PreGE2025 Polisi wamsaka aliyesambaza taarifa za upotoshaji katika ukurasa wa Polisi X (Twitter)

PreGE2025 Polisi wamsaka aliyesambaza taarifa za upotoshaji katika ukurasa wa Polisi X (Twitter)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hiki ni kituko!

Ukisikia mbwa kala mbwa ndio hii sasa🤣🤣 mambo yamekuwa moto taratibu tutaelewana.

Sasa wanamsaka nani wakati page yao ndio imesambaza taarifa hizo za upotoshaji?:KEKLaugh::KEKLaugh::BearLaugh: Nataarifa hii imetoka hapo hapo, sa tunajuaje kama na hii sio ya kwao?

Ila majirani inabidi tuongee vizuri wawa dada na kaka wa East Africa, halafu Nigeria na South Africa watakuwa mabinamu wa EA.

Wabongo nina imani tumepata somo🌚🌚

Pia soma:
=====

TAARIFA KWA UMMA POLISI YAWASAKA WALIOSAMBAZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI MTANDAO X (TWITTER) ​

Jeshi la Polisi linapenda kuwajulisha umma kuwa kuna taarifa za uongo, upotoshaji na zisizo na maadili zilizokuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jeshi la Polisi (tanpol) kwa lengo la kutaka kuuaminisha umma kuwa zimetolewa na Jeshi la Polisi kupitia mtandao wake wa X.

Taarifa hizo si za kweli na ifahamike kuwa Jeshi la Polisi haliwezi kuandaa na kusambaza taarifa kama hizo katika Mitandao yake ya kijamii.

Wakati tunaendelea kufuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo ili wakamatwe, tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na kuepuka kuendelea kuzisambaza endapo zitakufikia. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote yule aliyehusika na utengenezaji na utoaji wa tarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza.

Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

View attachment 3339663
ila poliCCM mmevuliwa nguo
yaani nyie ni watu wa virungu tu!

wenzenu wamesha-advance na ma-drone nyie ata ka-X account tu kanawashinda kulinda
 
Tanpol ambao hawana hata cybersecurity hizi attacks kutokea Kenya watawezaje kuwapata wahusika, wakati wao wamejikita zaidi kwenye kuteka na kupoteza Wapinzani wa Samia.
 
Kuna jamaa alihack account yangu ya jf humu nikawa nashangaa et ninacomment kule kwa jukwaa la siasa tena very serious...

Nikafatilia mpaka leo sijui imekuaje maana nimekuta comment zangu na mimi naponda serikali...

Wakuu mi nawataadharisha ukiona nipo nachangia mambo ya siasa sijui rais sijui lissu jua sio mimi..

Mi mambo yangu ni mishangazi tu ukinitoa hapo utanikuta nipo kule kwa blaza shimba kuangalia wanawake wenye makalio makubwa
 
Pale ambapo wenye akili hawana ajira na vilaza ndio wameshika hatamu ,mambo kama hayo ni kawaida sana.
 
Najaribu kuwaza ndo ingekuwa ya tume ya uchaguzi.

Afu ikulu nayo inatoa neno kukubali matokeo na kukaribisha uongozi mpya.

Mara na akaunti ya Bunge nayo inatoa hongera..

Hivi hali itakuwaje. Tulinde sana hizi akaunti zisidukuliwe kirahis.
 
Too bad waliosambaza ni wakenya wenyewe. badala ya kutafuta aliesambaza, wakae chini kufikiris cybersecurity plan zao, account inakuwaje hacked kirahis hivyo
Si wana intelligentsia ya kujua hata mtu kabla hajaqndamana hao mapolisi wa ccm? Sasa walishindwa nn kujua?
Ati amani ya nchi? Unaimba amani bia HAKI???
 
1000132171.png
 
Hiki ni kituko!

Ukisikia mbwa kala mbwa ndio hii sasa🤣🤣 mambo yamekuwa moto taratibu tutaelewana.

Sasa wanamsaka nani wakati page yao ndio imesambaza taarifa hizo za upotoshaji?:KEKLaugh::KEKLaugh::BearLaugh: Nataarifa hii imetoka hapo hapo, sa tunajuaje kama na hii sio ya kwao?

Ila majirani inabidi tuongee vizuri wawa dada na kaka wa East Africa, halafu Nigeria na South Africa watakuwa mabinamu wa EA.

Wabongo nina imani tumepata somo🌚🌚

Pia soma:
=====

TAARIFA KWA UMMA POLISI YAWASAKA WALIOSAMBAZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI MTANDAO X (TWITTER) ​

Jeshi la Polisi linapenda kuwajulisha umma kuwa kuna taarifa za uongo, upotoshaji na zisizo na maadili zilizokuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jeshi la Polisi (tanpol) kwa lengo la kutaka kuuaminisha umma kuwa zimetolewa na Jeshi la Polisi kupitia mtandao wake wa X.

Taarifa hizo si za kweli na ifahamike kuwa Jeshi la Polisi haliwezi kuandaa na kusambaza taarifa kama hizo katika Mitandao yake ya kijamii.

Wakati tunaendelea kufuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo ili wakamatwe, tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na kuepuka kuendelea kuzisambaza endapo zitakufikia. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote yule aliyehusika na utengenezaji na utoaji wa tarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza.

Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

View attachment 3339663
Sawa,taatifa hazijatolewa na Tanpol.Je,ni taatifa za urongo?
 
Hivi polisi wanamshtaki Lissu kuwa alichapisha taarifa za kichochezi mtandaoni,je na wao washitakiwe kwa kuchapisha taarifa za kichochezi?
 
Back
Top Bottom