Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

Polisi wampeleka Tundu Lissu kwa mkemia mkuu kupima Mkojo, awagomea..

View attachment 547452
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa ha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo.

Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana.

"Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema.

Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa kuingia na kumuona Tundu Lissu wakiwamo wanasheria wake. Mbali na Fatma, wengine waliokuwapo ni Peter Kibatala na Frederick Kihwelo.

====

UPDATE 1

Mapema kabla, Lissu alipitishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,alikataa kupimwa mkojo kwa sababu kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi.

More to follow

AKILI, TABIA na MWENENDO WAKE LAZIMA APIMWE KAMA ANATUMIA MIHADARATI AU LA!!!
 
Baba alinishauri niwe polisi lkn nikaasema sitoweza mzee labda tuhame nchi ndio niwe polisi. Ninapokuwa ktk majukumu Mimi kufuata jambo kisa mkubwa amesema siwezi. Jeshi la polisi liache kujivunjia heshima ikiwa Hii habari ni ya kweli. Matokeo Yake ni kulidharaulisha jeshi zima.
mkuu hii kazi ya kipuuzi sana hata mimi ilisha nishinda. japo sina kazi ila sijawahi tamani kuwa njagu hata siku moja
 
Unajua kwa watu wa serikali wanavyomwogopa Magu hawaamini kama kuna mtanzania akawa na courage ya kumsema hadharani unless ugoro umemwongezea nguvu. Ndio maana inabidi Lissu wampime kama anatumia dona.
 
Na asipopimwa itaathiri mini?

try me
Nani alifanya uchochez akapimwa mkojo?
We (nna uhakika)ni kijana tumia ujana wako kushughulisha ubongo.

ndio kazi ya polisi kuchunguza kila wanacho kitilia mashaka..........
Sasa wanatilia mashaka mkojo wa Lissu?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Nimesema watambandikia kesi mbaya sana!
Possible,

May Allah bless Me and You
 
Hii Tanzania pengine kweli kama alivyosema rais Magufuli tumerogwa tu. Tuhuma za uchochezi unapima Mkojo na kumsachi nyumbani kwake. Nadhani ni kufuatia maneno yake ndiyo maana yuko mikononi mwa polisi. Sasa mkojo wake una uhusiano gani na maneno ya uchochezi. Pili hivi kuna baadhi ya maneno alibakiza nyumbani. Polisi wetu bhana

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh! Hapo umeniacha hoooiii!!!!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
"Maisha ya mwanaume anayewindwa"

Nitaamini vipi huo mkojo wang unapopimwa nikiwekewa madawa nisingiziwe ngada je
na suala la uchochez na kupima mkojo vinaendana vipi. Yan hata waliomshika hawajui wanamshikia nini ndo maana wanahangaika na kutaka sample ya mkojo for what

Maelekezo na Maamuzi kutoka Juu
Wamemshuku anatumia kilevi ndio maana anaropoka hivyo ni lazima wajiridhishe hakuna kosa kutuhumu au kushuku ni kazi ya polisi. Hata wafungwa waliopo gerezani walishukiwa kwanza.

Kuhusu kutoamini sample ya mkojo kama itabadilishwa ama ala ipo sheria ya kuomba uchunguzi wa haki zaidi Kwa mfano aombe sample zikapimwe Rwanda n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wafuasi wa chama chakavu mmeishiwa hoja mmebaki vihoja.poleni sana hii Tanzania mpya wananchi tunajitambua

Hivi wewe hiyo kadi ya chama ulinichukulia wewe? Nedna kanichukulie umpe Njiwa aniletee huku kijijini kwetu nilipo... mwambie mpelekee Cocochanel atanipata... umeona nakupita bado eeeeeh ka vile unanifahamu shaaaa
 
Wamemshuku anatumia kilevi ndio maana anaropoka hivyo ni lazima wajiridhishe hakuna kosa kutuhumu au kushuku ni kazi ya polisi. Hata wafungwa waliopo gerezani walishukiwa kwanza.

Kuhusu kutoamini sample ya mkojo kama itabadilishwa ama ala ipo sheria ya kuomba uchunguzi wa haki zaidi Kwa mfano aombe sample zikapimwe Rwanda n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfano maneno gani aloyasema yanahusiana na kuhisi anatumia kilevi kwenye ile press?

May Allah bless Me and You
 
Wamemshuku anatumia kilevi ndio maana anaropoka hivyo ni lazima wajiridhishe hakuna kosa kutuhumu au kushuku ni kazi ya polisi. Hata wafungwa waliopo gerezani walishukiwa kwanza.

Kuhusu kutoamini sample ya mkojo kama itabadilishwa ama ala ipo sheria ya kuomba uchunguzi wa haki zaidi Kwa mfano aombe sample zikapimwe Rwanda n.k.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee, kwa rafiki yake bwana yule!!!
 
Back
Top Bottom