Katika andiko langu la awali nilizungumzia nadharia ya fremu (framing theory) na jinsi inavyoweza kutusaidia kuwajua "WATU WASIOJULIKANA" katika shambulizi la risasi dhidi ya Mbunge Lissu.
Nilisema ukitaka kujua hisia za mtu, mrengo wake na anachowaza basi soma maandishi yake.
Moja ya swali kuu leo ambalo nadharia ya fremu inatusaidia ni kujua ni nani waliohusika na shambulizi dhidi ya Lissu.
Uchambuzi, michango mingi na hata maandishi katika magazeti mengi makubwa nchini, yakitazamwa katika nadharia ya fremu, vinaibua kundi jipya linaloweza kutusaidia katika sakata hili la Lissu ambalo nitaliita tu la "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA."
Ukitaka kuwajua "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA" na uhusika wao ktk kumdhuru Lissu soma post za mwanzo tu za vijana wa Chadema waliorusha picha zinazodaiwa kuwa za Lissu na nyingine Mbowe akiwa hospitali.Picha zile 2 alipiga nani?Kwa nini mpigani alipiga picha 2 tu?Au kama alipiga nyingi kwa nini alisambaza picha 2 tu? Hapa kuna "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA."
Ukisoma magazeti ya Tanzania Daima na MwanaHalisi ya leo utakutana na simulizi nyingi baadhi zikimkariri hata Lissu akiwa hoi ICU eti akieleza kuwajua "WATU WASIOJULIKANA."
Ukisoma magazeti hayo utakubaliana nami kuwa kwanza kuna "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA" wanaomsemea Lissu kila siku.
Lakini pia ukitumia nadharia ya fremu utabaini kuwa vyombo hivi vinavyojinasibu na uchambuzi na uchunguzi ghafla kwa sasa vinaonekana kupewa taarifa za kuokoteza na "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA" ambao wanaonekana wako Nairobi ama Lissu akiwa anawajua au hawajui.
Ni watu hawa "WASIOTAKA KUJULIKANA" ambao wanapenyeza habari nyingi kuhusu Lissu na bahati mbaya au nzuri nadharia ya fremu inatuonesha dhahiri walikuwepo Dodoma Lissu akiwa hoi anaugulia maumivu ya risasi mwilini na sasa wako naye Nairobi akiuguza majeraha ya risasi zilizotolewa.
Je nadharia ya fremu inatuambia nini zaidi kuhusu watu hawa "WASIOTAKA KUJULIKANA" waliotufanya tuhangaike na "WATU WASIOJULIKANA" ktk sakata hili la Lissu?
Endelea kufuatana nami hatua kwa hatua na nadharia ya fremu.
Episode ijayo tutaeleza Je, Kubenea anajua nini kuhusu "WATU WASIOTAKA KUJULIKANA," na kwa nini anachokijua ni muhimu katika sakata hili?
Usikose
Political Jurist, UDOM.