Na kwamba mienendo ya kutoka na kurudi nje ya nchi lazima upate kibali? Kwamba anaenda nje bila kufuata taratibu maalumu kwamba mtajwa huwa anatumia ungo kusafiri? Naomba mnielewesheWakuu,
Ila Polisimpaka hata ni fezea kuanza kuwajibu! Hivi wanajiskiaje wakiandika huu upuuzi?
Uhamiaji wako wapi kufanya kazi yao? Na kipindi chote hiko walikuwa hawaoni kama anashida kwenye documents zake?
Asee Jeshi la Polisi sasa limekuwa kama tambara kwa wanasiasa, hii ni aibu sana! Tunaelekea wapi?
====
TAARIFA KWA UMMAJeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linatoa taarifa kwa Umma kuwa tarehe 13/05/2025 majira ya saa 06:45 usiku katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lango namba 03 (terminal 03) lilimkamata
KUKAMATWA KWA NAIBU KATIBU MKUU TANZANIA BARA WA
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa katika maandalizi ya kusafiri kuelekea Brussels Nchini Ubelgiji.
Jeshi la Polisi lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata
taratibu za kisheria hapa Nchini.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linaendelea na uchunguzi wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama kuhusu suala hilo.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu mtajwa
Imetolewa na;
Kaimu Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam
View attachment 3332607
Pia soma Pre GE2025 - News Alert: - CHADEMA: Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa leo. Inadaiwa amepigwa sana
exactly, hili ndio lilikua lango sema limebumbuluka.Lengo ilikuwa na kumpoteza, bahati intelejensia ya CDM ikajua .....
ikabidi wabadili gia ngani
Sema umetoka na F hapo kama mimi tuu.Nasoma comments zenu tu
Wanasema haagi serikali anaposafiri madawa atakua anauza mama yako labdaNaliagiza jeshi la polisi likafanye upekuzi nyumbani kwake, inawezekana anafanya biashara ya madawa ya kulevya ndo maana anatoa na kurudi bila kufata sheria.
Aende wakati kajiunga kwenye siasa za ndani ya nchi na kuiyumbisha?Na wewe unadhani ni sahihi kumkamata mtu ambaye sio raia wa nchi yako? Si umuache aende zake kwao?
Siri ni neno pana subiri mashtakaEti anasafiri kwa siri, kwa hiyo walitaka awe ana waaga kila anaposafiri.
Nchi hii bila kutokea machafuko tutiane adabu hatuwezi kuheshimiana Kamwe..Airport hakuna uhamiaji? Uhamiaji wakibaini hayo huzuia mtu kupita au hukamata?
Wanajidhalilisha wenyewe.Aseee amna mtu wa kuzuia hilo jeshi letu 😅maana linazidi kudhalilika aseee
.... hayaaaaaaaa...... ..Imagine, guys huyu samia dawa yake iko jikoni, very soon atashangazwa na kitakachomkuta.
HAKIKANasema tena hawa viongozi wa Chadema wanatembea na tiketi zao mfukoni majuzi niliandika,,wewe pangu pakavu endelea tu no election no reform ,ukipelekwa front line.
Ndiyo polisi wamekuambia haya?Uwe na passport ya Tanzania
Sasa kama una passport ya nchi nyingine na unatumia kusafiria ina maana wewe sio raia wa Tanzania
Tanzania haijaruhusu uraia pacha
Ushahidi kuwa kapigwa uko wapi?Sasa ndiyo wampige sana kwani aliiba Tanzania katia kwenye begi anapeleka ulaya?