Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Mkojo una acid ndiyo unamfanya awe mchochezi, hii ndiyo bongo bhana tusubiri matokeo ya vipimo.
 
Akiweka maji watajuaje kama ni maji au mkojo.. Au unatoa dushe mbele yao?
 


View attachment 547452
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa ha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.


Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

-------------

UPDATE 1
Mapema kabla,Lissu alipitishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,alikataa kupimwa mkojo kwa sababu kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi.

More to follow

Wanataka kumbambikia kesi ya unga kwani mikemia mkuu si Mungu ni binadamu anayepikea Amri toka juu kama wengine huu utawala wa kumbambikia kesi na visasi
 
Wanataka kumbambikia kesi ya unga kwani mikemia mkuu si Mungu ni binadamu anayepikea Amri toka juu kama wengine huu utawala wa kumbambikia kesi na visasi
Kwa hiyo kesi zote zilizopita kwa mkemia mkuu zilikuwa ni za kubambikia?
 
Elimu elimu elimu, sasa uchochezi unapatikana kwenye mikojo? Au vita ya madawa ya kulevya haijawahi kumuacha MTU salama[emoji1] [emoji1]
Inji hii(kwa sauti ya lyatonga)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhe. Tundu Lissu akataa Kupimwa mkojo baada ya kifikishwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwani kipimo hicho hakihusiani kabisa na tuhuma za uchochezi zinazomkabili
 
walimchokonoa mbowe weee, naona kawakalia kimya wakadhani jamaa atakuja juu, wameona hapana wacha waje kwa huyu
 
Mh. Lissu akataa kupimwa mkojo baada ya kufikishwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwani kipimo hicho hakihusiani kabisa na tuhuma za uchochezi zinazomkabili.

Na kuhusu upekuzi mpaka sasa bado unaendelea na karibia wanafika mwisho na Rais wa TLS yuko katika hali mzuri kabisa (kwa mujibu wa mkewe).

Tuzidi kumwombea na kumtia nguvu.

My take: Hivi jamani hawa watu wako vizuri kabisa kichwan? Sasa wanataka wampime mkojo for what?
 
Back
Top Bottom