Polisi wenye silaha na mafunzo wameshindwa na Panya Road. Je, mwananchi ataweza?

Polisi wenye silaha na mafunzo wameshindwa na Panya Road. Je, mwananchi ataweza?

Je, vikundi vya ulinzi vina mafunzo ya kukabiliana na wahalifu wanaotumia siraha za moto?
Wanaweza kuwapa 'radio call' za kuwasiliana na polisi wanapoona wahalifu wamejihami zaidi .

Au muwape namba za simu za wakuu wa vituo wawasaidie wanapoona wahalifu wamejihami zaidi.
 
Sawa ni kweli, suluhu ni nini?

Suluhu hapo ni kuwaacha wafanye uhalifu Kwa kitambo kidogo mpaka walete madhara Kwa jamii Yao hiyohiyo iliyowalea, ili wajifunze kuwa mchelea mwana kulia hulia Yeye.

Maana usitake kuniambia Wahuni wa mbagala wanaweza kwenda kufanya uhuni Sinza hiyo haipo, watafanya hapohapo Mbagala Kwa sababu ya wakazi wa eneo hilo kuwaendekeza.

Wakishaleta madhara ndio napendekeza serikali iingilie Kati. Hivyo tuu!
 
Wanaweza kuwapa 'radio call' za kuwasiliana na polisi wanapoona wahalifu wamejihami zaidi .

Au muwape namba za simu za wakuu wa vituo wawasaidie wanapoona wahalifu wamejihami zaidi.
Unadhani wahalifu wanaweza kuendelea kufanya uhalifu eneo husika mpaka polisi wafike kutoa msaada? Pia kumbuka hawa wanatembea kikundi huwezi kumkuta mmoja au wawili au watatu au wanne ni kuanzia saba na kuendelea, ni wananchi wachache sana wenye uwezo wa kukabiliana na kikundi cha wahalifu wanaotumia siraha

Binafsi wakiweka au kupunguza masharti ya kumiliki siraha ya moto mimi naweza kujilinda mwenyewe
 
Suluhu hapo ni kuwaacha wafanye uhalifu Kwa kitambo kidogo mpaka walete madhara Kwa jamii Yao hiyohiyo iliyowalea, ili wajifunze kuwa mchelea mwana kulia hulia Yeye.

Maana usitake kuniambia Wahuni wa mbagala wanaweza kwenda kufanya uhuni Sinza hiyo haipo, watafanya hapohapo Mbagala Kwa sababu ya wakazi wa eneo hilo kuwaendekeza.

Wakishaleta madhara ndio napendekeza serikali iingilie Kati. Hivyo tuu!
Asante
 
Wamachinga waliondolewa ili watalii wakija wapate pa kupita badala yake watalii wakija watakutana na watakaowapora pochi zao.
 
Huwaga Mimi nazungumzia mzizi WA tatizo,
HAO panya road ni matokeo ya Baadhi ya wazazi kushindwa kuwalea watoto wao, huo ndio ukweli.

Serikali inaweza kushika nafasi ya pili Kwa lawama.

Hivyo wakwanza kupokea lawama hapo ni wazazi wa HAO Vijana wapuuzi
Unazidi kukoroga. Ungekuwa unazungumzia mzizi wa tatizo kweli kweli ni lazima ungeona tatizo ni serikali imeshindwa kukidhi malengo ya uongozi. Nenda nchi zilizoendelea. Kiwango cha uhalifu wa namna hii kiko chini sana. Kwa nini? serikali zinakidhi malengo ya wananchi na siyo kwamba wazazi wa watoto huko wanajua zaidi kulea. Hata huko Oysterbay ulikosema siyo kweli kwamba wazazi wanajua zaidi kulea watoto bali ni uwezo wa wazazi kukidhi malengo ya watoto wao. Huko ''uswazi'' maisha yako rough kwa sababu ya kipato. Mtoto wa Masaki akimaliza darasa la saba anapelekwa shule, uswazi wazazi hawana namna, watoto wanalundika mitaani bila ajira wala kipato huku njaa inawaadhibu. Wataacha kuwa panya road? Hawana cha kupoteza.
 
