Polisi wamgomea Lissu kufanya mikutano Ngorongoro, yeye asema ataenda kwani sehemu hiyo sio Gereza

Polisi wamgomea Lissu kufanya mikutano Ngorongoro, yeye asema ataenda kwani sehemu hiyo sio Gereza

Samia ni zimwi kabisa, hivi huko Ngorongoro wanaficha kitu gani? huyu mwanamke ni mtu wa ajabu na hatari sana, asiye huruma kabisa.

Sasa ameamua kutumia cheo chake kuwanufaisha anaowajali yeye, wala hatujali watanganyika alioapa kuwatumikia.

Huyu mtu anastahili kabisa kupelekwa mahakamani kwa kukiuka kiapo alichoapa, amegeuka msaliti wa wazi kabisa asiye na chembe ya aibu.

Sitaki kuamini siku hizi ndani ya nchi yetu kuna sehemu hatutakiwi kukanyaga, huku ni kuvunja sheria makusudi, halafu akiambiwa ukweli anasema ameziba masikio na kutafuta uadui na watu, huyu dikteta mwanamke ni balaa kabisa.

Wajue tu, vile wanavyozidi kuzuia watu wasiende Ngorongoro ndivyo ambavyo wengi watataka kujua wanachoficha huko, iko siku ukweli utafahamika.
Kuna clip inatembea mtandaoni na hao watu ni waarabu wakiwa na bendera ya Tanzania wakiimba na kushinikiza kiiSlam! Nini hasa kinajiri bado kitendawili. Mwenye nayo atupie humu!
 
Unao ushahidi wa hili, au unajiandikia tu na wewe uonekane upo mtandaoni?
Kama usemayo ni kweli, basi tumefikia hatua ambayo hatujawahi kuifikia kama taifa. Kama hili lipo,, kuna makubwa yatakayofuata.
Hili siyo jambo la kufichika kama lipo.
Unataka ushahidi nikuletee kwenye matacle yako k3ng3 wewe?
 
Nimeonesha wasiwasi kuwa, Dola inaweza kutumiwa vibaya na Viongozi katika kunyanyasa wasio na hatia.

Ndiyo maana kama unakumbuka hata baadhi ya Viongozi wa dini wamewahi kuhojiwa uraia wao nyakati fulani baada ya kuonekana wana ikosoa Serikali

Baadhi ya wafanyabiashara kukumbana na nguvu ya dola baada ya kuonekana wapo upinzani.

Baadhi ya Viongozi wa Upinzani kufanyawi blackmailing hadi kulazimika kuhamia upande wao na wengine ndiyo hao akina Lissu waliokumbana na madhila ya dola hadi kupata ulemavu wa kudumu.
=======
Hoja yangu ni kuwa pamoja na madhira yote hayo Wananchi wamekuwa kimya bila kuchukua hatua kuonesha wamechoshwa na unyanyasaji huu.

Kwahiyo unaweza kupatwa na madhira makubwa lakini hutaona msaada kutoka kwa Wananchi hawa walau kuwafanya Serikali ibadili namna ya kudeal na raia wake.

Mifano ni mingi ya watu waliofanyiwa mambo ya hovyo bila kupata msaada wowote kwa raia wenzake jambo linalofanya wengine kuingia na woga unapo-deal na dola.
Mkuu, nilikuelewa vizuri kabisa hoja yako toka mwanzo.

Haya unayoyasema hapa siyo kwamba waTanzania hawayaoni au hayawasumbui. Nadhani hoja yako ingepata uzito zaidi kama ungejikita katika kutaka kujua kwa nini hali iwe hivyo?

Kwamba waTanzania hawa hawajali kunyanyaswa na serikali yao?

Kwamba wapo tu hayawahusu yanayowapata wezao?

Kwamba waTanzania hawa wanaiogopa serikali kwa vile ina mitutu ya bunduki nyuma yake?

Binafsi siyaamini majibu ya hayo maswali hapo juu.
Nijuavyo mimi, waTanzania hawa wanayajua yote haya na yanawasumbua sana kwamba yanatokea nchini mwao.
Kinachokosekana miongoni mwao ili washughulike na kuibadili hali hiyo ni uongozi tu unaoweza kuwaweka pamoja kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya.

Hali sasa imefika pabaya zaidi, na uamzi watauchukua hata kwa kutumia uongozi wasiokuwa nao imani kubwa, mradi tu uwaongoze kutoka kwenye hii hali duni inayozidi kuharibika kila siku.

Kwa hiyo nakusihi uvute subira kidogo, na ushiriki kwa kiasi chako hapo ulipo wewe.
 
Polisi wamekataza mikutano yetu ya hadhara Ngorongoro. Juzi Serikali ya Samia imekataza wabunge wa Ulaya kutembelea eneo hilo. Wanaficha kitu gani? Licha ya jitihada za Serikali, Ngorongoro sio gereza & Wamaasai sio wafungwa wa gereza hilo. Sisi tutakuwa Ngorongoro kuanzia kesho!

Tundu Lissu
Mtandao wa X
Tunapenda kukufahamisha kuwa barua yako tajwa tumeipokea ikiwa na maudhui ya kufanya vikao vya ndani na mikutano ya hadhara maeneo ya kata 3 zizopo tarafa ya Loliondo na kata 3 zilizopo tarafa ya Ngorongoro.

