Kama serikali ya mtaa inatoa barua za udhamini kwa vibaka na panya pindi wakikamatwa police, wewe ufanye nini,na huko police usipofatilia mwizi wako,mwizi anatoa rushwa anatoka.panya rodi si ndugu zako na jamaa zako, Sasa wewe kwa nini umeshindwa kuwakanya waache tabia za kihalifu au kuwaripoti Serikali za mitaa?
Mkuu kwanza ni aibu sana kuwapa wananchi jukumu la kujilinda bila silaha wala mafunzo, wakati vyombo vya usalama vipo!!! Mbona kukiwa na maandamano wananchi hawaambiwa wakabiliane na waandamanaji?Mkuu kuna vitu vya kipumbavu sana tunavilea tu tukisema tunaonekana ni watu wa kulalamika tu police kazi yao nini ikiwa tatizo limewashinda si kuna jkt na jwtz mbona tunaongezeana gharama za maisha tu
Ushauri mzuri sana huu...pia unaweza kuongezea hivi. Akipatikana mzazi analea kijana muhalifu huku akijua basi mzazi na mtoto ni wahalifu,hapo kila mzazi angetoa taarifa ya vijana wao wakorofiKuna wakat binadam inabid umdispose kama amegeuka vampire vile ili kunusuru wengine! Kwa nia njema orodha ikipatkana mana wanajulikana wapunguzwe kabla, wakat na baada ya tukio.
Polisi iboreshe kitengo cha intelijensia ikibid kuwepo mfumo rahis wa kila raia kutoa alert na ikibid kuwepo informers wa kiraia wanaolipwa kwa siri kuleta taarifa nyeti. Nashaur kila ofis ya kata iwe na mgambo na silaha hata moja kubwa!
Hawa panya road wanaiba na kuharib kwa dharau sana. muda mrefu bila hofu tena mchana pengine! Kama kwenye lawless country uani!
Pia kamati ya ulinzi na usalama YA KIJIJI iongezewe maarifa kujua kila raia wake na maisha yake! Jukum la usalama wa kila mtu huanza na mwenyewe!
Tukubari tu nchi yetu haina uwezo kuwajaza polis kila point nchini. Wananchi tuwe na ushirikiano. Hasa wa taarifa.
Mtu anakunywa bia 6 kila siku na kuhonga juu lakin anaona tabu kulipa sh 2000 kwa mwez vijana wanaojitolea walinde mtaa!
Waafrica sijui kuna evolution hatujafikia!
....plan ya muda mrefu ni serkali kutimiza wajibu wake wa kutengeneza miundombinu ya vijana kupata ajira. Wana dhamana hiyo. Hawa vijana ni nguvu kaz inayohitaj kuidivert kwenye utendaji chanya.
Wananchi wenyewe hawana uchungu na maisha yao, la sivyo wangeshakinukisha na kuwavurumusha hawa watawala waovu kwenye madaraka waliyojitwalia kwa kupora kura. Bila kufanya hivyo hata siku moja hawakuwa na uchungu na wananchi. Na mabaya zaidi wanawaletea hata vimada wao ndiyo wawe ma-DC japo abc za uongozi hawajui. Kazi yao kubwa ni kuuza sura kwenye mitandao. Ingekuwa watawala wamesikia kuna maandamano ya wapinzani ungesikia wanasema ''tunao polisi wa kutosha na atakayeandamana atakiona cha moto''.Kwani unafikiri nchi yetu huwa inajali
Hao wenyewe wanaangalia wamekula wameshiba ndio huongea huo upupu
Inshort hawana uchungu na wananchi hata kidogo hatuna viongozi tuna wahuni na wapigaji wakubwa
Huwa nawazaga yaani hawajamaa kwanini paka saivi wako hai si wangekufaga tu huko sio kula pesa za watu na kuleta ujinga wao
Hajui wamekufa wangapi ,wamejeruhiw wangapi wanaropoka tu
Una akili kama za watawala. Unajaribu ku-solve complex problem kwa kutoa jibu jepesi kabisa. Huna tofauti na yule mtawala wa Ufaransa aliyesema ''let them eat cake''.Panya Road ni matokeo ya jamii inayoendekeza ujinga.
Wazazi ndio wanachangia Jambo hili Kwa 90%. Wap ndio wanawafuga na ndio waliowazaa.
Mbona huko Mikocheni, Masaki, OSTERBAY hakuna panya Road?
Mkuu huyo jamaa asikubabaishe. Ukichukulia tatizo kwa wepesi bila kutafakari unaweza kuona amesema kweli na suluhisho lake ni ''wazazi kuwafundisha watoto wao''. Lakini tatizo linakwenda mbali zaidi na kwa kutafakari utaona hili ni tatizo la uongozi wa nchi ulioshindwa kutimiza malengo yake.Sawa ni kweli, suluhu ni nini?
Polisi hawatoshi kulinda kila eneo, lazima mitaa husika ijipange kulinda usalama wao.Nichangie mara mbili polisi na Sungungu?,basi polisi waache kazi tuajiri hao sungusungu
Kuheruhi nusu ya kuua
Afu ukute yeye mwenyewe ana mtoto mwenye tabia nzuri akiwa nyumbani,akiwa shuleni na maeneo mengine ana tabia nyingine 🤣Mkuu huyo jamaa asikubabaishe. Ukichukulia tatizo kwa wepesi bila kutafakari unaweza kuona amesema kweli na suluhisho lake ni ''wazazi kuwafundisha watoto wao''. Lakini tatizo linakwenda mbali zaidi na kwa kutafakari utaona hili ni tatizo la uongozi wa nchi ulioshindwa kutimiza malengo yake.
Polisi na mgambo na kuna wale waliopewa kazi ya kuondoa wamachinga majukumu yao ni nini?Hapana kazi ni lazima, ukichangia watalipwa hao vijana wa ulinzi shirikishi watakao kuwa wanalinda