Polisi watatu wafungwa miaka 20 jela kwa Rushwa

Askari hawa walikuwa wakifanya mambo aliyokuwa anayependa Magufuli kipindi chake . ================================================= View attachment 2864210
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu Askari Polisi watatu wa zamani wa Jeshi hilo Mkoa wa Arusha ( Inspekta Hillary Ferdinand Komba, Bartholomeo Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta ) kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.

Kosa lao hilo la matumizi mabaya ya madaraka walilifanya tarehe 19 March 2021 walipokwenda nyumbani kwa Profesa Justin Maeda Wilayani Arumeru, Arusha na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu kisha kutumia nguvu na kumchukua Profesa huyo hadi kwenye Benki mbili pamoja duka lake moja la vifaa vya ujenzi walikomlazimisha atoe pesa ( anazodai ni milioni 100) na kuwapatia ili wasimfikishe kwenye vyombo vya sheria wakimtuhumu kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na ngozi ya chui.

Profesa Maeda kwenye mahojiano ya @AyoTV_ April 2021 alisema Askari hao walimtaka awape kiasi hicho cha pesa lasivyo atashtakiwa kwa uhujumu uchumi na walimtisha kuwa jela inamuhusu, kitisho ambacho kilimfanya awape pesa hiyo harakaharaka ili kuepuka kupelekwa mahabusu au jela akihofia hali yake mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati huo.

Japokuwa Profesa Maeda alidai kuwapa Askari hao milioni 100 kwa tuhuma hizo alizodai ni za uongo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ikitoa hukumu kwa Askari hao leo imesema kiwango cha pesa walichokichukua kwa Profesa huyo ni shilingi milioni 73.

Sakata hili la Askari hao watatu liligundulika kwenye Vyombo vya dola baada ya Profesa Maeda ( pichani kulia) kujitokeza na kufikisha malalamiko yake kwa Vyombo hivyo ikiwemo TAKUKURU na Jeshi la Polisi ambalo baada ya uchunguzi wake liliamua kuwafukuza kazi Askari hao mwezi mmoja baadae. #MillardAyoMAHAKAMANI
Sasa hapo Magufuli anahusikaje? Au una chuki yako binafsi naye?
 
Magufuli alifariki March 17, 2021, wakati hilo tukio limetokea March 21, 2021. Kumbe marehemu anaweza kuwatuma watu?!

Msiwe mnakurupuka kuanzisha thread bila kwanza kufanya uchunguzi wa kina, na wengine nao kushangilia kama kasuku bila kufanya uchunguzi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Chuki ni ugonjwa mbaya sana,umewatia vipofu watu wanao mchukia Magufuli, kila baya wao wanamsingizia Marehemu Magufuli! Mungu awasamehe bure tu!!
 
Mboba inaonekana uliyekurupuka ni wewe?

Usiwe unakimbilia ku-comment bila ya kusoma vizuri na kuelewa. Rudia tena kusoma mada, halafu urekebishe comment yako iliyolalia kwenye maelezo ya kutoielewa mada.

"Kosa lao hilo la matumizi mabaya ya madaraka walilifanya tarehe 19 March 2021 walipokwenda ....".

Tarehe 21 umeitoa wapi?

"Askari hawa walikuwa wakifanya mambo aliyokuwa anayependa Magufuli kipindi chake ."

Wapi mleta mada amesema hao askari walikuwa wametumwa na Magufuli? Tabia ikijengeka kipindi fulani, kwa uelewa wako, huwa inakufa ghafla?
 
Magufuli alifariki March 17, 2021, wakati hilo tukio limetokea March 21, 2021. Kumbe marehemu anaweza kuwatuma watu?!

Msiwe mnakurupuka kuanzisha thread bila kwanza kufanya uchunguzi wa kina, na wengine nao kushangilia kama kasuku bila kufanya uchunguzi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Yanatabia ya kuridhisha hisia zao kuliko Akili.
 
Magufuli amefariki tarehe 17 March 2021 kosa limefanyika Tarehe 19 March 2021 pia Taarifa inatoka KANDA iliyomchukia Hayati maana yake nini Chuki ni mbaya sana kikomaa hufakaranisha umoja wa kitaifa.Tuacheni chuki sisi sote ni Watanzania.
Mzee alikuwa jembe kweli kweli,ila alikuwa katili mno,na alipenda kuzungukwa na watu wenye tabia za kikatili kama makonda na sabaya,Mungu amweke popote atakapoona inafaa,Amen
 
Askari hawa walikuwa wakifanya mambo aliyokuwa anayependa Magufuli kipindi chake . ================================================= View attachment 2864210
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu Askari Polisi watatu wa zamani wa Jeshi hilo Mkoa wa Arusha ( Inspekta Hillary Ferdinand Komba, Bartholomeo Augustine Maya na PC Apornary Proches Burretta ) kifungo cha miaka 20 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.

