Polisi wamenitrack niliokota simu, kesho natakiwa kituoni

Huyo mamako alikudanganya. Alienda kudanga akahongwa hiyo simu na mwizi au jambazi, muulize vizuri.

Babako unamjuwa? Mnaishi nae?
Dah umemkosea sana huyo jamaa.

Leo nimeconfirm kichwani ni mtupu hadi sio poa.
 
Zima simu potea. Waachane na wewe.
Apoteee aende wapi......huyu wanaye pamoja sambamba kama Tako na kiuno.... Laini si ya kwake na imeshasomeka na inajulikana ...watazaa naye huyu. .
 
Mkuu kuokota simu kupo, ila ni vyema ukaiacha hewani ili mwenye nayo akipiga upate kumrudishia. Huu ndio ubinadamu.
 
hio haisaidii simu wanatrack kupitia IMEI namba hivyo laini yoyote utakayoweka inaleta taarifa zako na huyu mleta mada aliweka laini yake tayari system imemtambua hasa kama laini aliyoweka alisajili kwa NIDA yake ndio kabisa hana ujanja
Simu naitupa kabisa,natumia simu yenye imei nyingine na laini nyingine kabisa,hapo vipi mkuu?
 
Sure. Kimasihara sana jamaa anaenda jela.

Hii ni sehemu ya kula ya polisi.
Hapo wanaweza kumpa kesi ya mauaji. Yaani watasema mwenye simu hii aliuawa. Ukiiona simu popote pale kimbia spidi zote maana huo ni msala.
 
Ulitakiwa ukaripoti polisi kuwa umeokota simu ..
 
Ukiokota simu peleka polisi au tangaza gazetini.

Kwanza hata usitangaze, unaweza kuokota kitu kinachoonekana simu kumbe ni bomu la kujilipua lenyewe kama huko Lebanon.
Siku moja gari la Magereza lilipita spiidi ikadondoka kofia ya afisa magereza. Nikapeleka kituo cha polisi. Yaani pamoja na wema niliofanya niliulizwa maswali mengi sana. Moja ya maswali waliniuliza.
" Kofia kama hii kwanini umeileta polisi kwanini usiiache hapo hapo?"
Swali la kimtego nikawajibu kwamba Kofia hii ina nembo halisi ya jeshi la polisi magereza, kama mhalifu ataipata kazi yake itakuwa ndogo sana ni kujishonea mag Wanda na akikamilisha ataenda gereza lolote na kujifanya askari akafanya uhalifu wowote.
Huwezi amini niliachiwa nikarudi nyumbani. Kesho yake nilipoenda kuripoti nikaambiwa jamaa alienda kituoni kuulizia kama kuna kofia imepelekwa pale. Niliikuta elfu kumi zawadi.
 
Sasa nawewe kwan ulihangaika hivyo? Mimi wangenikuta ndo nakojolea wakati wanarudi kuitafuta
 
Anaeokota simu ndio kama huyo anamrudishia mwenyewe au anaisalimisha polisi. Huyu anaeokota na kuanza kuitumia ni mwizi na akitaka kujua akaripoti polisivwanakomuhitaji aende.
 
Hiyo pochi ya mfukoni au ya begani?
Maana kwa fedha hiyo kapochi kulikuwa kakubwa bila shaka
 
Kuna jamaa na yeye alikutana na binti anazurulazurula na nguo za shule (primary) kama km 20 nje ya mji.Kumuuliza binti haelewi.Akamlipia nauli akampeleka kituo cha polisi.Kwa kifupi jamaa alikoma sidhani kama atarudia tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…