Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Pengine mh Tundu Lisu amepigwa risasi na watuhumiwa wa Makinikia (dhahabu, almasi na Tanzanite) kwa lengo la kutugawa na ku divert mjadara kuhusu wizi wa madini.. Sitaki kuamini kama serikali ama watanzania wanaweza kufika huko.Just thinking outside the box
 
May God 'posibolaize' the impossible, leave no stone unturned.
 

Kila mtanzania mwenye Akili timamu na mfuatiliaji wa mambo anajua hii kitu 100% ni matokeo ya msimamo wa Lissu dhidi ya ujinga wa watawala wa chama cha Kijani. Nani mwingine ana chuki binafsi na Lissu?

Unazungumzia kupewa ulinzi kwa Profesa Mruma, yule profesa anayekiri kuwa alisaini mkataba bila kuusoma. Nani ana mpango wa kwenda kumdhuru?
 
nyie ndo mtupe taarifa kwani ndo walinzi wa raia na mali zao.tumechoka na kila mara watu wasiojulikana.hao watu wasiojulikana wanapatikana hapa TZ tu
 
Huwezi kuthink nje ya box kabla kwanza hujathink ndani ya box.
Embu tuambie tu, ndani ya box unafikiri nani anahusika?

Nani ni adui wa Lissu?
Kwanini makada karibu wote wa kijani walikuwa busy mitandaoni kwa zaidi ya miezi mitatu sasa kuwaita kina Lissu ni 'wahaini'?
Unajua hukumu ya mhaini?
 
kwanza kwa kuangalia tukio lenyewe inaonyesha watu wale si wabobezi ktk kazi yao! risasi 10+ pale mlangoni na mtu anatoka majeruhi.. ilikuwa ni sekunde ngapi kutoka walipo mpk kwenye gari la lisu kuhakiki kuwa mlengwa amekufa au la.. namna ya ufatiliaji wa gari la lisu tu ni kihoja! kwa mwanainteljensia alietukuka atafanyaje ufatiliaji mpk mtu wa kawaida ang'amue mapema..?
kwa shambulizi la risasi zote zile inaonyesha walidhamiria kumuuwa!

inaniwia kigugumizi kusema hao watuumiwa wa makinikia ndo wamefanya hivyo! iweje wachague watu wasio makini hlf wafyatue risasi zote hizo kwa kujeruhi tu tena hujui kwamba muhusika utampata wapi..!
dhamana kubwa ilikuwa kwa dereva!
kama aliweza kugundua kuwa wanafatiliwa ni heri angepeleka gari kwenye kituo cha polisi kisha wangeomba ulinzi maana mtu aliekuwa amembeba nafikiri anamjua na wengi wanaweza kumchukia nashauri madereva wa viongozi wawe walinzi kabisa ili kuepusha mengi,escaping chance ilikuwepo lkn kung'amua inahitaji makini.
 
kama tuliambiwa yule aliyemtola bastola Mh Nnauye hajulikani na hakukamatwa (zimwi?), hata hao waliomshambulia Lissu wangeonekana kwenye video inawezekana pia tungeambiwa hawajulikani.
 
Natamani kuona matokeo ya kipimo cha akili yako ya kupambanua mambo.Labda kwa kukusaidia ni kwamba,Hata Mrema alikuwa kama Lisu,hata Lipumba alkuwa kama lisu kwa awamu yake taja na wengine unaowakumbuka,ni bahati mbaya tu kwa kamanda huyu mi namuita Brigedia but kazi ya kizalendo kaifanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaida silaha uliyoitaja inatakiwa kuwa katika mikono ya vyombo vya ulinzi,lakini imetokea Mara kadhaa silaha zimeangukia katika mikono ya wahalifu, hivyo ni Busara tuache vyombo vya usalama vifanye uchunguzi waovu hawa watajulikana, sio jambo jambo jema kuanza kuhisi mambo usiyokuwa na uhakika nayo ukachanganya na USHABIKI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha uongo, mrema na lipumba hawakuwahi kuwa wanasheria kama Lisu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaza kwa mawazo mapana sana tena sana na ninaumia moyo sana , pamoja na UCCM wangu wa damu kabisa lakin nadiriki kusema hali hii haimpendezi mungu ,TUNALITIA LAANA NA NAJISI TAIFA LENYE BARAKA .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…