Suluhu hapo ni kuwaacha wafanye uhalifu Kwa kitambo kidogo mpaka walete madhara Kwa jamii Yao hiyohiyo iliyowalea, ili wajifunze kuwa mchelea mwana kulia hulia Yeye.

Maana usitake kuniambia Wahuni wa mbagala wanaweza kwenda kufanya uhuni Sinza hiyo haipo, watafanya hapohapo Mbagala Kwa sababu ya wakazi wa eneo hilo kuwaendekeza.

Wakishaleta madhara ndio napendekeza serikali iingilie Kati. Hivyo tuu!
Jamaa wewe mbona hutaki kuangalia mambo kwa kina? Hali ikindelea namna hii hatw wewe uliyeko Masaki au Oysterbay huko salama. Kiujumla ni kuwa nchi yetu haiko salama. Kilöa mwaka vijana wanapomaliza shule watawala wanasema ''haya vijana kajiajirini'' huku wao na watoto wao hawajawahi kuonyesha mfano wa kujiajiri hata siku moja. Hakuna plan yoyote ya miaka mitano au kumi ijayo, wao wanadhani bodaboda na umachinga ndiyo suluhisho. Ni suala la muda tu hata wewe unaandika kejeli kama hizi utajuta na kujiuliza tumefikaje hapa. Hutakuwa salama hata kidogo. Pia polisi na jeshi hawatakuwa na uwezo wa kufanya chochote.
 
Ushauri mzuri sana huu...pia unaweza kuongezea hivi. Akipatikana mzazi analea kijana muhalifu huku akijua basi mzazi na mtoto ni wahalifu,hapo kila mzazi angetoa taarifa ya vijana wao wakorofi
Aliyeondolea nguvu jamii kulea watoto kwa ushirikiano kasababisha ongezeko la kila uharibifu na uhalifu.
Enzi zetu una misbehave huko unalambwa mboko za kukupanga, na ukirud home mzaz akajua unaongezewa. Leo hii ukimkanya mtoto wa mtu unapokea bonge la tusi. Ukijichanganya na mzaz anaibuka kukusweka ndan! Hadi walimu inawakuta, walezi wetu tegemezi!
Sion wazaz wanaoleta watoto watukutu polis wala kwa mtendaj.
Mbaya zaid kuna mizaz nayo haikubari nafas zao kiumri inashirikiana na watoto uhuni, wizi, uzinzi, pombe hadi madawa ya kulevya. Lizee halitak hata shikamoo ya binti mdogo liko busy timing!
Kibaya zaid mlezi muhim sana, yan mwalimu shulen, anapogeuka PREDATOR!
Umaskin nao unawaondolea misimamo.
Hakuna social responsibility.
Hizi sera na sheria nyingine kupitia mwavuli wa haki za binadam tuzipe kanuni za kiuafrica. Inawezekana tunaua jamii yetu baada ya muda flan. Sijawai kuwaamin wazungu!
Mf ni sheria ya mwl kutompiga kiboko mwanafunz bila mbinu halis za detterence
 
Panya Road ni matokeo ya jamii inayoendekeza ujinga.
Wazazi ndio wanachangia Jambo hili Kwa 90%. Wap ndio wanawafuga na ndio waliowazaa.

Mbona huko Mikocheni, Masaki, OSTERBAY hakuna panya Road?
Ukiwalaumu wazazi sidhani kama uko sawa. Watoto wengine wametoka mikoani wakiwa wadogo wakaja Jijini kutafta maisha Ramani zimekataa mtu anaamua kujiingiza kwenye hizo shughuri.
 
Aibu kwa polisi wapo kimya kisa raisi yupo kimya mbona awamu iliyopita likitokea tukio mtaani hadi doria zilikuwepo kisa huyu mama mpole kama mtoto wa twiga ndio mfumbie macho.
 
