Tetesi: Polisi wazingira Keys Hotel Kwenye Mahafali ya CHASO Kilimanjaro

Kiukweli nimeshangazwa sana na muendelezo huu wa jeshi la polisi kuzuiya mahafali ya CHASO jana UDOM na leo jijini Moshi.
Kiukweli nikiwa kama mwana UVCCM tena mkereketwa sijafurahishwa na ukandamizaji huu wa hali ya juu unaofanywa na askari wetu, kwani kawaida hata sisi UVCCM huwa tunamafali yetu kila mwaka.

My take: Najua "mnapokea oda kutoka juu", lakini jaribuni kushirikisha na akili zenu,huku mkae mkikumbuka kuwa unapokula na kipofu siku zote, jitahidi usumshike mkono.

Leo mmezuiya mahafali yao, je na kesho mtazuiya na ya UVCCM??
 
Akili yako haina tofauti na ya kuku,(tena kuku aweza kuwa na afadhali)
Hayo makatazo ni maalum kwa vyama vya upinzani?
Tungemwelewe sana kama katazo hili lingelenga vyama vyote,LAKINI hii ya kuwaacha CCM wafanye wanavyotaka bila kuguswa na police,(mikutano ya kisiasa)halafu vyama vingine vinanyanyaswa kwa makusudi,NI KUPANDA CHUKI KUU MIONGONI MWA WANANCHI,HATA WALIOKUWA WAMEANZA KUMUUNGA MKONO(NIKIWEMO MIMI)WATAMCHUKIA MARA KUMI ZAIDI YA AWALI!!!
 
mdogo wangu anataka kufanya kitchen party wiki ijayo,lakini kwa hali hii hakuna namna ngoja niende kuomba kibali kituo cha kati...........
 
Binafsi namuunga mkono Baba J kwa anayoyafanya ili 2020 tuchukue point zetu 3 asubuhi na mapema kama kumsukuma mlevi vile.

Go baba J,go
 
Mkuu hata hapa chuoni wamefika, wameingia chuoni Mwenge, wamezunguka ndani tunawaangalia tu maana wanafunzi wengi hawakuwepo, wamekaa kama dakika ishirini hivi wakaenda zao, Yaani nimeshindwa hata kuelewa tunakoelekea siko sasa.
Hatari sana
 
Kuna Mushker ndani ya nchi yetu. Hilo bango la CCM mbona waliotukana wamenyamaza?
 
Kweli nina hasira na chuki. Lakini hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho. Hivi huu woga ni wa nini?
 
Mkuu huyu mleta mada mmoja anaitwa Barbarosa ni zaidi ya mfitina, nafikiri si mtanzania kwao ni gisenyi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…