Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?

  • Total voters
    244
Utafiti umeufanya zaidi ya WALIBYA wenyewe waliomuua? Wewe una uchungu zaidi ya Walibya walioitwaa panya na kuwaua kabla ya majeshi ya kigeni kuingilia kati?????? Maandamano ya kumtoa Ghadafi yalifanywa na Walibya man.Wewe mTanzania umebaki kupayuka tu.
Kwa akili kama hizi Africa itaendelea kutawaliwa milele. Hivi ni nani aliyewaroga waafrika??

Walibya ni miongoni mwa raia wa dunia hii waliopata huduma za kijamii daraja la kwanza.

Ukweli usiopingika ni kuwa kila binadamu ana mapungufu yake, westerners ambao kwa kiwango kikubwa hawakupenda misimamo ya Gaddafi ndio walimuua Gaddafi kwa kusaidiwa na walibya wachache waliopandikizwa chuki na westerners kupitia mapungufu ya Gaddafi kama binaadamu.

Kwa hali yoyote ile unapopima uadilifu au ubora wa binadamu hatutegemei kupata 100% positive lazima kuwe na mapungufu ndivyo ilivyokuwa pia kwa Gaddafi.

Vita nyingi zinazoongozwa na wamarekani ukichunguza kwa jicho la tatu ni kwa maslahi yao na si ya watu wanaodai inawapigania. Hili utalielewa kama akili yako umeiweka huru kupokea positive thoughts tu.
 
Huo mpambano si sawa. Gaddafi ni gaidi muuaji muingo aliyeua mpaka maafisa wa jeshi lake mwenyewe na kubaka wake zao. Alikuea na harem alilofanyia uchafu huku akinywa Johnnie Walker na kujidunga madawa ya kulevya.

Mapungufu yoyote ya Mandela yakipimwa na Gaddafi Mandela ataonekana mtakatifu.

Mandela mtafutie mtu mwingine wa kumpamnanisha naye. Labda Nyerere.

Si Gaddafi.
Mtu aliyefanya ukombozi kwa nchi nyingi hata huyo Mandela kipindi anaitwa gaidi na CIA na yupo kwenye watchlist ya CIA Gadaffi ndiye aliyekuwa anatoa financial support kwake yeye

Na kwenye liberation ya African Gadaffi ndiye pinnacle akishirikiana na akina Castro

Mandela sifa yake kubwa ni kufungwa jela tu
 
Ghadaffi alitoa msaada kwa nchi zipi? Waweza fafanua?
 
Kwa akili kama hizi Africa itaendelea kutawaliwa milele. Hivi ni nani aliyewaroga waafrika??

Walibya ni miongoni mwa raia wa dunia hii waliopata huduma za kijamii daraja la kwanza.

Ukweli usiopingika ni kuwa kila binadamu ana mapungufu yake, westerners ambao kwa kiwango kikubwa hawakupenda misimamo ya Gaddafi ndio walimuua Gaddafi kwa kusaidiwa na walibya wachache waliopandikizwa chuki na westerners kupitia mapungufu ya Gaddafi kama binaadamu.

Kwa hali yoyote ile unapopima uadilifu au ubora wa binadamu hatutegemei kupata 100% positive lazima kuwe na mapungufu ndivyo ilivyokuwa pia kwa Gaddafi.

Vita nyingi zinazoongozwa na wamarekani ukichunguza kwa jicho la tatu ni kwa maslahi yao na si ya watu wanaodai inawapigania. Hili utalielewa kama akili yako umeiweka huru kupokea positive thoughts tu.
Unaowatetea hawakuuona huo utakatifu wa Ghadafi.Acha kusingizia USA
 
Mtu aliyefanya ukombozi kwa nchi nyingi hata huyo Mandela kipindi anaitwa gaidi na CIA na yupo kwenye watchlist ya CIA Gadaffi ndiye aliyekuwa anatoa financial support kwake yeye

Na kwenye liberation ya African Gadaffi ndiye pinnacle akishirikiana na akina Castro

Mandela sifa yake kubwa ni kufungwa jela tu
Watoto ambao hawajui historia ya Mandela kabla ya kufungwa jela ndio wanasema Mandela sifa yake kubwa kufungwa jela.

Nenda kasome nani kaanzisha "Umkontho we Sizwe". Nenda kasome Rivonia Trials za 1963 -64. Kasome Mandela alivyoranda kijasusi Africa nzima kupanga mipango ya ukombozi.

Gaddafi mshenzi tu kamsaidia mpaka Idi Amin katika vita vya Kagera Mtanzania anayemsifia Gaddafi hajielewi.
 
