Polisi Michael Rasha Atoa ujumbe kwa IGP Wambura. Rais Samia ampe Ukuu wa Wilaya

Ndio! Hawa ndio askari tunaowataka katika nchi yetu. Anajua nini maana ya uzalendo. Sio uzalendo wa maneno vitendo zero! Huyo ameakisi kilichopo moyoni. Mungu akubariki Kamanda.

Jamii inataka polisi wa aina hii,serikali ya ccm inataka polisi tulio nao[emoji1784][emoji1784][emoji1784]
 
Kumbe sio kila Polisi ana roho mbaya wala katili. Wapo Polisi baadhi wema.

Yupo Rasha mmoja kwa Polisi 1,000. Sema watu kama hawa wanakomolewa kwa kupelekwa Vijiji vya ndani ili wasionekane kitaifa.

Rasha alitakiwa ahudumie japo Wilaya nzima sio kata tu.

Wanaotenda mema bila kujali mapito yao, tuwatie moyo

Nilimshuhudia akivusha wanafunzi kwenye mto uliofulika wengine akiwabeba Mgongoni.

Mungu amlipe nini?
View attachment 2822021
Polisi Kata wa Kata ya Usangule Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Michael Rasha akiongea na kumfariji mtoto Erick Hongera (6 ) ambaye amekuwa akikaa kwa upweke katika maeneo ya Shule.

Mtoto Erick amekuwa na mazoea ya kwenda shule ya Msingi Manda Juu na kukaa nje ya jengo la shule hiyo kwa upweke na mfadhaiko kutokana na wazazi wake kutokumpeleka shule.

Mkaguzi Rasha ameongea nae na kumfariji ili kuona ni jinsi gani anaweza kumsaidia aweze kujiunga na watoto wenzake ili kupata haki yake ya msingi ya kusoma.

Katika harakati za kumsaidia mtoto huyo, Mkaguzi Rasha amechukua hatua ya kwenda kuongea na wazazi wake ili kujua changamoto na kuitafutia ufumbuzi ili mtoto huyo aweze kwenda shule kama wanafunzi wenzake.

Credit: Picha na caption nimeitoa Channel ten
Hii ndio maana ya Utu.
 
Ulinzi na usalama wa raia.
Katimiza jukumu la msingi na nadhani huenda akaibua mengi yanayomsibu huyo mtoto.
 
Kwa hakika Nampongeza kabisa kwa moyo wake huo wa upendo na ukarimu mkubwa sana wa kumsaidia mtoto huyo . Hiyo ni sadaka kubwa sana mbele za Mwenyezi Mungu ambayo anaipokea moja kwa moja.

Mungu atamlipa kwa wema wake na uungwana wake alioutenda kwa mtoto huyo.atamlipa zaidi ya msaada anaoutoa.

Nasi wengine hatuna budi kuiga moyo wa namna hiyo kwa kuwatendea wengine wema na hivyo kuwapatia nuru, matumaini, tabasamu na furaha katika mioyo yao iliyokuwa imekata Tamaa,kuvunjika moyo,kuona giza mbele,kuwa na upweke na kukosa matumaini.
Nikadhani unataka maelekezo ya kina ili umpeleke kwa unayempigiaga domo kila dakika hapa?
 
Hongera kwake huyu jamaa,ni mfuatiliaji mzuri wa mambo akionekana atafika mbali.

Nime-zoom kumtizama huyo mtoto nikamtizama na mwanangu hapa pembeni yangu hadi huruma,Tanzania tuna hali ya umaskini mbaya sana viongozi angalao wawakumbuke watoto kama hawa wanaotafuta faraja ya kupata hii elimu yetu ya kuunga unga.
Umeongea kwa uchungu sana Mkuu...wamo humu WANAPITA
 
Back
Top Bottom