Kuwa RC sio kipimo cha akili/elimu wala upeo na sio sifa ya kunifananisha nayo.
Umenishangaza kwa kusema SA ina huduma bora za kijamii ukiilinganisha na Libya ya Gadaffi. Pia nimeendelea kusikitika kwa kusema Mandela hafananishwi na mtu yoyote duniani (refer to your foregoing posts) kisa busara,kupokea wakimbizi wa Somali na kusuluhisha migogoro kana kwamba Mandela ndio kiongozi wa kwanza kupokea wakimbizi, kusuluhisha migogoro na kupokea wakimbizi.
Kwa msaada tu wa taarifa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopokea sana wakimbizi hasa kutoka Congo, Burundi na Rwanda.Pia Nyerere ,Mkapa na Kikwete wamehusika sana kwenye usuluhishi wa migogoro.Kikwete kwa sasa anasuluhisha Libya na Mkapa Burundi. Haya yote ni mambo ya kawaida sana kidiplomasia.
Tunapowazungumzia Gaddafi na Mandela tunataka mtu uoneshe unique characters na mchango kwa Africa na waafrika na si kutuletea mambo ambayo ni so obvious kila mtu anaweza kufanya. Kwa mfano Nyerere kutumia resources za watanzania kwa ukombozi wa Africa, Gaddafi kutumia resources za walibya kwa waafrika na sio kutuletea habari za hekima ,busara na kupokea wakimbizi , vitu ambavyo kila nchi inafanya.