Ghadaffi alitoa msaada kwa nchi zipi? Waweza fafanua?
Wakati Mandela kafungwa jela Gadaffi alikuwa anamwaga hela kwenye chama cha ANC akikisaidia kwenye kampeni dhidi ya apartheid millions of dollars, south Sudan gadaffi ndiye aliyekuwa anawafadhili akina Garang na aliplay part kubwa mpaka inapata Uhuru.. Nimezitolea mfano nchi hizi mbili ila nchi kibao mpaka za south America ,Black movement wa USA nk
 
... Vyombo ya mangaribi hasa media na viongoz wao wanampamba sana madiba kwa sababu hakugusa maslahi ya wazungu.
Mkuu acha tukupe elimu kama unataka kuelimika. Madiba hakuwa rafiki wa wazungu hata siku moja. Ulaya na USA yote ilikuwa pamoja na makaburu. Madiba kaondolewa ktk list ya magaidi ya USA wakati wa Obama au Bush. Sasa unapata wapi habar kuwa vyombo vya 'mangaribi' vinampamba madiba?
 
Gadaffi alikuwa pamoja na waafrika ili aweze kuwapelekesha kwa pesa zake za mafuta. Alitaka iundwe United States of Africa ili aiongoze, sawa sawa na Mseveni aliyeitaka political federation ya EAC ili awe rais wa EAC. Tujiulize Gadaffi kapigania lipi kwa maslahi ya kiafrika?

Nyerere alimuomba fedha kwa ajili ya foundation yake, yeye akaahidi kujenga msikiti kana kwamba Mwalimu Nyerere Foundation inajenga misikiti. Alikuwa amesahau kabisa kuwa alirudishiwa viaskari vyake vilivyokuwa vinatetemeka kwa baridi ya Mbeya vilivyotekwa kwenye vita ya Uganda bila kudai fidia yoyote. Mwanaafrika hawezi kutuma majeshi yake kwenda kupigana na waafrika wenzake. Hakutuma majeshi wakati wa harakati za ukombozi anakuja kutuma majeshi Uganda kisa Idd Amini mwislam mwenzake, halafu mnataka kumtaja kama hilo wa Africa!?

Leo tumepewa kazi ya kulinganisha kati ya samaki na konokono, yupi anajua kuogelea zaidi.
 
Vita ya Uganda watu wengi hawataki kujisomea, wanataka wasimuliwe vijiweni na watu wanaomchukia mwalimu. Facts:
  1. Mgogoro kati ya Nyerere na Iddi Amini haukuanza 1978, bali miaka ya mwanzon mwa 1970. Nyerere angekuwa mpenda vita angepambana na Iddi Amini kabla hajajiimalisha ili amuweke 'rafiki yake Obote'.
  2. Baada ya vita, Nyerere hakumpa madaraka Obote, bali Yusuf Lule. Dhana kwamba alienda vitani kwa ajili ya Obote inatoka wapi?
  3. Nyerere hakuanzisha vita. Iddi Amini ndo alikuwa wa kwanza kushambulia Tanzania. Akapiga Kagera na Mwanza. Bado Nyerere hakurukia vita au ku-retaliate. Aliomba nchi za OAU (sasa AU) zilaani kitendo kile. Hakuungwa mkono. Ina maana Nyerere aliitafuta Diplomasia, lakini hakupata muafaka.
  4. Iddi Amini hakupendwa na wananchi wake, kulikuwa na kikundi cha waasi kilichoongozwa na Mseveni na kilichopigana bega kwa bega na majeshi yetu. Hapa napinga dhana kuwa Idd Amini alikuwa mtu mwema aliyeonewa na Mwalimu.
Kwa uungwana, niseme kuwa Tanzania 'iliwahost' waasi wa Uganda waliokuwa wanaongozwa na Mseveni. Walikuwa wanafanya mashambulizi Uganda na kukimbilia Tanzania. Hii ndio sababu kubwa ya mgogoro kati ya Iddi Amin na Nyerere. Binafsi sishangai Nyerere kuwaruhusu 'waasi' kina Mseven na Besigye kufanya harakati zao kutoka Tanzania.

Idd Amin alikuwa ameleta mchezo mchafu wa mapinduzi Afrika Mashariki. Ikumbukwe jaribio la uasi la 1964 lilifanyika Uganda, Tanzania na Kenya pia. Hivyo utawala wa kijeshi wa Idd Amini ulikuwa lazima uchukiwe na Nyerere. Mpambana na mkoloni mweupe, hawezi kumuonea aibu mkoloni mweusi ambaye ni Idd Amin!
 
Back
Top Bottom