Hata hivyo tarafa ya Ngorongoro ni eneo la Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro na kwamba kuingia na kutoka eneo hilo ni sharti kufuata taratibu zinazosimamia eneo hilo (kupata kiball kutoka Mamlaka ya Ngorongoro).

Aidha kwa upande wa tarafa ya Loliondo kulingana na tarifa mbaimbali tulizo nazo haziruhusu kufanya shughuli za kisiasa hasa mikutano ya hadhara.

Kutokana na sababu hizo hapo juu, tunaelekeza kwamba usitishe mikutano hiyo kwa sasa hadi wakati mwingine ambao utakuwa mwafaka kwa ustawi wa amani na utulivu wa wilaya yetu.

Kwamba?

"Hata hivyo tarafa ya Ngorongoro ni eneo la Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro na kwamba kuingia na kutoka eneo hilo ni sharti kufuata taratibu zinazosimamia eneo hilo (kupata kiball kutoka Mamlaka ya Ngorongoro)."

Hiiiiiiiii bagosha! --- nabii jiwe katika maneno yake.
 
Nadhani wanakosea. Rais Dkt Samia hataki uminyani ya uhuru wa siasa. Hawa polisi wanakosea. Mh. Lisu hata fanyeje hakubaliki kabisa. 2025 ni Dkt Samia pekee ndiye anapendwa zaidi. Polisi wamuache azurule atakavyo maana kukaa ndani ulaya kumemchosha sana. Ukizingatia hana mshahara hizo ndiyo per diem zake jamani.
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Chawa Force Unit
 
Nilijua tu kuwa wewe ni bwege mmoja asiyekuwa na mbele wala nyuma.
Njoo ule maisha huku na watoto wakali wewe, NJAA na UJIRA wa kusifia uhalifu na upumbavu zitakuua huko Lumumba

Tafuta pesa.jpg
 
Unao ushahidi wa hili, au unajiandikia tu na wewe uonekane upo mtandaoni?
Kama usemayo ni kweli, basi tumefikia hatua ambayo hatujawahi kuifikia kama taifa. Kama hili lipo,, kuna makubwa yatakayofuata.
Hili siyo jambo la kufichika kama lipo.
Vitisho vya kitoto kabisa hivi, wewe ni mnufaika wa huo UHARAMIA wa serikali ya ccm? Ni shahidi ngapi zimepelekwa kwenye mamlaka husika na hazijawahi kufanyiwa kazi? Grow up black man
 
Njoo ule maisha huku na watoto wakali wewe, NJAA na UJIRA wa kusifia uhalifu na upumbavu zitakuua huko Lumumba

View attachment 2743595
Si nilisema wewe ni bwege tu, kumbe hukuelewa?

Kama haya ndiyo maisha unayoyasujudia, huoni kuwa wewe ni bwege kwelikweli?

Hapo na hao watu wana lipi la ziada linalokufanya wewe kutamani maisha hayo?
 
Vitisho vya kitoto kabisa hivi, wewe ni mnufaika wa huo UHARAMIA wa serikali ya ccm? Ni shahidi ngapi zimepelekwa kwenye mamlaka husika na hazijawahi kufanyiwa kazi? Grow up black man
Vitisho hapo vipo wapi?
Ulichofanya hapa ni kuthibitisha kwamba unajiropokea tu mambo bila ya kuwa na uhakika wowote wa uwepo wa mambo hayo.

Hovyo kabisa.
 
Kuna simba 4,na chui watatu wameonekana wakizurura maeneo husika na ndio sababu ya Mamlaka husika kuzuia watu kudhuru maeneo hayo ni kwa usalama wao, msijie mkaliwa na Simba mkaitupia lawama serekali.
 
Kwamba?

"Hata hivyo tarafa ya Ngorongoro ni eneo la Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro na kwamba kuingia na kutoka eneo hilo ni sharti kufuata taratibu zinazosimamia eneo hilo (kupata kiball kutoka Mamlaka ya Ngorongoro)."

Hiiiiiiiii bagosha! --- nabii jiwe katika maneno yake.
Taratibu zote zimefuatwa, vibali vimetolewa na TANAPA, Sasa Polisi wanafanya kazi isiyowahusu.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Samia ni zimwi kabisa, hivi huko Ngorongoro wanaficha kitu gani? huyu mwanamke ni mtu wa ajabu na hatari sana, asiye huruma kabisa.

Sasa ameamua kutumia cheo chake kuwanufaisha anaowajali yeye, wala hatujali watanganyika alioapa kuwatumikia.

Huyu mtu anastahili kabisa kupelekwa mahakamani kwa kukiuka kiapo alichoapa, amegeuka msaliti wa wazi kabisa asiye na chembe ya aibu.

Sitaki kuamini siku hizi ndani ya nchi yetu kuna sehemu hatutakiwi kukanyaga, huku ni kuvunja sheria makusudi, halafu akiambiwa ukweli anasema ameziba masikio na kutafuta uadui na watu, huyu dikteta mwanamke ni balaa kabisa.

Wajue tu, vile wanavyozidi kuzuia watu wasiende Ngorongoro ndivyo ambavyo wengi watataka kujua wanachoficha huko, iko siku ukweli utafahamika.
Trh 1 mwezi ujao jiandae kuwa msitali wa mbele hili mkamtoe ikulu
 
Back
Top Bottom