Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 6,696
- 6,734
Wanabodi
Huu ni wito kwa Katibu Mwenezi mpya wa CCM, Comred Paul Makonda, kwanza kwa kumpongeza kwa kuifufua hamasa ya CCM kupendwa upya na kukubalika sana kupitia amsha amsha zake za Magufuli type (populist na populism) kila anapopita, tatizo lake ni moja tuu, anaipiga hii ngoma kwa nguvu mno, hivyo kuirindimisha kwa mlio mkubwa sana. Tatizo la ngoma inayovuma, ni ukiisikia ngoma inavuma sana, ujue inakaribia kupasuka!. Ili twende salama na kufika salama 2025, sisi watu wenye jicho la tatu, tunampa ushauri wa bure Mwenezi Makonda, twende taratibu mdogo mdogo ili tufike salama, kwa speed aliyoanza nayo, kama ataendelea kwa kasi hii, asije kushangaa hii ngoma ikampasukia njiani kabla hatujafika safari yetu!.
Wito huu ni kwa wanaomtakia mema Paul Makonda na ili kulithibitisha kuwa tunamtakia mema, angalia tumeanza nae wapi.
Mimi nilianza nae hapa Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Nikaja hapa Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe walilolikataa Waashi litafanywa kuwa Jiwe Kuu la Pembeni
Alipopitia misukosuko tukasimama nae kwanza kwa kutoa wito Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... kisha tukamshauri Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .
Kuna watu wenye roho za kwanini tukawaambia Wale mnaosubiri kwa hamu Makonda atumbuliwe, mtasubiri sana!. Ukiwa ni mpakwa mafuta, ni mpakwa mafuta!
Na mwisho nikapendekeza Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze...
Hivyo mheshimiwa sana Mwenezi Makonda, twende taratibu mdogo mdogo, hii duniani ni tambara bovu, tembea nayo taratibu!.
Wish you all the best
Kakayo
Paskali
Kweli Paskali...Ngoma ikilia sana hupasuka. Na mbwembwe ziwe na kiasi na staha.