Polisi Michael Rasha Atoa ujumbe kwa IGP Wambura. Rais Samia ampe Ukuu wa Wilaya

Polisi Michael Rasha Atoa ujumbe kwa IGP Wambura. Rais Samia ampe Ukuu wa Wilaya

Mkuu heshima kwako.

Kweli kuna mapolisi wana roho ya kiungwana sana.

Nimemkumbuka mmoja Kati ya Igunga na Nzega wakati barabara ya lami inajengwa..alisaidia watu tuliokuwa tunasotea kazi.

Kila siku chakula cha mchana tulikula kwake.

Pia ni mkulima alikuwa na TATA jeupe...bakhti mbaya jina limenitoka.
Jitahidi kufuatilia yulijue jina lake. Ili abaki kwenye kumbukumbu.
 
Kumbe sio kila Polisi ana roho mbaya wala katili. Wapo Polisi baadhi wema.

Yupo Rasha mmoja kwa Polisi 1,000. Sema watu kama hawa wanakomolewa kwa kupelekwa Vijiji vya ndani ili wasionekane kitaifa.

Rasha alitakiwa ahudumie japo Wilaya nzima sio kata tu.

Wanaotenda mema bila kujali mapito yao, tuwatie moyo

Nilimshuhudia akivusha wanafunzi kwenye mto uliofulika wengine akiwabeba Mgongoni.

Mungu amlipe nini?
View attachment 2822021
Polisi Kata wa Kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha akiongea na kumfariji mtoto Erick Hongera (6 ) ambaye amekuwa akikaa kwa upweke katika maeneo ya Shule.

Mtoto Erick amekuwa na mazoea ya kwenda shule ya Msingi Manda Juu na kukaa nje ya jengo la shule hiyo kwa upweke na mfadhaiko kutokana na wazazi wake kutokumpeleka shule.

Mkaguzi Rasha ameongea nae na kumfariji ili kuona ni jinsi gani anaweza kumsaidia aweze kujiunga na watoto wenzake ili kupata haki yake ya msingi ya kusoma.

Katika harakati za kumsaidia mtoto huyo, Mkaguzi Rasha amechukua hatua ya kwenda kuongea na wazazi wake ili kujua changamoto na kuitafutia ufumbuzi ili mtoto huyo aweze kwenda shule kama wanafunzi wenzake.

Credit: Picha na caption nimeitoa Channel ten
Hongera kwake
 
Hizo hela zinazotumiwa vibaya na mama urojo kununua magoli sijui kulipia viingilio mashabiki ambao hawajaomba kulipiwa Mara elfu 10 zingetumika kusaidia watoto maskini kama hawa ingeleta maana
 
IMG_1342_Original.jpg

Igp mwenyewe sasa baada ya kusoma hii taarifa.
 
Mkuu nampongeza askari kwa Wema aliufanya na ndio maana halisi ya kuwa askari!
Lakini napingana na wewe kwenye swala la kupewa ukuu wa wilaya…sasa watu wema wote wakipewa vyeo uko mtaani tutabaki na wakina nani? Kwanini hawa watu wasibaki mtaani ili kusambaza wema?
Mbona tutaanza kutengeneza taifa la wanafiki wanao vizia vyeo mkuu? Kwani askari huyo akipewa zawadi nyingine zaidi ya ukuu wa wiaya?
 
Ndio! Hawa ndio askari tunaowataka katika nchi yetu. Anajua nini maana ya uzalendo. Sio uzalendo wa maneno vitendo zero! Huyo ameakisi kilichopo moyoni. Mungu akubariki Kamanda.
 
Acha makasiriko. Hili ni Jukwaa huru kwa kila mtu kusifia apendacho. Sasa unataka usifie upande wako tu. Tuwape nafasi watu waseme. Tukosoane kwa upendo na kuelekezana kwa heshima
Kuna nilipomtukana mtu mimi?

Kusema “Ungekuwa na akili” haijawahi kuwa tusi useme nimemkosea mtu heshima hiyo ni lugha sahihi kabisa ya kuelekezana kwenye mijadala.
 
Kumbe sio kila Polisi ana roho mbaya wala katili. Wapo Polisi baadhi wema.