Simoni Siro je Polisi imekosa kabisa mbinu ya kudhibiti panya road na wahalifu wengine? Kama polisi imeshindwa hawa vijana wachache wasiokuwa na mafunzo vipi ishu ya ugaidi wataweza kweli?

DC TMK Joketi anataka wananchi waunde vikundi vya ulinzi shirikishi,sa kazi ya polisi ni nini? Kama wameshindwa basi agawe na silaha wananchi wajilinde.

Kuna hoja kuwa polisi hawatoshi kulinda mitaa yote,sa kama serikali imechukua hatua gani kama polisi hawatoshi? Wakati kuna migambo? Yani polisi walale nyumbani na mwisho wa mwezi apokee mshahara huku mlipa kodi akifanya kazi mchana na usiku akalinde?

Hili swala binafsi haliingii akilini sababu ndani ya miaka 6 ya Magufuli hatujawahi kusikia hivi vikundi vya kijinga. Kama Siro umeshindwa kazi jiuzulu tu.
Najiuliza maswali mengi sana lakini sipati jibu. Ni kwa nini wakati wa mwenda zake hawa panya road walipotea na kwa uongozi huu wa bi tozo wameongezeka sana?
 
Panya Road ni matokeo ya jamii inayoendekeza ujinga.
Wazazi ndio wanachangia Jambo hili Kwa 90%. Wap ndio wanawafuga na ndio waliowazaa.

Mbona huko Mikocheni, Masaki, OSTERBAY hakuna panya Road?
Sasa wao wanatafutiwa mahitaji na wazazi wao na huko waishi kama watoto wa bata kila mmoja analitafutia tumbo lake.
 
Afazali ww umejibu kwa ushahid ulio uchi uchi, penhine jamaa alikuwa bado haja jiunga na JF au
Lakini wananchi wakipindi hicho angalau walitoa kipigo kwa baadhi yao lakini wasasa hawakumkamata hata mmoja!
 
Ukiwalaumu wazazi sidhani kama uko sawa. Watoto wengine wametoka mikoani wakiwa wadogo wakaja Jijini kutafta maisha Ramani zimekataa mtu anaamua kujiingiza kwenye hizo shughuri.

Waliowaowapokea wanawajibu wa kukinywea kikombe.

Mimi huwaga napenda mtu madhara ayapate ndio apewe msaada.
Yaani mtoto akililia wembe unampa alafu ukimkata ndio unamnyang'anya, hii inamsaidia kuelewa zaidi.
Kuliko maneno matupu
 
Jamaa wewe mbona hutaki kuangalia mambo kwa kina? Hali ikindelea namna hii hatw wewe uliyeko Masaki au Oysterbay huko salama. Kiujumla ni kuwa nchi yetu haiko salama. Kilöa mwaka vijana wanapomaliza shule watawala wanasema ''haya vijana kajiajirini'' huku wao na watoto wao hawajawahi kuonyesha mfano wa kujiajiri hata siku moja. Hakuna plan yoyote ya miaka mitano au kumi ijayo, wao wanadhani bodaboda na umachinga ndiyo suluhisho. Ni suala la muda tu hata wewe unaandika kejeli kama hizi utajuta na kujiuliza tumefikaje hapa. Hutakuwa salama hata kidogo. Pia polisi na jeshi hawatakuwa na uwezo wa kufanya chochote.

Nchi haipo salama Kwa wasiotaka Usalama Mkuu.

Huwezi kuta matukio yakatokea Huko OSTERBAY, sijui Masaki, Mikocheni ukasikia watu wakilalamika, hapo ni Shaba tuu wakazike toto Lao.

Hata south Africa Yale matukio ya Xenophobia hayakutukia Maeneo ya kishua, wanajua moto wake.

Uhalifu siku zote hutokea Maeneo ya watu wasiopenda usalama. Hilo lazima ukae ukilijua.
 
Wanasema kila mtoto ana riziki yake, tusizae tena!

😀😀

Yaani ni Bora Kafiri kuliko mtu asiyeweza Kuwatunza watu wake, familia yake.

1 Timotheo 5:8
Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
 
Back
Top Bottom