View attachment 3151999
View attachment 3151998
View attachment 3152001
MODS MSIUNGANISHE MADA HII NA NYINGINE ZENYE MAUDHUI TOFAUTI!
Utendaji ulioonekana hivi karibuni katika "kumteka" au kumtia nguvuni mwananchi anayeitwa Tarimo huko Kiluvya, unatia mashaka makubwa juu ya weledi kiutendaji wa sehemu za jeshi letu la Polisi.
Polisi ni chombo kinachotakiwa kujiendesha kisheria kwa kutumia PGO-Police General Orders.
Kumtia nguvuni raia yeyote kuna utaratibu ulioelezwa kisheria katika PGO.
Sasa kwa kituko kilichoonekana hivi karibuni kinaifedhesha jeshi la Polisi, na zaidi ya hapo kinamfrdhehesha sana Mkuu wa Polisi nchini IGP Camillius Wambura.
Polisi wanaooperate kama hooligans wa Haiti, hii haileti picha nzuri mbele ya wananchi.
Kulikuwa na ulazima gani kutumia style ya kwa kweli kihuni, kama polisi walioenda kumu arrest, na wanajua kwamba huyu ni mhalifu, kwenda na arrest warrant, tafuta viongozi wa mtaa kwa ushahidi, kumweleza huyo Tarimo makosa yake, na mwisho kumpandisha Defender?
Nahisi kuna maafisa chini wa IGP wanamtengenezea zengwe kumuaibisha IGP aonekane hafai kwenye cheo chake.
All in All, jeshi la Polisi kwa vitendo kama hivi halionyeshi proffessionalism kazini, bali wanonekana kama hoologans!