Pongezi kwenu Single Mothers
Mwanao uyo aliyepatikana kwa zinaa akikua mwambie akaoe single maza sawa eh?
Sio kwamba wanaume wenye malengo nanyi hamuwaoni ila mnaamua tu kujifaragua shwain!! Mbili na nusu

Unalala na wanaume sita tofauti wote peku unategemea nani akubali kulea mimba ya utata?

Control your psycho matters
 
Wengine utakuta Mama zao ni Single Mother lakini ndio wanaongoza kwa kuwasema Single Mother kila kukicha, siyo vizuri kabisa Single Mother nao ni Binadamu kama walivyo Binadamu wengine.
Haijalishi single maza ni nani yako ... upuuzi ni upuuzi tu
 
Mi naona wanaume wana nafasi kubwa sana ya kufuta kama sio kupunguza kabisa hii kitu ya single mothers....

Mwanamke hata awe mzuri vipi usikubali kukutana naye bila kinga

Kama akipata mimba bila kutarajia na wewe mwanaume haupo tayari fanyeni mpango hiyo mimba itolewe ila wengi mtasema ni dhambi Mungu hapendi sijui ukristo mwingi as if wakati mnadinyana Mungu alikua anafurahia

Mwanaume kama binti huna mpango wa kumuoa usikubali akubebee mimba

Tungeshirikiana kulimaliza hili jambo wote badala ya kunyoosheana vidole. Hao single mothers mimba hawakuipata wenyewe jamani

Wakiwakubalia mkawapa mimba mkaawaacha mnawaita wahuni....mkikataliwa mnasema wanawake wanawaringa ngoja tuone nani atamuoa umri ukienda

Maneno mabaya ya wanaume kama haya ndio yanafanya wanawake wengi wanakua na low self esteem wanakua frustrated sababu yenu.


Mnaweza mkadhani mkiongea kitu humu jf ni utani ila maneno makali popote pale yana madhara makubwa sana hasa yakisemwa na watu wengi.

Wanaume punguzeni lawama kwa kweli na masimango kwa single mothers. Yangu ni hayo tu[emoji124]
 
Hii ni sawa na kutuambia mwizi asisemwe kwa tabia yake ya wizi, muongo vivyo hivyo,muuaji kadhalika kitu ambacho siyo sawa lazima wasemwe ili hii tabia ya kuzaa nje ya ndoa ambayo kwa jina moja inaitwa uzinzi iishe kabisa kwa hiyo usizuie watu kukemea maovu
Sasa mnapowasema msisahau kuwasema na hao wanaowazalisha tofauti na hapo unakuwa ni unafiki tu ndiyo maana tunasema kama hamuwezi kuwasema na wanaowazalisha basi hata single mothers nao msiwaseme
 
nasupport kuwasema hapa jukwaani ilikukemea huu ujinga wa kuasingle maza ..wewe mtu hajakuoa unazaanae watu wamaana wenye nia ya kuoa unawakataa alafu ukikimbiwa ukaachiwa mtoto unalialia.
NOTE: with exception ya wanaokimbiwa wakiwa ndani ya ndoa ambao ni asilimia chache sana au wanaofiwa na waume zao

Tunawaambia haya sio kwamba hatuwapendi bali ni ukweli tunaletewa mizigo nyumbani for instance mimi wadogo zangu wawili wakike ni single maza nnaona wanavyokiwa mzigo unategemea tutetee huu upuuzi
Hapo kwenye paragraph ya mwisho wahanga ni wengi sana.

Kuna demu mmoja tumekuwa nae kitaa kimoja, tangu akiwa mdogo alikuwaga anatamani sana kuzaa na mzungu, yaani yeye ndoto zake alikuwa anasema ni lazima aje kuolewa na mzungu au ikishindikana kuolewa basi hata kuzaa nae tu.

Alikuwa anatamani sana kuwa na biracial child, ukicheki simu yake unakuta amejaza picha za vitoto vizuri vizuri tu kama vile vya Mabeste.

Sasa baada ya kuona hakuna uwezekano wa kumpata mzungu ikabidi ajipachike kwa chalii mmoja wa kiarabu anauza spare parts za piki piki, akajibebesha na mimba kabisa ya yule mwarabu.

Baada ya mwarabu kupewa taarifa za ujauzito alichomwambia yule demu ambaye mimi ni kama dada yangu aende akaitoe ile mimba, akampa na hela kabisa ya kutolea mimba. Yule sister alivyo ambiwa hivyo alimtukana sana yule mwarabu akasema mimba hatoi kama ni kulea atalea mwenyewe na ukawa ndio mwisho wa mahusiano yao.

Baada ya sister kujifungua alimuita yule mwarabu amuone mtoto wake, mwarabu akamwambia hamtambui yule mtoto kama ni wake akampa na vitisho vingi sana.. Sister akakubali yaishe na hakumsumbua tena.

Imepita miaka minne sasa tangu hilo tukio litokee mwarabu alishaoa mwarabu mwenzie wala hana habari na mtoto aliyezaa na sister, na sister nae hana habari na mwarabu kabisa.

Anachojivunia tu sasa hivi huyo dada yangu ni kupata katoto kazuri. Ila ana shida kibao yeye na mwanae, last time nimeenda home nilivyoonana nae aliniomba nimsaidie 50k, nilipojaribu kumuuliza kuhusu baba wa mwanae kama anawajibika akanijibu "hebu naomba usinilize".

Na hawa ndio aina ya single mothers wa miaka ya leo hii, they're the victims of their own stupid mistakes.
 
Back
Top Bottom