Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Sina shaka na lissu...hata wamkate mikono nina hakika atasimamia anachokiamini...
 
Daaah kumbe zile kauli huwezi kuzitoa ukiwa mzima aisee!
Watu wamepata pa kutokea hapo!!! sasa na wale wanaoshindwa kumjua Ngedere!! Hizi siasa za awamu hii............. Huko mbele Tanzania yetu itajiweka wapi na siasa zake kama nchi. KWA WA NJE WANAJIONEA SINEMA YA BURE
 
View attachment 547452
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa Kituo cha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.


Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.


Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

More to follow
Wanafikiri hayo majibu ya mkemia yataaminika
 
Mkojo unahusiana vipi na uchochezi? Hii nchi ngumu sana kwakweli


BAADA KUTUMIA AINA HIZO ZA "KINACHOHISIWA", MTUMIAJI HUWA KATIKA HALI KUTOJITAMBUA NA KUPATA UJASIRI WA KUFANYA/KUROPOKA CHOCHOTE ANACHOFIKIRI NI SAHIHI. HEBU ANGALIA "MATEJA" WANAVYO JIAMINI MARA BAADA YA KUTUMIA HASHISHI/AFYUNI. MATOKEO YA KIPIMO CHA MKOJO HUONESHA KAMA MTU ANATUMIA VILEVI HIVYO. KWA HALI ILIVYO "INAWEZEKANA" HUYO ALIYETAJWA NI "TEJA MTANASHATI" TOFAUTI NA "MATEJA" WACHAFU WACHAFU MLIOWAZOEA
 
UNAWEZA KUMKATALIA MTU DHAMANA KUMBE MGONJWA, SASA AKIMALIZIKIA HUMO NDANI ZIKAZUKA TUHUMA ZINGINE
 
So wanahisi kavuta bangi right??
Ebu ngoja ni google nione huo mkojo wa mbunge wetu wanautaka wa nini......hawachelewi kusema tumekamata makontena19 ya makinikia kwenye mkojo wa muheshimiwa.
 
Duh kwumbe mkojo unaweza kuwa kifaa au zana ya kufanya uchochezi wacha nami nikapime wangu nijue kama nina vimelea uchochezi
 
Uchochezi .............. kipimo mkojo!!?

Mtu anatafitiwa kesi ya nguvu!! I hope hakula au kunywa kitu kwenye mazingira ya utata akiwa Kolokoloni!!
 
Dah...jamani nahamgaika na mtu mmoja anayeongea ila hajau-a!! badala ya kuhangaika na kundi la watu wanaou-a ndugu zetu hapa kibiti kweli jamani kweli...aghaaa....mnatengeneza woga kwa watanzania waliowapa kura wakiamini mtakuwa busy kulinda usalama wa nchi na kuleta amani ya taifa?

mnajua kwa sasa watu wamejawa hofu na chuki mioyoni mwao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom