Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kuna tatizo kubwa la weledi ndani ya Jeshi la Polisi.
POlisi wa nchi hii, bila shaka hawana weledi wa kutosha, na wala hawajishughulishi kujua sheria ili wafanye kazi zao kwa weledi. Lakini pia yawezekana wanajua sheria inataka nini ila kwa kiburi na kwa makusudi wanaamua kuikanyaga sheria kwa kuamini kuwa hakuna wa kuwawajibisha. Wengi wao ni kama wanaamini kuwa Polisi wana uwezo wa kufanya chochote bila ya kuzingatia katiba, sheria na kanuni. Ndiyo maana mara kadhaa tumeshuhudia Polisi wakifanya mambo ya ajabu yanayozuiwa na katiba na sheria za nchi, na hata kanuni za utendaji kazi za Jeshi la Polisi.
Mara kadhaa tumesikia kuwa eti jeshi la polisi limezuia mkutano wa chama cha siasa au limetoa kibali!! Ni mambo ya ajabu sana.
Kuhusiana na suala la mikutano ya vyama vya siasa, chama cha siasa kinachotaka kufanya mkutano, kinawajibika kuwapa taarifa Polisi. Chama hakiombi kibali, bali kinatakiwa kutoa tu taarifa ili kupatiwa ulinzi wa polisi. Kama kuna mazingira yoyote yale ambayo Polisi wanaona ni changamoto kwenye suala la usalama, mamlaka yao yanaishia kwenye kushauriana na chama husika juu ya namna bora ya kufanya ili kujihakilishia usalama. Polisi hawana mamlaka ya kufuta mkutano wa chama cha siasa. Chama husika kama baada ya kushauriana na polisi, kinaona ni aheri kuuahirisha mkutano huo, basi ndicho kitakachokuwa na mamlaka ya kuufuta mkutano kilichokuwa kimepanga kuufanya.
Kufuta shughuli zozote za kisiasa, kama kuna ulazima wa kufanya hivyo, kunaweza tu kufanywa na Rais kwa kutangaza hali ya hatari kwa kuzingatia sheria inasema ni mazingira gani Rais atalazimika kutangaza hali ya hatari.
Watanzania tuungane katika kuzifanya hizi taasisi za ulinzi na usalama, hasa Polisi, zifanye kazi kwa mujibu wa sheria, na siyo kwa matakwa ya mtu mmoja, ambaye yawezekana moyoni mwake akawa na dhamira chafu au akatumiwa na watu wenye dhamira chafu dhidi ya nchi.
Kila itakapotokea Polisi ametoa tangazo au kutenda jambo lolote lililo kinyume na katiba, sheria za nchi au kanuni, basi mara moja polisi huyo ashtakiwe kama yeye kwa kosa la kutumia madaraka vibaya (japo tunajua kuwa mahakama zetu nazo zinaiingiliwa).
OCD wa Ngorongoro afunguliwe mashtaka haraka sana kwa kuvunja sheria.