Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Polisi Dodoma: Mwenye taarifa kuhusu waliompiga Lissu risasi apeleke polisi

Huo utafiti uliuanzia wapi? Au ulianzia pale alipopigiwa risasi?
 
Sina hulka ya kutokukuamini Mzee Tupatupa, lakini hili nina mashaka nalo kidogo unless udokeze kidogo kuwa yule jamaa yetu kutoka Bandari salama alilala wapi ili niunganishe na habari nisikiazo na kama zitalandana basi nitajua kuwa kweli uchunguzi wako ulikuwa makini
 
Mimi sioni sababu ya kuhangaika kumtafuta muhusika wakati ushahidi wa kimazingira unainesha wazi nani muhusika! Hata mtoto wa kindergaten anamjua!
 
Umeanza kujidhalilisha lini km hukutuwekea hapa basi huouchunguzi wako niwa WASIOJULIKANA
 
"Bunduki za nini jamani kwenye kujenga hoja?"
Kwa mstari huo,utafiti wako umepata jibu kuwa,walioshindwa hoja ndio walotaka kumuua Lissu!! YAWEZEKANA KABISA
 
Pia tunaomba uende Myanmar ukafanye utafiti ya juu kinachojiri pale kati ya serikali ya warohingya mrejesho utauleta humuhumu
 
Tutamptibu popote pale wakiomba!! Lazima akatibiwe Muhimbili!! Wabunge wamechanga pesa za Matibabu!! Lissu ana haki kama Mbunge kutibiwa!!!
 
Kwa majuma kadhaa nilikuwa hapa Dodoma kwa kazi maalum lakini binafsi. Nilikuja hapa kupata dondoo kuhusu nini hasa kilitokea kabla, wakati na baada ya shambulio la risasi la Mbunge Tundu Lissu. Nimeyapata ya kuyapata na kusikia ya kuyasikia.

Niliyoyapata nitayakabidhi Polisi kwa namna nitakayoona inafaa kuitikia wito wa kuwasilisha 'taarifa' yoyote. Lakini, nitayahifadhi kwa kumbukumbu zangu na, ikiwezekana, kumkabidhi Mhusika atakaporejea.

Sikupata mengi lakini nimayapata ya muhimu. Nitayaweka kwa vyombo husika ili viyafanyie kazi pamoja na taarifa, nyaraka na kumbukumbu nyingine. Polisi watatenda hadi wananchi watapenda. Polisi wako imara kila idara. Sasa, narejea Kibiti Pwani.

Bunduki za nini tena jamani kwenye kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Mkuu acha hadithi za kitoto, ati humu kwenye chungu kuna nyama ya kuku, lakini msifunue mfuniko mpaka kesho!
 
Kwa majuma kadhaa nilikuwa hapa Dodoma kwa kazi maalum lakini binafsi. Nilikuja hapa kupata dondoo kuhusu nini hasa kilitokea kabla, wakati na baada ya shambulio la risasi la Mbunge Tundu Lissu. Nimeyapata ya kuyapata na kusikia ya kuyasikia.

Niliyoyapata nitayakabidhi Polisi kwa namna nitakayoona inafaa kuitikia wito wa kuwasilisha 'taarifa' yoyote. Lakini, nitayahifadhi kwa kumbukumbu zangu na, ikiwezekana, kumkabidhi Mhusika atakaporejea.

Sikupata mengi lakini nimayapata ya muhimu. Nitayaweka kwa vyombo husika ili viyafanyie kazi pamoja na taarifa, nyaraka na kumbukumbu nyingine. Polisi watatenda hadi wananchi watapenda. Polisi wako imara kila idara. Sasa, narejea Kibiti Pwani.

Bunduki za nini tena jamani kwenye kujenga hoja!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
HABARI MPYA: Kamanda wa Polisi Dodoma amesema yeyote mwenye taarifa kuhusu wahusika waliompiga risasi Tundu Lissu waiwasilishe polisi.

Kwa sasa wamepata taarifa kuwa gari iliyoonekana ni gari nyeupe aina ya Nissan.

Naye mkuu wa mkoa wa Dodoma amesema polisi wameshaanza kufanya upelelezi kuhusu wahusika na kusema watu waendelee kusubiri taarifa kutoka kwenye jeshi hilo

Amesema hawatapenda kuona mikusanyiko sehemu yoyote ya Dodoma mjini kwa sababu jeshi la polisi bado linafuatilia asili ya tukio lenyewe na mikusanyiko ya watu inaweza kutumika vibaya.
Pia wataendelea kuwafaamisha raia kwenye kila hatua watakayofikia

Jamani muogopeni Mungu.Kumbe uchunguzi bado haujaanza pamoja na vyanzo vya kuanzia vikiwa wazi hivyo.Mbona tunachezeana akili hivi?si vizuri kuichukia nchi yako lkn,hawa watu watulazimisha kutenda hiyo dhambi!Na kibaya zaidi hatujui nchi nyingine ya kwenda kuishi!
Yaani inakera mno!kibaya zaidi sasa imefika mahali unaoneshwa ubabe waziwazi!
adc7684e7b5f47745028ccb004d3f1db.jpg

[HASHTAG]#Mwananchileo[/HASHTAG]
 
Wasalam, natafakari kwa kina sipati jibu kichwa kinauma. Nafikiri wakati umefika sasa serikali yetu sikivu ya ccm na jeshi la police watuambie ni kinanani walitaka kumuua tundu lisu kama wamekwama waunde tume ya kimahakama ichunguze swala hili, au waruhusu vyombo huru vya uchunguzi kutoka nje ya nchi yetu. Ova.
 
Serekali inawatu wengi,pamoja na mimi pia ni serekali,lakini wauaji ni wawili tu kutoka serekalini.
Labda tumuachie tu mungu ila kusemakua kuna serekali itakuja isimame kidedea kukwambia muuaji utasubiri sana.
 
Hakuna haja ya kutuelezaa kusoma ushindwe hadi kusoma picha tushindwee wajameni aghhh
 
Back
Top Bottom