Kosa lao hilo la matumizi mabaya ya madaraka walilifanya tarehe 19 March 2021 walipokwenda nyumbani kwa Profesa Justin Maeda Wilayani Arumeru, Arusha na kufanya upekuzi pasipo kufuata utaratibu kisha kutumia nguvu na kumchukua Profesa huyo hadi kwenye Benki mbili pamoja duka lake moja la vifaa vya ujenzi walikomlazimisha atoe pesa ( anazodai ni milioni 100) na kuwapatia ili wasimfikishe kwenye vyombo vya sheria wakimtuhumu kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na ngozi ya chui.

Profesa Maeda kwenye mahojiano ya @AyoTV_ April 2021 alisema Askari hao walimtaka awape kiasi hicho cha pesa lasivyo atashtakiwa kwa uhujumu uchumi na walimtisha kuwa jela inamuhusu, kitisho ambacho kilimfanya awape pesa hiyo harakaharaka ili kuepuka kupelekwa mahabusu au jela akihofia hali yake mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo wakati huo.

Japokuwa Profesa Maeda alidai kuwapa Askari hao milioni 100 kwa tuhuma hizo alizodai ni za uongo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ikitoa hukumu kwa Askari hao leo imesema kiwango cha pesa walichokichukua kwa Profesa huyo ni shilingi milioni 73.

Sakata hili la Askari hao watatu liligundulika kwenye Vyombo vya dola baada ya Profesa Maeda ( pichani kulia) kujitokeza na kufikisha malalamiko yake kwa Vyombo hivyo ikiwemo TAKUKURU na Jeshi la Polisi ambalo baada ya uchunguzi wake liliamua kuwafukuza kazi Askari hao mwezi mmoja baadae. #MillardAyoMAHAKAMANI

Kweli mnamkosea Magufuli wa watu, walimpelekea hizo hela? Sijawahi mpenda magufuli, ila hao wnafungwa kwa tamaa zao.
 
Mbona kiongozi wao mkuu eskariot sabaya wamemuachia?. Kweli wasiokuwa nacho hawana haki
 
Hao Vima kipindi cha Magu wamewabambikia sana kesi watu na kuwachukulia hela waliendelea wakidhani itabaki kuwa rahisi tu na kumbuka huyu Mzee kijana wake ndio alikomaa bila hivyo nae asingetoa taarifa maana Kijana wake aliapa kuwa haiwezekani Mzee wangu afanye kazi mpaka kustaafu kalitumikia Taifa vyema harafu wahuni tu wampe kesi za kijinga katika umri huu ntapambana nao kwa gharama yeyote ile ...
Kubambikiana kesi kupo toka hata Magu hajawa Rais, nakumbuka kipindi cha Jakaya,watu walikua wanawekewa viungo vya albino uwani kwao,alafu ghafla police eti wanakuja na wanataka kupekua nyumba,na walivyokua wajinga wakiingia ndani tu,wao hao moja kwa moja kwenye mtego wao waliotega na kuibua kizibiti, na hapo ndiyo sasa maongezi ya pesa yanaanza! Kuna police wengine Mungu atawaazibu vibaya sana kutokana na matendo yao!!
 
Sasa hizo hela zake mahakama inasemaje ? Itamke alipwe na serikalii au inakuwaje
Hela alishakula Sabaya na genge lake hapo maskini polisi waliambulia hata million moja moja labda na kuhaidiwa vyeo, ona leo kazi hawana na wake zao wanaenda kuchapwa mshededee na wanaume wengine kuwatoa genyee
 
Chuki ni ugonjwa mbaya sana,umewatia vipofu watu wanao mchukia Magufuli, kila baya wao wanamsingizia Marehemu Magufuli! Mungu awasamehe bure tu!!
Acha ujinga,mbona bwawa la umeme na sgr tunasema ni kazi ya magufuli hadi leo wakati yeye ameshakufa kitambo? Magufuli ndiye aliyeweka misingi ya ukatili uliokuwepo na unaoendelea hata sasa.
 
Back
Top Bottom