Polisi wamsaka Baba kwa tuhuma za mauaji ya mwanae

Polisi wamsaka Baba kwa tuhuma za mauaji ya mwanae

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mzazi anayefahamika kwa jina la Daniel Muga, Mnyaturu ambaye ni fundi ujenzi, mkazi wa Bombambili Ukonga Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa miaka mitatu kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Februari 28, 2022 saa 3:00 Usiku baada ya mzazi huyo kumpigia simu mke wake, Merry Joseph, Mnyamwezi ambaye walikuwa na mgogoro wa kifamilia na walikuwa wametengana kwa muda, huku muuwaji akidai alitaka aende alipokuwa ili ampe fedha za matumizi ya mtoto wao.

“Mama huyo akiwa na mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka mitatu alikubali wito huo nalipofika alibembelezwa ili warudiane lakini alikataa,” amesema Kamanda ACP Muliro.

Anaeleza kuwa wakati anaondoka ndipo alishambuliwa kwa kitu kizito kichwani yeye na mtoto wake hali iliyosababisha mtoto huyo kupoteza maisha na yeye kupata majeraha na kulazwa Hospitali ya Amana.

Kamande ACP Muliro amebainisha kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka.

Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa na kuwaomba wananchi wema kutoa taarifa kwenye kituo chochote cha Polisi au kwa mamlaka za kisheria zitakazowezesha mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.

0001.jpg
 
Kwani kuna ulazima wa kutaja makabila yao?
... pamoja na taarifa nyingine, ripoti ya polisi kuhusu uhalifu haijakamilika bila kutaja JINA, UMRI, KABILA, DINI, TUKIO, MAHALI na TAREHE YA TUKIO.

Sijajua mhalifu akiwa mmarekani au mrusi huwa wanataja kabila gani.
 
Sasa huyo mtoto alifanya kosa gani?! Tena mtoto wako kabisa?! Huu sasa ni utaahira uliopitiliza

Anyway, tubuni na mkamilishe bwawa la Nyerere kama redemption
 
Hayo ya jamaa na mkewe sitahukumu.

Ninachojiuliza mtoto amekosa nini?
 
Back
Top Bottom