Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Najiuliza mwisho wa Profesa Lipumba kisiasa utakuaji. Hivi siasa inaweza kukufanya usahau siku moja utaondoka hapa duniani. Taifa linapoanza kutumia hila kuchochea migawanyiko kumbuka haiishii kwenye vyama. Kumbuka tayari mwanasiasa anaposahau kuwa unapotumiwa thamani yako inapungua na unapoteza ubinadamu. Kuwa Profesa au Doctor bila ya hekima ni hatari kubwa. Pale unapoona kiongozi anatumia mabavu kutawala ni kipimo cha kutosha kwamba panakosekana hekima. Hekima ni nini, wengi wanafikiria ni busara. La hasha ni zaidi ya Hilo. Hekima ni mizani ya kufanya mazingatio Kabla ya kufanya lolote. Tanzania ina matukio makubwa mawili wiki hii: kunyimwa dhamana Lissu na kukubali spika kufukuzwa wabunge wa CUF. Bila ya kutumia hekima taifa litazidi kugawanyika. Nakumbusha balaa zinazotokea nchi nyingine zinaanza na kukosekana busara. Matarajio ya wenye hekima; viongozi ambao walitumikia ngazi za juu za uongozi kuwashauri watawala. Haya na mengine mengi yasipotafutiwa ufumbuzi wa kisiasa tunajitengenezea matatizo ambayo wakati huo Lipumba na washirika wake watakuwa wameshaondoka ni vizazi vyetu ndio vitapata matatizo. Hakuna faida ya kunadi tunataka tulipwe pepo, au kuwa na sijida kubwa au kubusu mikono ya makuhani, huku tunawazuia watu ambao kosa lao ni kutuonya. Hatutaki kuonywa, kukosolewa kwa nini tunajiingiza kwenye uongozi?
 
Lissu ni mzalendo haswa na nchi yake, wako wengine wafia serikali bila uzalendo kwa nchi yao wanajifanya kuwa wazalendo kuliko lissu wakati mikataba yote ya kijinga wameshiriki kuitunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Twende mbele turudi nyuma kipindi cha miaka mitano hapa Tanzania Mwanaume alikuwa mmoja tu.

Kipindi ambacho kila mtu aliufyata hakuna cha waziri, kada, poti wala nani woote walikaa kimya.

Ni mwanaume mmoja tu alibaki tena akiwa hana backup ya vyombo.

Huku aliyekuwa akitisha akiwa na back up ya kila kitu( vyombo)

Huyu mwamba uwezo wake wa kujua sheria na kuzitumia ipasavyo na ujasiri ndio ulimponza.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema tunataka hii nchi iendelee tunahitaji vijana wakorofi wenye uwezo wa kuhoji na kujenga hoja za kisomi. Akaongeza kuwa Nchi haipaswi kuwapa mwanya vijana mbumbumbu.

 


View attachment 547452
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa ha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.


Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

====

UPDATE 1

Mapema kabla, Lissu alipitishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,alikataa kupimwa mkojo kwa sababu kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi.

More to follow

Tunamshukuru sana Mungu kwa mambo mema makuu aliyotutendea March 2021
 
Walikuwa sahihi sana tu.

Chadema wote inapaswa wakamatwe na kupimwa.
 
Back
Top Bottom