Fake namba kutoka ENZ kuwa STM gari la Tarula????!!!!
2. Fake pistol au toy????
3. Walifika eneo la tukio na kumkamata vs shuhuda walisema aliita gari lingine likamchukua na kutokomea ???!!!
 
Back
Top Bottom