Tetesi: Polisi wazingira Keys Hotel Kwenye Mahafali ya CHASO Kilimanjaro

Tetesi: Polisi wazingira Keys Hotel Kwenye Mahafali ya CHASO Kilimanjaro

Kiukweli nimeshangazwa sana na muendelezo huu wa jeshi la polisi kuzuiya mahafali ya CHASO jana UDOM na leo jijini Moshi.
Kiukweli nikiwa kama mwana UVCCM tena mkereketwa sijafurahishwa na ukandamizaji huu wa hali ya juu unaofanywa na askari wetu, kwani kawaida hata sisi UVCCM huwa tunamafali yetu kila mwaka.

My take: Najua "mnapokea oda kutoka juu", lakini jaribuni kushirikisha na akili zenu,huku mkae mkikumbuka kuwa unapokula na kipofu siku zote, jitahidi usumshike mkono.

Leo mmezuiya mahafali yao, je na kesho mtazuiya na ya UVCCM??
 
Serikali ipige marufuku na kuweka kanuni ngumu kwa Vyuo husika kutokukubali matawi ya Siasa Vyuoni kuanzishwa na Wanachuo wasijihusishe na siasa kabisa na ikigundulika wafukuzwe chuo. Hii italeta discipline na watazingatia masomo tu. Police Hongereni na msiwachekee hao nia yao ni kuivuruga jamii kwa kuichonganisha na Serikali waliyoichagua wenyewe. VYAMA VYA SIASA ZINGATIENI MAKATAZO MBALIMBALI MNAYOPEWA NA POLICE
Akili yako haina tofauti na ya kuku,(tena kuku aweza kuwa na afadhali)
Hayo makatazo ni maalum kwa vyama vya upinzani?
Tungemwelewe sana kama katazo hili lingelenga vyama vyote,LAKINI hii ya kuwaacha CCM wafanye wanavyotaka bila kuguswa na police,(mikutano ya kisiasa)halafu vyama vingine vinanyanyaswa kwa makusudi,NI KUPANDA CHUKI KUU MIONGONI MWA WANANCHI,HATA WALIOKUWA WAMEANZA KUMUUNGA MKONO(NIKIWEMO MIMI)WATAMCHUKIA MARA KUMI ZAIDI YA AWALI!!!
 
mdogo wangu anataka kufanya kitchen party wiki ijayo,lakini kwa hali hii hakuna namna ngoja niende kuomba kibali kituo cha kati...........
 
Binafsi namuunga mkono Baba J kwa anayoyafanya ili 2020 tuchukue point zetu 3 asubuhi na mapema kama kumsukuma mlevi vile.

Go baba J,go
 
Mkuu hata hapa chuoni wamefika, wameingia chuoni Mwenge, wamezunguka ndani tunawaangalia tu maana wanafunzi wengi hawakuwepo, wamekaa kama dakika ishirini hivi wakaenda zao, Yaani nimeshindwa hata kuelewa tunakoelekea siko sasa.
Hatari sana
 
Kuna Mushker ndani ya nchi yetu. Hilo bango la CCM mbona waliotukana wamenyamaza?
 
Kweli nina hasira na chuki. Lakini hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho. Hivi huu woga ni wa nini?
 
Naona kwa mbaaali ukweli wa maneno haya.... Tazama ziara za kwanza, Rwanda na Uganda.. Utapata maono ya hatari tuliyonayo... Hebu tujiulize...., kwani marehemu Mch Mtikila alikuwa mjinga kusema pia Mkapa nae si wa hapa....? [emoji32]
Watanzania wasomi tutafakari sana wapi nchi yetu inapelekwa...
Mkuu huyu mleta mada mmoja anaitwa Barbarosa ni zaidi ya mfitina, nafikiri si mtanzania kwao ni gisenyi
 
Back
Top Bottom