Pesa kwa me au ke?
 
Kila starehe ina gharama zake.
 
Wanaingilika kirahisi ila ukishapewa wana visa flan hivi

Ukitaka umroge mpende mwanae
 
Habari za Jumapili wakuu! Hongereni kwa Ibada kwa wale mlioenda ibadani👋👋

Lengo la mada hii, ni kukushauri na kukutia Moyo wewe Single mother uliejikatia tamaa. Mimi ni miongoni mwa single mother. Nilipata ujauzito nikiwa Form 4 nina miaka 17 tu! Nililelewa katika Familia ya kilokole na hata haya mambo ya kujiingiza kwenye Mahusiano ya kimapenzi sikuyataka kabisa but makundi& mzazi ndo vilisababisha hivi (nikipata muda nitaleta mada kuhusu hiki)

Baada ya Kujigundua ni mjamzito niliomba Rehema sana nikatubu Kwa Mungu ninakaendelea na masomo. Namshukuru Mungu mimba haikuonekana hadi Siku najifungua zilibaki siku 3 nianze Necta. Nakumbuka nilijifungua Ijumaa then j3 nikaingia Chumba Cha mtihani nikafanya paper nikatoka na 4 mbaya but Cheti nilipata.

Baada ya Hapo nilinuniwa na Mzee karibu Mwaka,nikaishi Maisha ya tabu sana Kiasi kwamba nilitamani kunywa Sumu nife ila nikawaza, kwani mm ndo nimekuwa wa Kwanza? Nikaamua kutokujichukia na kutokulia tena Nikaamua kuanza kufanya biashara na nikawa najiamini sana kama hakijatokea chochote, then Mzee akashauriwa akanipeleka Chuo but ile Caring haikuwepo!

Namshukuru Mungu nilifanikiwa kumaliza, nikatafuta Kazi na nikaamua kujisimamia mwenyewe,nikajithamini na Nikapata Kibali sanaa!

NINACHOTAKA NIKWAMBIE NI HIKI:- Wewe bado ni wa thamani hata kama una mtoto! Usijirahisirahisishe kwa Wanaume,eti Kisa ulishazaa!! Uthamani wako uko palepale

🖍️Usikate tamaa kwa Maneno yao au Kejeli zao,Focus kuitengeneza ile future uliyoipoteza hapo Awali.

🖍️Mrudie Mungu na uweke tumaini Kwake kikamilifu. Nina Uhakika atakupa Nafasi tena kama hautakuwa na Mchanganyo!! Kuwa na Msimamo Mungu atakupatia wa kwako!

Mwisho, achana na Uzinzi! Subiri Mume mwema Kutoka kwa Mungu (but kama utakuwa serious na Mungu)
 
Mkuu unajua wafrika tunapenda sana uongo na kufatijiana pasipo na ukweli.single mother anaweza kuwa na thamani katika mambo mengine lakini kuhusu swala la kuolewa ni uongo na tunadanganyana.

Sote tuna ndugu zetu na wengine Dada zetu walio single mother ukweli ni kuwa katika Wanaume 100 ambao wanataka kuoa ni Mwanaume 1 au 2 anayeweza kuoa mwanamke aliyezalishwa na kuachwa-hata wewe uliyetoa huu Uzi ungekuwa ni ME sidhani kama ungeweza kuoa Mwanamke aliyezalishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…