Akikulilia shida msaidie kama unaweza huwezi muache na shida zake sio kuhangaika kumsema hao waoaji wa maana hawajawekwa bango kwamba huyu ni wa maana na huyu sio wamaana
 
Akikulilia shida msaidie kama unaweza huwezi muache na shida zake sio kuhangaika kumsema hao waoaji wa maana hawajawekwa bango kwamba huyu ni wa maana na huyu sio wamaana
Hivi mkuu, binti anapowakataa vijana ambao hawajaoa na kujibanza kwa mume wa mtu anategemea atakuwa yeye ndio muke ya huyo jamaa?

Huwa nawaonea huruma wale waliofiwa na waume zao na ambao wanaume zao ndio chanzo Cha wao kuwa hivyo.

Waliobakwa ni bahati mbaya tu.
Hawa wanaotumia uchi Kama kitegauchumi aafu waje kuonewa huruma Ni ujinga. Waolewe wawe wake wenza huko.

Unazalishwa na mume wa mtu aafu unaanza kusumbua wachungaji wakuombee upate mume!!
Pumbaf
 
Kiukweli sio tabia nzuri kuwasema single maza lakini wakati mwingine inaweza kuokoa wasichana wenye mpango huo kwa kuona mtazamo wa jamii ukoje.

Hasa hasa wale waliozaa na waume za watu au wale wanaotegemea kujibebesha mimba ila mwanaume atangaze ndoa haraka.
 
sema nikimwonaga mwafrika anamsema vibaya single maza namshangaa sana kwasababu asilimia kubwa ya watoto wanalelewa na hao hao.Wazee wanakimbia majukumu.
Single mothers hawana tatizo kabisa. tatizo linakuja akishaolewa na mwanaume ambae hajazaa nae:

1. anaweza akaingia ndoani kwa interest za kumtafutia mtoto maisha bora, na upendo wake juu yako ukawa ni wa kuchovyachovya tu.

2. baba wa kambo hawezi kumuadhibu mtoto wa kambo, na akimuadhibu anaonekana kama mnyanyasaji.
na baba original wa mtoto akitaarifiwa mtoto wake anachapwa anaweza akachukua hatua kali dhidi ya baba wa kambo ingawa hata angekua yeye angeweza kumpiga mtoto wake na mtoto angemezea tu.

3. mtoto wa kambo kama ni mkubwa anaweza akaleta complications kwenye ndoa. na hapo mamaake lazima atasimama upande wake.

4. baba original wa mtoto anaweza akaiathiri ndoa ikaonekana chungu. Mawasiliano ya mara kwa mara, text za usiku na simu za hapa na pale zinaweza zikamuathiri kisaikolojia baba wa kambo.

5. kuonana mara kwa mara kwa baba original wa mtoto na mzazi mwenzake kunaweza kuamsha hisia za zamani na wakajikuta wanafanya uzinzi, kupelekea single mother kuisaliti ndoa.

sometimes kuoa single mother ni sawa na kwenda kuchota petroli iliomwagika. akitokea mvuta sigara tu HASTA LA VISTA.
 
Call it love and devotion
Call it a mom's adoration, foundation
A special bond of creation, hah
For all the single moms out there
Going through frustration
👌
 
Single mother 70% nizao la wanaume wazembe,wavivu,waoga,wanapenda sana NGONO lakini wanaogopa MAJUKUMU.

30% ni wao wenyewe wanawake wanajitakia.

Kwa kifupi tatizo la single mother linatokana na kizazi cha vijana wakiume wasiopenda kuwajibika,lakini ni mabingwa wa kufanya ngono.
 
Sauti imesikika vzuri nafikiriiii.wakihitaji tutaeka speaker
Bado hatujasikia. Kinachofanyika hapa ni kuhalalisha kitu ambacho si sahihi kuwa sahihi.

Single mother ambao hawapaswi kusemwa ni wajane na wale ambao ndoa zimevunjika/wametengana kwa sababu moja au nyingine. Ila danga kuwa single mother lazima tuwaseme tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…