Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Usiwaamini sana wanaposema tunaomba ushirikiano wako maana unaweza kujikuta matata ni bila kutegemeaNdugu zangu salam
Kutokea tukio la binti kufanyiwa ukatili wa kingono na njemba zaidi ya wanne kumekua na makatazo mbali mbali na amri za kutisha zakutokuisambaza video iliyorekodiwa ikionyesha wahusika waliotekeleza unyama huo.
Vyombo mbali mbali vimeomba na kuombwa ushikikiano ili watu hao watiwe nguvuni .
Swali ni kwamba
1: Huku uraiani sisi wengine tunaoishi na ndugu jamaa na marafiki zaoau walikua marafiki zetu, tutajuaje wahusika ni hawa ili tuwachomeshe wakamatwe kama kuna katazo la kuendelea kuisamba hiyo video limetolewa?
2: Majeshi mengine na taasisi zingine za kiupelelezi zitajuaje kama wahusika ndo hawa ili baadhi ya askari watakao kutana nao katika mizunguko ya kimaisha wawatie nguvuni?
3: Tunajua walikua wanaenda kwenye nyumba za ibada, sehemu za huduma za kijamii, na kwenye mikusanyiko mbali mbali au sehemu za starehe, je, kama wametoa katazo ni vipi sisi raia / askari ambao hatujaona sura za wahusika tunaweza vipi kushirikiana kutoa taarifa au kuwatia nguvuni kuwa wa husika ni hawa ili hali kunakatazo limetolewa la kutokuendelea kusambaza ile video ya unyama uliofanyika?