Yupo Rasha mmoja kwa Polisi 1,000. Sema watu kama hawa wanakomolewa kwa kupelekwa Vijiji vya ndani ili wasionekane kitaifa.

Rasha alitakiwa ahudumie japo Wilaya nzima sio kata tu.

Wanaotenda mema bila kujali mapito yao, tuwatie moyo

Nilimshuhudia akivusha wanafunzi kwenye mto uliofulika wengine akiwabeba Mgongoni.

Mungu amlipe nini?
View attachment 2822021
Polisi Kata wa Kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha akiongea na kumfariji mtoto Erick Hongera (6 ) ambaye amekuwa akikaa kwa upweke katika maeneo ya Shule.

Mtoto Erick amekuwa na mazoea ya kwenda shule ya Msingi Manda Juu na kukaa nje ya jengo la shule hiyo kwa upweke na mfadhaiko kutokana na wazazi wake kutokumpeleka shule.

Mkaguzi Rasha ameongea nae na kumfariji ili kuona ni jinsi gani anaweza kumsaidia aweze kujiunga na watoto wenzake ili kupata haki yake ya msingi ya kusoma.

Katika harakati za kumsaidia mtoto huyo, Mkaguzi Rasha amechukua hatua ya kwenda kuongea na wazazi wake ili kujua changamoto na kuitafutia ufumbuzi ili mtoto huyo aweze kwenda shule kama wanafunzi wenzake.

Credit: Picha na caption nimeitoa Channel ten
Hawa ni binadamu kama wengine! Ila kuna mashetani waliokalia viti vya uongozi wa dola wanawatumia kwa sababu ya changamoto za umaskini tu.
Nilikamatwa na trafick nikiwa na rafiki zangu mwaka jana. Yule trafick akaanza kujadili rushwa kwa kunitaka kutoa rushwa.
Kumbe machalii kwenye gari walikuwa wanamrekodi kwa kamera za simu. Ndipo mmoja wao akanitamkia tushuke anisaidie kuongea na askari. Akaoneshwa rekodi yote na picha jinsi alivyoanza tukamtisha kwa ubabe haswa. Kijana alilia akataka hata kutupa rushwa sisi. Alidai hiyo hela inaenda hadi kwa IGP na kwamba asipofikisha "lengo" atarudishwa bench au vijijini>>>>Alilia machozi na akapiga magoti! TUlimuonea huruma na kumuacha
 
Wewe ni mgeni hapa Tanzania.
Hujiulizi kwanini alitoa huduma hiyo huku yuko ndani ya uniform?
Ni nani alichukua picha wakati huyo police officer akitoa huduma?
Polisi Tanzania mema mawili mabaya mia.
Hata hawa polisi unaowaona wazembe siku ukiua utajua kuwa si wazembe na utahisi kila mahali wanakufuata
 
Mkaguzi kachukua hatua sahihi kabisa, kwanza, kwenda kusikiliza tatizo kwa Wazazi. Hivi ndivyo suluhu ya jambo inavyotatafutwa

Kwa upande mwingine sisi kama Taifa tumefeli. Huyu mtoto 'akiwa Ali Dangote' ( Mungu saidia asiwe) tunalaumu Wazazi na mtoto. Tunashindwa kuelewa hatukumuandaa kuanzia utotoni.

Tupo bize kuangalia ma V8 mangapi yatanunuliwa kwa viongozi gani.
Tupo Bize kushabikia Wabunge wanaogawa kofia na vitenge
Tupo Bize kutunga sheria za kuwalipa Wapenzi wanapostaafu kwa kisingizo cha '' wenza wa viongozi''

Tunapata wapi fedha za kuhudumia hayo hapo juu! kutoka kodi za Baba na Mama wa huyu mtoto au huyu mtoto mwenyewe siku atakapoweza kubeba gunia sokoni kwa mgongo.

Pascal Mayalla JokaKuu
Very pathetic. Mkaguzi apewe maua yake.
 
Na madelu anaweza kupita mitaa hiyo na viieite lake kafunga vioo full, nchi hii watu wanapenda umwinyi sana...
 
Back
Top Bottom