Masiihi Dajal
Member
- May 30, 2017
- 13
- 9
Najiuliza mwisho wa Profesa Lipumba kisiasa utakuaji. Hivi siasa inaweza kukufanya usahau siku moja utaondoka hapa duniani. Taifa linapoanza kutumia hila kuchochea migawanyiko kumbuka haiishii kwenye vyama. Kumbuka tayari mwanasiasa anaposahau kuwa unapotumiwa thamani yako inapungua na unapoteza ubinadamu. Kuwa Profesa au Doctor bila ya hekima ni hatari kubwa. Pale unapoona kiongozi anatumia mabavu kutawala ni kipimo cha kutosha kwamba panakosekana hekima. Hekima ni nini, wengi wanafikiria ni busara. La hasha ni zaidi ya Hilo. Hekima ni mizani ya kufanya mazingatio Kabla ya kufanya lolote. Tanzania ina matukio makubwa mawili wiki hii: kunyimwa dhamana Lissu na kukubali spika kufukuzwa wabunge wa CUF. Bila ya kutumia hekima taifa litazidi kugawanyika. Nakumbusha balaa zinazotokea nchi nyingine zinaanza na kukosekana busara. Matarajio ya wenye hekima; viongozi ambao walitumikia ngazi za juu za uongozi kuwashauri watawala. Haya na mengine mengi yasipotafutiwa ufumbuzi wa kisiasa tunajitengenezea matatizo ambayo wakati huo Lipumba na washirika wake watakuwa wameshaondoka ni vizazi vyetu ndio vitapata matatizo. Hakuna faida ya kunadi tunataka tulipwe pepo, au kuwa na sijida kubwa au kubusu mikono ya makuhani, huku tunawazuia watu ambao kosa lao ni kutuonya. Hatutaki kuonywa, kukosolewa kwa nini tunajiingiza kwenye uongozi?