Mwanamke anayepata ushirikiano (child support) kutoka kwa mzazi mwenzie katika malezi ya mtoto nae pia ni singlemom?
 
Reactions: 511
Hii ni nadharia. Nilitegemea utupe uzoefu. Inaonesha wewe ni mwandishi tu huna uzoefu wa masuala haya
 
Reactions: 511
Tuna mifano mingi mitaani kwetu ila tuangalie mifano ya single mothers wafuatao katika picha hizi.

Monalisa na mwanae
Kajala na mwanae

Monalisa, mwanamama ambae safari yake haijagubikwa na skendo za ovyo ovyo na mwanae ambae hata sasa tunamuona katika mstari usio na skendo za kifala fala.

Kajala, mwanamama ambae safari yake imegubikwa na skendo za ovyo ovyo na mwanae ambae sasa amekuwa chronic wa skendo za kifala fala.

Single mothers mtalaumu wanaume kwa upande mkubwa, ila ndio imeshatokea, huyo mtoto utaishi nae. Kama una tabia za utapeli utapeli ambazo zilipelekea hadi bwana wako akuache, usipozibadilisha kitakacho fatia ni mtoto wako kuwa tapeli hata mara tatu zaidi yako.

Hii yote ni kuwa malezi ni ya upande mmoja, kwa hio jitahidi uache matabia yako ya ovyo ovyo ili umtengeneze mtoto ambae atakuwa chanya kwa upande mkubwa.

Wanaume pia, kama unamjua ex wako ni wa ovyo ovyo alafu anabaki na mtoto wako kwa ajili ya malezi, hesabu maumivu ndugu yangu, labda urudi mezani uangalie namna utapata shared custody.
 
Mtoto haangalii unachomwambia bali anafata unachofanya.
Kisaikolojia watoto wako hivo
.ukifeli kwenye matendo yako,umefeli kwenye malezi.

Mfano wewe unavaa nusu uchi kisha unamfokea mtoto kavae nguo ndefu,atabaki ubongoni anajiuliza kwanini mama avae nguo fupi mi nivae ndefu?utamcontrol lakini akija kubalehe na kupata uhuru atajiamulia.

Maji hufata mkondo
 
Haswaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…