Habari zangu ziwafikie wanaume wote waingwana wa hapa JF
Na zisiwafikie wote wasio waungwana.
Huwa nahuzunishwa sana na kusononeka sana ninapoona kila Mara mada zikiwa za kuwaponda wadada wanaolea watoto wenyewe.
Ikumbukwe ukiona mdada analea mtoto mwenyewe kwa kumhudumia kwenye dhiki na faraja
Kumsomesha, kumvika kumlisha...n.k
Dada huyu kwenye jamii anahitaji pongezi kubwa sana na si haya ninayoyasoma kila siku humu.
Nani asiyejua ulezi ulivyo mgumu?
Why huyu Dada hakumtupa huyu mtoto au kumtelekeza kituo cha basi au kuitoa mimba?
Yumkini mabinti wakiendelea kusoma haya ya JF kwa baadhi ya Wavulana wasiojitambua wengi wao sasa wakipata ujauzito badala ya kulea mimba na kuzaa watatoa au kuvinyonga vichanga vyao mbali huko na kurudi mtaani wakijifanya watakatifu.
Kwanza mtambue kwamba hakuna chini ya jua mdada au mwanamke anayetamani au kupenda kulea mtoto mwenyewe.
Ni tumaini la kila mdada alee mtoto ndani ya ndoa au walee na Baba wa mtoto.
Utafiti unaonyesha kuna baadhi ya wakaka au Wababa huonyesha mapenzi yote awali na mipango mingine kuendelea but katikati hukutana na Binti mwingine na kumuacha huyu wa mimba.
Anaenda kwa mwingine anampachika mimba anamwacha anaenda kwa mwingine mpaka atakapokinai
No wonder kuna wkt mkikua mnaambia yule na yule ni watoto wa Baba mama mbalimbali..( hapa sio tabia mbaya ya Dada Bali ya huyo Mkaka au Mbaba.
Pia tafiti zinaonyesha kwa mwaka Mwanamke ana uwezo wa kuzaa uzao mmoja tu lakini Mbaba Akazaa hata 20 na zaidi kwa kuchovyachovya.Na hata family planning was supposed to go directly to men!!!!
So kwa kuwa baada ya kupachikwa na kukimbiwa na huyu kirukaruka mzigo anayeubeba ni mdada obviously lazima lawama abebe yeye( Mungu aje asaidie wanaume kwa siku zijazo wabebe mimba nao waone hii kadhia hakika hizi kashfa na dharau kwa Single Mothers zitakoma.
Sote twajua hulka nyingi za wamama ni ulezi na huruma
Anaona imetokea hivyo huyu kirukaruka kakimbia au hasomeki anawaza atoe azae amtupe???
Most of them wanakeep pregnancy na kuzaa na kulea baadaye mtoto yule anakuja kuwa hata A good leader or somebody.
Kabla hujamtupia Mawe Single mother angalia njia zake si wrote wanaweza na so wote waliopata kwa uhuni.
Pia chunguzeni hili Malaya na makahaba waliokubuhu kama wanabeba mimba!!!
Please please Acheni Mada hizo za kuwakashfu hawa Single mothers kwani wanayopitia sio rahisi kama mnavyodhani.
May God forgive and give them strength!