PreGE2025 Polisi wasema wamemkamata Golugwa kutokana na taarifa za siri kuwa anasafiri bila kufuata sheria!

PreGE2025 Polisi wasema wamemkamata Golugwa kutokana na taarifa za siri kuwa anasafiri bila kufuata sheria!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu,

Ila Polisi :BearLaugh: :BearLaugh: mpaka hata ni fezea kuanza kuwajibu! Hivi wanajiskiaje wakiandika huu upuuzi?

Uhamiaji wako wapi kufanya kazi yao? Na kipindi chote hiko walikuwa hawaoni kama anashida kwenye documents zake?

Asee Jeshi la Polisi sasa limekuwa kama tambara kwa wanasiasa, hii ni aibu sana! Tunaelekea wapi?

====

TAARIFA KWA UMMA
KUKAMATWA KWA NAIBU KATIBU MKUU TANZANIA BARA WA
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

​
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linatoa taarifa kwa Umma kuwa tarehe 13/05/2025 majira ya saa 06:45 usiku katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lango namba 03 (terminal 03) lilimkamata
Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels Nchini Ubelgiji.

Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata
taratibu za kisheria hapa Nchini.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama kuhusu suala hilo.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu mtajwa

Imetolewa na;
Kaimu Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam


View attachment 3332607

Pia soma Pre GE2025 - News Alert: - CHADEMA: Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa leo. Inadaiwa amepigwa sana
Na kwamba mienendo ya kutoka na kurudi nje ya nchi lazima upate kibali? Kwamba anaenda nje bila kufuata taratibu maalumu kwamba mtajwa huwa anatumia ungo kusafiri? Naomba mnieleweshe
 
Naliagiza jeshi la polisi likafanye upekuzi nyumbani kwake, inawezekana anafanya biashara ya madawa ya kulevya ndo maana anatoa na kurudi bila kufata sheria.
Wanasema haagi serikali anaposafiri madawa atakua anauza mama yako labda
 
Na wewe unadhani ni sahihi kumkamata mtu ambaye sio raia wa nchi yako? Si umuache aende zake kwao?
Aende wakati kajiunga kwenye siasa za ndani ya nchi na kuiyumbisha?

Raia wa nje anaruhusiwa kuwa katibu wa chama cha siasa nchini? Kama sio gaidi ni nini?
 
Police hawana sera wala point.
Wanazidi kuwapa Chadema Credit
 
Katika awamu ya tano ilinifanya niwaze sana na mawazo yangu yanabakia na maswali mengi mpaka leo.
Hivi ni kweli kuna watu wanapambana kupata uongozi wa kisiasa ili waikomboe nchi pamoja na watu wake katika kujenga ustawi? Maana naona kama vita hii ni ya manufaa binafsi ila kwa koti la kuwatetea wanyonge.
Na ukichunguza vizuri kuna watu walipata madaraka kwa njia safe lakini wakaamua kuhodhi nafasi zote kwa kuweka ndugu,jamaa na marafiki na kwa bahati mbaya hao jamaa,ndugu na marafiki wakabadilisha ajenda na wakakosa kukubalika sasa wakatafuta mbinu ya kung'ang'ania vyeo na madaraka yao hawa wamekuwa ruba huwezi kuwatoa kwa makelele na matusi maana wana mbinu nyingi ikiwemo ile ya wakoloni ya divide and rule.
Kama tumepewa uwezo na Mwenyezi Mungu wa kutambua mema na mabaya kunashida gani kuwatambua hawa wasio kuwa na nia njema na kuwakataa katika njia uliyobora zaidi ya hizi tunazozitumia? Tuwakatae kama ambavyo tunamkataa shetani na mambo yake?
Hata hao Polisi ambao ni kikwazo nao pia wamedhohofika kwenye mioyo kutokana na wale wachache walio hodhi mamlaka.Cha kufanya ni tukubaliane kupata watu sahihi na kutoa watu waovu ambao wanatumia uovu wao kuendeleza ukandamizaji wa kila aina ya haki.
Kama walikula nyama ya mtu hawezi kuacha kula nyama hiyo.
 
Back
Top Bottom